Usiruhusu kurasa mbaya ya maisha imalize kuishi kwako

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
10,059
15,795
Kila mwanzo mpya huja kutoka mwisho wa mwanzo mwingine." ~Seneca

Ulimwengu unakutana na matukio mengi sana ya kutisha, hasa baadhi ya wanadamu kukatisha uhai baada tu maisha yao kupatwa na hali inayo nyong'osha. Ona maisha ni kitabu ambacho ndani yake wewe ndiyo muhusika mkuu, mara nyingi muhusika mkuu anapitia katika misukosuko mizito lakini katika hiyo bado anaishi, ona wewe ndiyo unapitia hiyo misukosuko lakini unatakiwa kuishi.

Katika maisha tunaweza kukutana na kurasa chungu, ni kurasa ambazo hatutakiwi kuziruka ili tuweze kuufahamu ukweli wa ushindi wa muhusika mkuu, ninaweza kukuambia kuwa maisha ni mabadiliko endelevu.

Katika maisha tunaweza kukutana na sura ya Kuachwa au kuacha, ni sura ambayo tunahitaji tu kuisoma, kwakua hutuonesha aina ya watu tunao changamana nao na jinsi tunavyo lazimika kuwaacha au hata kutuacha kuna wakati sababu tunazijua na kuna wakati sababu hatuzijui ila tunajikuta tu tukitimiliza sheria ya Falsafa ya Ukuaji katika sentensi za kujiambia maishani"Kila kitu kinabadilika"

"Mwisho wa uhusiano sio mwisho wa maisha. Ni nafasi ya mwanzo mpya. Ni kweli utateseka sana kwa ajili ya mtu huyo, lakini wakati mwingine mambo hayawezi kuwa kama yalivyokuwa hapo awali hata ujaribu kiasi gani. Katika kesi hii, itakuwa bora kufunga sura, kugeuza ukurasa na kuanza mpya." alisema Nelart

Hatupaswi kuishi katika maumivu hatupaswi kuishi katika zamani hii kwani itatuonesha hatuna thamani na kuona ulevi usio na mipaka ndiyo kimbilio halisi au hata kuona kujiua ndiyo kutuliza maumivu. Hatupaswi kujikimbia kwakua maisha yamejaa hali ya kushangaza sana. Usione umepoteza, usione huwezi kupata tena endelea kusoma kurasa za mbele usifunge kitabu cha maisha kwani utakatisha kuishi kwa muhusika

Tunaweza kukutana na kurasa ya Kukataliwa, pale tunapokutana na kurasa hii huwa tunajidharau sana, tunajiua kwa ndani kwakua tunakubali maoni sana ndiyo yatuoneshe usahihi na usio usahii, lakini maoni yote niya kweli lakini sio sahihi

Unahitaji kuendelea kusoma kurasa za mbele huku ukifahamu kila mtu atasema kwa jinsi yeye mtazamo wake ulivyo, hivyo katika kila mtazamo wa mtu utahitaji kuongeza na uwerevu wako. Sio kwakua ya mitazamo ya wengine unajiua kila fikra na kihisia endelea kugeuza karatasi kwakua hicho ndicho kinacho mjenga muhusika kuwa kweli ni muhusika mkuu

Usipoteze matumaini. Mwanzo unaweza kuwa mchungu kama mwisho, lakini kwa uchungu huo, unaweza kuzaa uzoefu mzuri ambao unakungojea karibu na kona. Kuna mambo mazito zaidi, ambayo yanaweza kukuangusha ukiwa utabaki katika kufunga kitabu cha maisha kisa kurasa hiyo tu.

Unahitaji kusoma kurasa ngumu maishani unahitajika kusoma kurasa za kifo cha wapendwa wako na hata kutokuwa na kazi au hata kufukuzwa kazi, unahitaji kusoma kurasa za kushindwa kwako mara nyingi, unahitaji kusoma ili tu maisha yasikurudishe katika sura hiyo hiyo unayo ifunga. Isome tu usiifunge kwa kujiua, kujiua kisa ya kurasa hiyo ni dhambi ya Ubinafsi. Unahitajika kusoma kurasa hiyo na kusonga mbele

Usimsukumie mwingine kurasa yako endelea kuisoma huku ukisema nina nguvu zaidi kuliko chochote ulichochukua kutoka kwangu na sitakupa umiliki wa maisha yangu, kupitia fikra na hisia zangu. Nataka ujue kuwa utapitia nyakati hizi ngumu.

Anasema Adam Bergen "Wakati maisha hayaendi kwenye mpango, ni lazima tukubali mabadiliko na kutambua kwamba maisha yetu yana sura nyingi; moja imeisha na nyingine inakaribia kuanza.

Lakini hatuwezi kuendelea na sura inayofuata ikiwa tutaendelea kusoma tena za zamani. Tunapaswa kukubali kwa hiari kwamba maisha yanaendelea, na kwamba tuna nafasi ya kuunda kitu kikubwa na bora zaidi"

Usikubali sura mbaya iwe kikwazo cha wewe kuifikia sura mpya.Tunahitaji kukubali ukweli na kupunguza taraja kuu kuu ili tuendelee mbele kwa utulivu. Maisha yatatupa mengi tusome ili tujifunze.

Unahitaji kuziweka vizuri hizi sentensi tatu katika maisha yako 1.Maisha hutokea kwa faida yako si dhidi yake, 2. Kila kitu huponya kwa muda wa kutosha 3. Haina maana kuendelea kupinga.

"Maishani tunahitaji kuupata uzoefu wa ubinadamu"

SEKOMBA NGOVI
 
Asante sana mkuu!
 
Back
Top Bottom