Maandamano yaitishwe nchi nzima kupinga upigaji madili kupitia mgao wa wa Umeme. Waziri Makamba alituambia tuna ziada ya MW 1400. Huu mgao wa nini?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Hapa tunaibiwa kiwaziwazi kabisa.

Yaani mkuu wa wizara anayehusika na umeme anatamka wazi kuwa tuna ziada ya Mw 1400.

Halafu ghafla naibu wake anadai kuna upungufu!

Halafu mgao unatamalamaki nchi nzima.

Tuandamane kupinga huu wizi. Tuandamane watanzania.
 
Watawapiga hao majizi. Huyu mama kiukweli anayumba japo hawamwambii ukweli.
 
Hayo maandamano hayatawezekana kwasababu zifuatazo

1-Hatuna umoja. Wakati wewe unaona uchungu nchi kuwa gizani na kukosa maji, upande wa pili kuna maelfu ya vijana (chaws) wapo tayari kutetea upuuzi wawanaoitwa viongozi kwa ujira wa vipesa vidogo tu.

2-Maandamano hayaonyeshi wazi nini hasa kitafanikiwa baada ya hayo maandamano? Au ndiyo kuandamana tu? Halafu ikifika jioni unarudi nyumbani? Sasa tutakuwa tumefanikiwa nini hapa?

3-Maandamano kuwa na itikadi za kichama badala ya ajenda zinazolenga kutatua kweli changamoto zetu wadanganyika. Na hii inaturudisha kwenye point namba moja, tunagawanyika. Ujinga mtupu.

4-Watu wanaoguswa na tatizo la ukosefu wa umeme na maji na kweli wanasikia maumivu ni idadi chache tu yawatanzania. Idadi kubwa ya watu hawana kazi zinazohitaji umeme kwahiyo hawawezi kuona umuhimu sana.

Watanzania watakuwa tayari kudai maendeleo yenye tija mpaka siku ile…ile siku.

Wanasiasa watakapoanza kushika wananchi makalio.
 
Umesema vizuri. Kwenye point no.4 ukiona umeme umegusa wengi ujue ni mechi ya simba na Yanga. Na wao ni wajanja kidogo kwenye hizi mechi wanajitahidi sana umeme usikate. Sisi wa kuhurumia
 
Huo mgao tuandamane kisa mikoa michache?? Mbona hatuandamani kushinikiza KIGOMA WAJENGEWE BARABARA NZURI?
 
Back
Top Bottom