Maamuzi ya Nyerere kutuingiza AU, SADC, EAC na hatimaye Muungano yatatutesa hadi kiama. Nini kifanyike?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Ukweli usemwe

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa katika uongozi wake yapo mambo mazuri alifanya na pia yapo ya kipuuzi ambayo alifanya. Akaendelea kusema anashangaa wanaomfuatia wanayaacha yenye tija na kuendeleza yale mabaya yake.

Katika mambo ya kipuuzi aliyoyafanya mojawapo ni lile la kuipeleka nchi kwenye Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ambayo sasa inaitwa Umoja wa Afrika (AU) bila kuzingatia utashi na maamuzi ya wananchi.

Ikumbukwe kipindi hiko, Mwalimu alikuwa anaungwa mkono hata na watoto wadogo hivyo angepeleka jambo la kujiunga na jumuia za kikanda wangepiga kura na kumbukumbu ingebaki. Lakini maamuzi yake aliyoyafanya kwa niaba ya Taifa zima hayakuzingatia utashi wa nchi na kiukweli hata Katiba yetu hairuhusu jambo hilo. Katiba ipo kimya kama ilivyonyamazishwa na waliyoiandika.

Sambamba na hilo, uamuzi wa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ni mufilis endapo utaratibu haukufuatwa. Sidhani kama wananchi enzi hizo waliulizwa na kuridhia kupitia kura kabla ya Nyerere na Karume kuungana. Leo tuna muungano unaolindwa kwa mtutu wa bunduki na wizi wa kura. Muungano ambao viongozi wanaapa kuulinda kwa sababu una maslahi kwao na si kwa wananchi.

NINI KIFANYIKE
Mzee wa Msoga aliwahi kusema kwenye kikao cha wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki kuwa, kabla ya kupata Rais mmoja wa Jumhiya ni sharti wananchi waulizwe kwanza.

Pamoja na mapungufu kadha wa kadha yanayozungumzwa dhidi ya JK, lakini hili la kurudi kwa wananchi kupata ridhaa ni jambo ambalo hakuna rais wa Afrila aliwahi siyo kusema tu, bali hata kuliwaza.

Nashauri, serikali ianze mchakato wa kura za maoni kuhusu sisi kujiunga jumuiya zote za kikanda yaani
AU (African Union)
SADC (Southern African Developing Countries)
EAC (East African Comunity)
ADB
OIC (YKWIM)
Na zingine ambazo wametupeleka huko kama misukule.

Bunge lisitumike kama mhuri wa kufanya maamuzi yanayohitaji utashi wa wananchi ambao ndiyo wenye nchi

Kinyume na hapo, hizo jumuiya zina manufaa makubwa kwa viongozi badala ya kunufaisha nchi.

CC: Gwappo Mwakatobe FaizaFoxy zitto junior Pascal Mayalla Erythrocyte Mzee Kigogo Retired raraa reree Extrovert Mdude_Nyagali Depal Mamndenyi Joannah Mzee Mwanakijiji funzadume Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume
 
Hapa chochote kinaweza kufanyika na kikafanyika vizuri tuu lakini ni mpaka kwanza tuitoe ccm madarakani bila hivyo tutegemee blahblah za kufa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa, tatizo ni CCM

Hata aje malaika hatoweza kuirejesha relini.

Chama hiki kinahitaji kuzaliwa upya yaani kikae pembeni kijitafute na kujiunda
 
Ukweli usemwe

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere

Katika mambo ya kipuuzi aliyoyafanya mojawapo ni lile la kuipeleka nchi kwenye Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ambayo sasa inaitwa Umoja wa Afrika (AU) bila kuzingatia utashi na maamuzi ya wananchi.
Duh... !.
Kiukweli somo la Uumajumui wa Pan Africanism linahitajika sana kwa Watanzania!. Mwalimu Nyerere alikuwa ni Pan Africanist, alikuwa yuko tayari hata kuchelewesha uhuru wa Tanganyika ili tuwasubirie wengine!. Si wengi wanajua hata WB, IMF ni regional blocks, Gaddafi alitaka tuanzishe AB na AMF kuachana na WB na IMF, mabeberu wakampoteza!. Africa is the richest continent, kwanini tuwategemee WB na IMF?

Sasa tumeanzisha Afcfta ili Waafrika tununue bidhaa za Africa na kuinuana na sio kutegemea bidhaa za mabeberu. Huhitaji kuwauliza wananchi kujiunga na regional blocks.

Ila muungano, Bunge la Tanganyika liliridhia, hivyo Watanganyika tulishirikishwa, ila Zanzibar, ndio hawakushirikishwa!.

