MAANDAMANO ARUSHA: Wanafunzi Wa Sekondari Iliboru Wanaandamana.

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,995
2,494
Wanafunzi wa sekondari ya Iliboru wanaandamana.

Wametoka shuleni mpaka ofisi za mkuu wa mkoa Arusha mjini. Wamefukuzwa na Polisi wamerudi mpaka geti Kuu la Kuingia AICC na kuna polisi wakutosha. Na polisi wengine wanaongezeka.

Madai yao sijaweza kujua ni nini haswa lakini mabango yote yanaelezea kuwa
"Hatumtaki Mwalimu Mkuu"
"Aondoke aende zake"

AICC kuna mkutano mkubwa unaendelea na wanafunzi wameona ndio mahali sahihi ya kuchukua Attention.

Nawasilisha.
 
Tunashukuru kwa taarifa,ingekuwa vema zaidi kama ungepata japo picha na utuwekee hapa tuone nini kinajiri huko.
 
Safi sana wazee wa vipaji maalumu! Kama bwai mbwai komaeni hapo hapo AICC na kama haitoshi wengine wasogee nyumbani kwa mkuu wa mkoa hapo road ya aicc mkacheze basketball uwanjani kwake.
 
Wanafunzi wa sekondari ya Iliboru wanaandamana.

Wametoka shuleni mpaka ofisi za mkuu wa mkoa arusha mjini. Wamefukuzwa na Polisi wamerudi mpaka geti Kuu la Kuingia AICC na kuna polisi wakutosha. Na polisi wengine wanaongezeka.

Madai yao sijaweza kujua ni nini haswa lakini mabango yote yanaelezea kuwa
"Hatumtaki Mwalimu Mkuu"
"Aondoke aende zake"


AICC kuna mkutano mkubwa unaendelea na wanafunzi wameona ndio mahali sahihi ya kuchukua Attention.

Nawasilisha.

Hivi si ni Andrew Kwayu? Au Mwingine? Kama ni Kwayu atakua amebadirika kweli?
 
Mkuu mkoa wa Arusha anaishi juu kidogo ya mahakama ya mkoa, pembezoni mwa hotel ya Mount Meru.
 
Inakuja siku mfungwa atachagua gereza kama si bwana jela!!! Nyie subirini tu, hizi tabia za kupandikiza maviongozi kwenye taasisi!!!! mh!
 
Haya ni matokeo ya kutapakaa kwa viongozi wanaoendekeza dhuluma, kiburi na matakwa binafsi katika utendaji wao hali ya kuwa wamepewa dhamana ya kusimamia maslahi ya umma. Napenda sana hii spirit ya maandamano kwa vijana, kwani inanipa faraja kuwa itakapofika zamu yao kuongoza watakuwa wanaheshimiana sababu wanajua ukiboronga tu unawaongoza wataandamana wakung'oe madarakani.
 
Tunashukuru kwa taarifa,ingekuwa vema zaidi kama ungepata japo picha na utuwekee hapa tuone nini kinajiri huko.


Niko na simu plus nilisimama kidogo sana. AICC ni eneo lindwa sana tena wakati kama huu wa mikutano mikubwa.
 
UPDATES:
Japo polisi wameongezeka zaidi tokea kipindi kile na-update, vijana wanaongezeka na bado wamekaa pale Lango la AICC opposite na Geti la Mount Meru Hosp.

Walinzi wa ICTR wako makini langoni mwao.
 
dah my old school...itakua tu kuna jambo si sawa hapo ilboru...hawawezi andamana for nothing.
 
dah my old school...itakua tu kuna jambo si sawa hapo ilboru...hawawezi andamana for nothing.

sijui wamegomea nini ? au chui ?

haaa haaa .... nilikuwa Bweni la Hanang ... miaka ileee 92 .. onwards A-level
 
hata matokeo ya ilboru yanatisha sio mazuri nadhani kuna tatizo iliboru nayoijua enzi zile tupo Mtwara tech
 
sijui wamegomea nini ? au chui ? haaa haaa .... nilikuwa Bweni la Hanang ... miaka ileee 92 .. onwards A-level
nasikia siku hizi hawali chui sana...nadhani itakua tu mambo ya kitaaluma,dah sijui ule mto umekauka pale bondeni?? "ofisi ya MALI HAI" hahahahahaah...
 
Chama langunkomaeni vijana mpaka kieleweke!
Bse huwa ninaamini several people hawawezi andamana kwa kitu cha kipumbavu there must be something genuine that hurts many
 
Back
Top Bottom