Maamuzi magumu ya mimi mkweche kwa nafasi ya ubunge 2015!

MKWECHE

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
299
64
Ki-Ukweli Cheo/nafasi/kazi ya Ubunge ni nafasi nyeti, kadhalika ni fursa Adimu sana ya kuwatumikia wananchi wote Jimboni. Ukiwa na kazi kubwa ya kujitoa na kujituma katika kuwaelekeza wananchi namna nzuri na mwafaka ya kupata Mandeleo katika eneo husika na kwa kutumia Rasilimali zote zilizopo, sambamba na maendeleo kuhakisha na kufuatilia huduma na ahadi za serikali zawafikia bila mawaa, nk.

Nikienda mbali zaidi nafasi ya Ubunge ni ya Kujitolea kutumikia zaidi ya Kutumikiwa na ndio maana Kuna 'Kamsemo ka Nimeombwa nigombee'
Maamuzi yangu Magumu ni kwamba Kuanzia Mwaka 2015 Ubunge kiwe cheo cha Kujitolea,Isiwe Kazi ya Mushahara Zaidi ya Kujitolea Kuongoza wananchi bila malipo, hasa baada ya Kuguswa na Changamoto zinazowakabili. Isiwe Kazi ya mvuto wa-Mshahara wake Mnono na Marupurupu!

Kitendo cha mtu tena Msomi, mathalan Professor au Doctor wa University au Hata Mkurugenzi wa Shirika Pevu anaamua kuacha Kufundisha au Kazi yake nzuri na Kwenda Jimboni kufanya kazi isiyo na Malipo itakuwa kweli Amekereketwa na Maendeleo ya watu wake na amekuja kutumikia!

Wengine watasema sasa atafanyaje kazi!Kama Akiwa bungeni apewe stahiki za safari na kuishi kule kikaoni na baadae nauli!
Akiwa Jimboni akitaka kwenda kutembelea wananchi atapewa gari la Halmashauri,Akitumia gari lake mafuta anaweka mwenyewe!

Jamani Kujitolea na kutumikia wananchi kwa vitendo sio Lelemama ni wajibu mzito
Hapo vipi Wadau!Haya ndio Maamuzi magumu ya kuanzia kwenye medani SIASA kwa Mimi Mwa-Mkweche!
 
wewe utakuwa ni rostam/lowasa/chenge sasa hapo huoni bunge litajaa matajiri
Khaa!Ngugu ndio imekuwa haya tena!Kwani kwa Mtazamo wako matajiri ndio watu wa kujitolea!Bahati mbaya wabunge matajiri siwajui ila sina hakika kama wameingia kwa kujitolea!Naomba Utulie na Kupima Uzito wa Kujitolea!
Mie Mwa-Mkweche lakini!
 
sasa nani ataweza kufanya kazi bila malipo, hiyo kazi itakuwa ni Mkweche!
Mbona Mabalozi wa nyumba kumi hawalipwi na kazi za kutumikia wananchi wanafanya tena ndio wapo karibu!
Unafikiri nguvu nyingi na minyukano ya kupata jimbo yaletwa na Kiu ya Kitumikia wananchi?
 
Back
Top Bottom