P
 
Baada ya Nyerere kuachia ngazi na kutwaliwa na Yehova, nyie mmefanya kipi tofauti na wizi, rushwa, ufisadi , kuuza raslimali za Taifa na kujilimbikizia mali?.

Tunaishi kwa umoja makabila yote Tanganyika kwa sababu ya Nyerere.
Hebu tuambie waliofuata baada yake wana kipi cha kujivunia kama Taifa kwa ujumla walichofanya?.

Wewe kama wewe Msanii umelifanyia nini Taifa hadi sasa kabla ya kuhoji wengine?
 
Ukweli usemwe

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa katika uongozi wake yapo mambo mazuri alifanya na pia yapo ya kipuuzi ambayo alifanya. Akaendelea kusema anashangaa wanaomfuatia wanayaacha yenye tija na kuendeleza yale mabaya yake.

Katika mambo ya kipuuzi aliyoyafanya mojawapo ni lile la kuipeleka nchi kwenye Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ambayo sasa inaitwa Umoja wa Afrika (AU) bila kuzingatia utashi na maamuzi ya wananchi.

Ikumbukwe kipindi hiko, Mwalimu alikuwa anaungwa mkono hata na watoto wadogo hivyo angepeleka jambo la kujiunga na jumuia za kikanda wangepiga kura na kumbukumbu ingebaki. Lakini maamuzi yake aliyoyafanya kwa niaba ya Taifa zima hayakuzingatia utashi wa nchi na kiukweli hata Katiba yetu hairuhusu jambo hilo. Katiba ipo kimya kama ilivyonyamazishwa na waliyoiandika.

Sambamba na hilo, uamuzi wa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ni mufilis endapo utaratibu haukufuatwa. Sidhani kama wananchi enzi hizo waliulizwa na kuridhia kupitia kura kabla ya Nyerere na Karume kuungana. Leo tuna muungano unaolindwa kwa mtutu wa bunduki na wizi wa kura. Muungano ambao viongozi wanaapa kuulinda kwa sababu una maslahi kwao na si kwa wananchi.

NINI KIFANYIKE
Mzee wa Msoga aliwahi kusema kwenye kikao cha wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki kuwa, kabla ya kupata Rais mmoja wa Jumhiya ni sharti wananchi waulizwe kwanza.

Pamoja na mapungufu kadha wa kadha yanayozungumzwa dhidi ya JK, lakini hili la kurudi kwa wananchi kupata ridhaa ni jambo ambalo hakuna rais wa Afrila aliwahi siyo kusema tu, bali hata kuliwaza.

Nashauri, serikali ianze mchakato wa kura za maoni kuhusu sisi kujiunga jumuiya zote za kikanda yaani
AU (African Union)
SADC (Southern African Developing Countries)
EAC (East African Comunity)
ADB
OIC (YKWIM)
Na zingine ambazo wametupeleka huko kama misukule.

Bunge lisitumike kama mhuri wa kufanya maamuzi yanayohitaji utashi wa wananchi ambao ndiyo wenye nchi

Kinyume na hapo, hizo jumuiya zina manufaa makubwa kwa viongozi badala ya kunufaisha nchi.

CC: Gwappo Mwakatobe FaizaFoxy zitto junior Pascal Mayalla Erythrocyte Mzee Kigogo Retired raraa reree Extrovert Mdude_Nyagali Depal Mamndenyi Joannah Mzee Mwanakijiji funzadume Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume
Hebu nitajie Taifa lolote duniani kote ambalo halina jumuiya yoyote ya ushirikiano?
 
tabia ya kutag watu imerudi tena? basi kwa maoni yangu ambayo mleta mada hulazimishwi kuyazingatia ni kwamba jumuiya za kikanda zipo kisiasa SADC hawana hata mtandao wa barabara wa kujivunia unaounganisha nchi zote wala reli ya kisasa, hata biashara baina ya nchi hizi (SADC, EAC na AU) zimejaa vikwazo utafikri tunafanya biashara na watu na mabara mengine. Zanziba ni pigo kwa watanganyika prevelege anazopata mzanzibar awapo Tanganyika ni kinyume kabisa ya kile Mtanganyika anapata awapo visiwani. Nyerere alikuwa mtu mwenye upeo mdogo sana.
 
Duh... !.
Kiukweli somo la Uumajumui wa Pan Africanism linahitajika sana kwa Watanzania!. Mwalimu Nyerere alikuwa ni Pan Africanist, alikuwa yuko tayari hata kuchelewesha uhuru wa Tanganyika ili tuwasubirie wengine!. Si wengi wanajua hata WB, IMF ni regional blocks, Gaddafi alitaka tuanzishe AB na AMF kuachana na WB na IMF, mabeberu wakampoteza!. Africa is the richest continent, kwanini tuwategemee WB na IMF?

