Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,968
- 955
MHE. MUNDE TAMBWE APIGILIA MSUMARI MAAMUZI YA TIMU YA MAWAZIRI NANE NA BARAZA LA MAWAZIRI KUHUSU UGAWAJI MAENEO KALIUA
Mbunge Viti Maalum Wanawake Mhe. Munde Abdallah Tambwe amemshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii kwa tamko lake la kusema Maamuzi ya Timu ya Mawaziri Nane (08) ya Baraza la Mawaziri yaheshimiwe.
"Kaliua kuna tatizo kubwa la Vijiji vya Usinga na Kakoko, Vijiji vilipitiwa na timu ya Mawaziri Nane ambao walisema wananchi waongezewe eneo kwa sababu Kaya 1300 wanaambiwa zihamishwe" - Mhe. Munde Abdallah Tambwe
"Nimemsikia Waziri wa Maliasili na Utalii anasema yale yote yaliyosemwa na Timu ya Mawaziri 8 na Baraza la Mawaziri yaendelee kuwa vilevile" Amesema Mhe. Munde Abdallah Tambwe, Mbunge wa Viti Maalum UWT
"Tuna Mbuga ya Ugala lakini hakuna hoteli nzuri, hatuna Barabara ya kutupeleka Ugala, hakuna Mawasiliano kwa maana ya Simu. Tunaomba Waziri wa Maliasili na Utalii uliangalie hilo. Pia, mtuunganishe na Ofisi za Utalii za Arusha watu wakija Tabora waelekezwe mahali Ugala ilipo" - Mhe. Munde Abdallah Tambwe, Mbunge wa Viti Maalum UWT
Mhe. Munde Tambwe amesema jambo hilo la kuwahamisha watu lilikuwa linaleta taswira mbaya kwa kuwa kulikuwa na mpango wa kuhamisha wananchi wa Ukumbikakoko na Usinga ambalo lilikuwa kinyume na maamuzi ya timu ya Mawaziri 8 na Baraza Ia Mawaziri la kusema wananchi waishi na kuongezewa eneo.