Maana ya neno Tasnia

simply,ni "nyanja"eg wabongo weng wamejikita ktk tasnia ya filamu/bongofleva=wabongo weng wamejikita ktk nyanja ya filamu/bongofleva.
 
Tasnia ni FIELD kwa kiingereza. Mfano, wadau wote wa tasnia ya uhandisi wanaalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi.
 
Nimeona gazetini tangazo la Bodi ya Korosho, wameandika .....TASNIA YA KOROSHO...
Binafsi natatizika kidogo na matumizi sahihi ya neno hili.
 
Tasnia ni jumla ya rasilimali na watu wanaozalisha, wanaonunua, wanaonufaika na wanaosaidia mrengo fulani wa huduma/kazi/taaluma.

Kwa mfano tukisema tasnia ya filamu tunamaanisha wazalishaji, wateja, wasambazaji, serikali pamoja na rasilimali wanazotumia kuzalisha, kusambaza na kufikisha bidhaa ambayo ni filamu.
 
Back
Top Bottom