Sasa tumeanzisha Afcfta ili Waafrika tununue bidhaa za Africa na kuinuana na sio kutegemea bidhaa za mabeberu. Huhitaji kuwauliza wananchi kujiunga na regional blocks.

Ila muungano, Bunge la Tanganyika liliridhia, hivyo Watanganyika tulishirikishwa, ila Zanzibar, ndio hawakushirikishwa!.

P
Mkuu Paskali
Sikatai nia njema ya Nyerere lakini ninachokikosoa ni njia kufikia huko.

Kwa nini tulikuwa tunafanya uchaguzi ilihali tulikuwa tunampenda sana?

AU ni kichaka cha viongozi wa Afrika au klabu ya Addis. Kila jqmbo ambalo AU inafanya linahitaji baraka ya jumuia za kikanda za magharibi. Angalia hiko walikoendelea jumuiya zao zote zinahitaji nchi husika ipate ridhaa ya wenye nchi. Tusingeiona BREXIT leo endapo
 
Ukweli usemwe

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa katika uongozi wake yapo mambo mazuri alifanya na pia yapo ya kipuuzi ambayo alifanya. Akaendelea kusema anashangaa wanaomfuatia wanayaacha yenye tija na kuendeleza yale mabaya yake.

Katika mambo ya kipuuzi aliyoyafanya mojawapo ni lile la kuipeleka nchi kwenye Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ambayo sasa inaitwa Umoja wa Afrika (AU) bila kuzingatia utashi na maamuzi ya wananchi.

Ikumbukwe kipindi hiko, Mwalimu alikuwa anaungwa mkono hata na watoto wadogo hivyo angepeleka jambo la kujiunga na jumuia za kikanda wangepiga kura na kumbukumbu ingebaki. Lakini maamuzi yake aliyoyafanya kwa niaba ya Taifa zima hayakuzingatia utashi wa nchi na kiukweli hata Katiba yetu hairuhusu jambo hilo. Katiba ipo kimya kama ilivyonyamazishwa na waliyoiandika.

Sambamba na hilo, uamuzi wa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ni mufilis endapo utaratibu haukufuatwa. Sidhani kama wananchi enzi hizo waliulizwa na kuridhia kupitia kura kabla ya Nyerere na Karume kuungana. Leo tuna muungano unaolindwa kwa mtutu wa bunduki na wizi wa kura. Muungano ambao viongozi wanaapa kuulinda kwa sababu una maslahi kwao na si kwa wananchi.

NINI KIFANYIKE
Mzee wa Msoga aliwahi kusema kwenye kikao cha wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki kuwa, kabla ya kupata Rais mmoja wa Jumhiya ni sharti wananchi waulizwe kwanza.

Pamoja na mapungufu kadha wa kadha yanayozungumzwa dhidi ya JK, lakini hili la kurudi kwa wananchi kupata ridhaa ni jambo ambalo hakuna rais wa Afrila aliwahi siyo kusema tu, bali hata kuliwaza.

Nashauri, serikali ianze mchakato wa kura za maoni kuhusu sisi kujiunga jumuiya zote za kikanda yaani
AU (African Union)
SADC (Southern African Developing Countries)
EAC (East African Comunity)
ADB
OIC (YKWIM)
Na zingine ambazo wametupeleka huko kama misukule.

Bunge lisitumike kama mhuri wa kufanya maamuzi yanayohitaji utashi wa wananchi ambao ndiyo wenye nchi

Kinyume na hapo, hizo jumuiya zina manufaa makubwa kwa viongozi badala ya kunufaisha nchi.

CC: Gwappo Mwakatobe FaizaFoxy zitto junior Pascal Mayalla Erythrocyte Mzee Kigogo Retired raraa reree Extrovert Mdude_Nyagali Depal Mamndenyi Joannah Mzee Mwanakijiji funzadume Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume
Punguza Konyagi we Mzee unaelekea kubaya
 
Ndio maana mnaongea pumba kama kina Lisu eti mtu akihundua Madini yawe yake 😆😆😆😆😆😆🤣🤣🤣🤣
Lisu yupo sahihi. Kuiboresha hoja yake ningesema mwenye eneo lazima awe mwanahisa kwenye mradi wa uchimbaji kwa mgawanyo ufuatao
Serikali 50%
Mwekezaji 43%
CSR 4%
Mmiliki wa eneo 3%

Kwa kuanzia
 
Back
Top Bottom