Maalim Seif ziarani Marekani - akutana na Mabalozi wa nchi mbali mbali

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na balozi wa Cape Verde nchini Marekani bibi Fatima Veiga (kushoto). Wa pili kushoto ni balozi wa Tanzania nchini Marekani bibi Mwanaidi Maajar na kulia ni afisa ubalozi wa Tanzania nchini humo Suleiman Saleh.

Balozi Jorge Hernandez wa Honduras (katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko nchini Marekani. Kulia ni Balozi wa Brazil nchini Marekani, Mauro Vieira.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Syracuse cha mjini New York Dr. Horace Campbell. Dr. Horace aliwahi kuwa mkufunzi wa siku nyingi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka nchi mbali mbali duniani wanaoziwakilisha nchi zao nchini Marekani. Mabalozi hao kutoka kushoto ni balozi Harold Foresyth (Peru), Balozi Mauro Vieira (Brazil) na Balozi Jorge Arguello (Argentina).

Balozi wa Msumbiji nchini Marekani (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko Marekani. Kulia ni balozi wa Cape Verde bibi Fatima Veiga. (Picha zote na mpiga picha maalum, New York).

Na Mwandishi Maalum, Marekani

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na mabalozi wa nchi mbali mbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Marekani na kubadilishana mawazo juu ya masuala tofauti yakiwemo ya kiuchumi, afya na teknolojia ya habari.

Katika mazungumzo yake na balozi wa Malaysia nchini Marekani bwana Othman Hashim, Maalim Seif amesema Zanzibar inaweza kushirikiana na Malaysia katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu ya juu, biashara, uwekezaji na kilimo.

Maeneo mengine ambayo Zanzibar na Malaysia zinaweza kushirikiana ni teknolojia ya habari, benki za kiislamu na utalii. Katika mazungumzo hayo viongozi hao pia wamekubaliana juu ya suala la kufuatilia mazungumzo hayo ambapo Zanzibar itatuma maofisa wake nchini Malaysia, ili kuona namna ya kukuza mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.

Kabla ya kukutana na mabalozi hao, Makamu wa Kwanza wa Rais alipata fursa ya kushiriki kwenye mikutano na makongamano mbali mbali juu ya mambo ya siasa na mahusiano ya kimataifa yaliyoandaliwa na taasisi ya National Democratic Institute mjini North Carolina, Marekani.

Makamu wa Kwanza wa Rais pia amefanya mazungumzo na mkuu wa taasisi inayojishughulisha na utoaji wa misaada ya vifaa vya hospitali katika nchi mbali mbali duniani Bwana Abdul Makembe Kimario.

Katika mazungumzo yao viongozi hao walijadiliana juu ya uwezekano wa Zanzibar kuweza kufaidika na misaada hiyo ya vifaa vikiwemo vitanda vya kulazia wagonjwa, vitanda maalum vya kufanyia upasuaji na mashine za uchunguzi wa maradhi mbali mbali katika hospitali zake za Wilaya na hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa misaada ya vifaa vya hospitali kwa zaidi ya nchi 124 duniani zikiwemo China, India na Israel.

Maalim Seif pamoja na viongozi na mabalozi wa nchi mbali mbali pia walihudhuria katika kongamano maalum, ambapo walishuhudia viongozi wa vyama vya Republican na Democratic vya nchini Marekani wakihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 6 mwaka huu nchini humo, ambapo chama cha Demcratic kinawakilishwa na Rais wa sasa wa Marekani Rais Barack Obama na chama cha Republican kinawakilishwa na Bwana Mitt Romney.

Makamu wa Kwanza wa Rais aliwasili nchini Marekani tarehe 02 mwezi huu kwa ziara ya kikazi.

Katika uwanja wa ndege wa New York alipokelewa na Balozi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvaku Manongi na huko Mjini North Carolina alipokewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani bibi Mwanaidi Sinare Maajar.
 
hiyo ziara ya kichama au kiserikali maana naye huyu toka afunge ndo,mbwebwe zimezidi,poleni sana CUF
 
Maalim seif sharrif yupo Hapa marekani kwa Ziara sasa ni wiki na amekutana na viongozi mbalimbali pamoja na Watu tofauti, ajenda kuu alokuja nayo ni ya ( ZANZIBAR HURU)
 
zanziba huru ni ndito ya mchana,yeye mwenyewe amekubali kuolewa bila mahali na magamba.sasa ameenda kuwadai wamarekani au??
dah,nimemsikia mbunge huko kenya anadai kibaki ni legevu.

kati ya dhaifu na legevu bora nin???
 
