STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Usipate shida mkuu, ni typo.
wamefulia, hawana hela ya kuwapa watu na kukodi magari ya kuwabebea watu. tumebana mifereji yao yote ya kupatia hela.
Usipate shida mkuu, ni typo.
hiki chama kiitwacho CCCM kimesajiliwa na Tendwa au ni saccoss hiiKwa kuwa CDM wanatumia haki yao ya kikatiba kuzunguka nchi nzima kutangaza sera zao na msingi wao juu ya hali mbaya ya umeme, ugumu wa maisha na kadhalika haina budi kwa CCCM na wao kuzunguka nchi nzima kutumia majukwaa na maandamano kujibu hoja na tuhuma za CDM na kuwaeleza wananchi wanampango gani katika kutatua kero zao, na kwa kuanzia waende kanda ya ziwa kufuta nyayo za CDM na wafanye hivyo hivyo kwa mikoa mingine ambayo CDM watafanya maandamano na mikutano ya hadhara.
Lakini angalizo langu ni jee, nani katika CCCM mwenye mvuto na anayekubalika na watanzania ambaye atazunguka Tanzania nzima kujibu tuhuma na hoja za CDM, je CCCM watapata mahudhurio makubwa kama wanayopata CDM na je mwitikio wa maandamano na mikutano ya hadhara ukiwa mbaya hii itatufundisha nini?
Je mwenyekiti na katibu wa CCCM wako tayari kuchukua jukumu hili na kuzunguka Tanzania nzima kujibu hoja za CDM kwa wananchi.
Nawakilisha.
CCCM bila shaka chama kipya hiki ila sijawahi kisikia, wanaanza lini waandamano? Na viongozi wake ni akina nani?
Kuna tetesi kuwa chama cha mapinduzi kitaitisha maandamano makubwa nchi nzima mara baada ya kikao cha halmashauri kuu baadaye mwezi huu. Maandamano hayo yataanzia Singida Mjini, halafu Dodoma, Morogoro, Tabora, Lindi, Mtwara na kuishia Temeke Dar. Lengo ni kupima kama athari za vuguvugu la CDM limefika hadi katika mikoa hii ambayo ni ngome yake ya miaka mingi. Hakutakuwa na kuwabeba watu kwenye malori isipokuwa watu watahamasishwa tu kuhudhuria. Hata wanamuziki wa bongo fleva hawataalikwa.
Source: Ofisi ya katibu mkuu CCM makao makuu.