Maandamano kupinga mgawo wa umeme yanukia

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Maandamano kupinga mgawo wa umeme yanukia
Send to a friend
Thursday, 30 June 2011 20:42
0digg

Kizitto Noya, Dodoma
MAANDAMANO makubwa ya kupinga mgao wa umeme nchini yanaweza kutokea wakati wowote kuanzia sasa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alilieleza Bunge jana.

Mnyika alisema hayo baada ya kuomba mwongozo wa spika na kuuliza sababu za maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu, hayakuwapo katika siku ya jana kama inavyofanyika katika kila Alhamisi.

Kwa mujibu wa Mnyika, maswali kwa waziri mkuu ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa, linapita katika matatizo mbalimbali likiwamo la mgao wa umeme na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu.

Alisema kuondoa utaratibu huo bila maelezo ya kuridhisha, ni kutowatendea haki Watanzania ambao wangependa kusikia kauli ya serikali kuhusu matatizo hayo.


"Mheshimiwa mwenyekiti, kanuni ya 30 kanuni ndogo ya 6 inahalalisha Bunge kuwa na maswali kwa waziri mkuu, na imesema maswali hayo hayatakuwepo endapo tu waziri mkuu hayupo. Lakini leo (jana) tunamwona waziri mkuu yupo na maswali hayo hayapo,"alisema

"Mheshimiwa mwenyekiti, wakati wowote kutakuwa na maandamano makubwa ya watu kupinga bei ya umeme, wamenitumia ujumbe kwa njia ya simu kututaka Chadema tuandae maandamano hayo na leo (jana) ningepata fursa kumuuliza waziri mkuu kuhusu suala hilo ili wananchi wapate majibu ya moja kwa moja."


"Kuna mambo kama wanafunzi Udom kuanza kurudishwa kwa kutumia itikadi za kisiasa, tumezisoma kwenye vyombo vya habari na leo (jana) ilikuwa siku pekee kwa waziri mkuu kutoa kauli ya serikali,"alisema.


Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawane, alipuuza maelezo hayo ya Mnyika akisema wabunge wana nafasi nyingi za kuwasiliana na serikali zaidi ya kumuuliza waziri mkuu maswali ya hapo kwa hapo.

"Waheshimiwa wabunge, kama tulivyosema wiki iliyopita kwamba kwa kuwa Bunge linajadili makadirio ya waziri mkuu, tukaona ni vyema tumwache asikilize vizuri hoja zetu ili atoe majibu ya usahihi. Lakini, wabunge wana njia nyingi za kuwasiliana na serikali. Kama mheshimiwa mbunge unaona kuna jambo la dharura, unaweza kutumia nyingine kuwasilisha hoja hiyo kwa waziri mkuu.

Jana ilikuwa wiki ya pili mfufulizo kwa Bunge kusitisha maswali ya hapo kwa papo kwa waziri mkuu. Mara ya kwanza ilikuwa Alhamisi iliyopita.
 
Back
Top Bottom