Aache ndoto za Mchana. Zanzibar huru itoke wapi mbele ya makucha ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano? Si walikubali wenyewe kuuza Identity yao kwa Woga wa Karume, sasa wanatupigia kelele za nini?
 
Kajua cuf ishakufa ivo Ana chake 2015 si angeenda bakwata au kwa kadhikudai talaka marekani ndio kadhi? Atajuta kuilewa kauza utu kanunua utumwa
 
Maalim seif sharrif yupo Hapa marekani kwa Ziara sasa ni wiki na amekutana na viongozi mbalimbali pamoja na Watu tofauti, ajenda kuu alokuja nayo ni ya ( ZANZIBAR HURU)

Marekani haiwezi kusikiliza WAPENDA FUJO WANAOHAMASISHA UDINI KAMA NGUZO YAO YA UHURU;

WANALINGANISHA UAMSHO NA HAKI NA USAWA WAO? Wanaongelea kuwa SENSA Sio haki hata kwa WAZANZIBARI; kila

kitu cha MAENDELEO Sio Haki; Unadhani WAAMERIKA watamsikiliza? SIDHANI... KAMA ATAPELEKA SIASA ZAKE KALI?

LABDA AMEZIACHA MLANGONI MWA NDEGE... SIO DUNIA YOTE AMBAYO INAKUMBATIA UBABE WA

WAISLAMU WENYE SIASA KALI...
 
Maalim seif sharrif yupo Hapa marekani kwa Ziara sasa ni wiki na amekutana na viongozi mbalimbali pamoja na Watu tofauti, ajenda kuu alokuja nayo ni ya ( ZANZIBAR HURU)

Halafu Marekani ikiwapa uhuru wakajiunge na Irani? Amekosea pa kwenda kudai.
 
Hakuna kitu kama hicho. Maalim Seif anajua fika kiini cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama ni kweli ana mawazo hayo; anajifanya hamnazo na ni dalili wazi kabisa kuwa chama chake kimejizika chenyewe baada ya kukubali kuolewa na CCM. Sasa anaota ndoto za kuwapo kwa Zanzibar huru, ili afanyanyeje? Hapo utapinga madai kwamba ajenda ya uamsho ilikuwa ni ya wakubwa katika Zanzibar?
 
Kabla ya kukubali Zanzibar Huru, napenda kijua kwa undani yaliyokubaliwa ndani ya muafaka? Nini kilichoshindikana kuunganisha CUF na CCM kama vile ASP na TANU kwa Tanzania as whole na sio kama walivyoigawa Tanganyina na Zanzibar?
 
maalim-564x272.jpg

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na mabalozi wa nchi mbali mbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Marekani na kubadilishana mawazo juu ya masuala tofauti yakiwemo ya kiuchumi, afya na teknolojia ya habari.

Katika mazungumzo yake na balozi wa Malaysia nchini Marekani bwana Othman Hashim, Maalim Seif amesema Zanzibar inaweza kushirikiana na Malaysia katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu ya juu, biashara, uwekezaji na kilimo.

Maeneo mengine ambayo Zanzibar na Malaysia zinaweza kushirikiana ni teknolojia ya habari, benki za kiislamu na utalii.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao pia wamekubaliana juu ya suala la kufuatilia mazungumzo hayo ambapo Zanzibar itatuma maofisa wake nchini Malaysia, ili kuona namna ya kukuza mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.

Kabla ya kukutana na mabalozi hao, Makamu wa Kwanza wa Rais alipata fursa ya kushiriki kwenye mikutano na makongamano mbali mbali juu ya mambo ya siasa na mahusiano ya kimataifa yaliyoandaliwa na taasisi ya National Democratic Institute mjini North Carolina, Marekani.

Makamu wa Kwanza wa Rais pia amefanya mazungumzo na mkuu wa taasisi inayojishughulisha na utoaji wa misaada ya vifaa vya hospitali katika nchi mbali mbali duniani Bwana Abdul Makembe Kimario.

Katika mazungumzo yao viongozi hao walijadiliana juu ya uwezekano wa Zanzibar kuweza kufaidika na misaada hiyo ya vifaa vikiwemo vitanda vya kulazia wagonjwa, vitanda maalum vya kufanyia upasuaji na mashine za uchunguzi wa maradhi mbali mbali katika hospitali zake za Wilaya na hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa misaada ya vifaa vya hospitali kwa zaidi ya nchi 124 duniani zikiwemo China, India na Israel.

Maalim Seif pamoja na viongozi na mabalozi wa nchi mbali mbali pia walihudhuria katika kongamano maalum, ambapo walishuhudia viongozi wa vyama vya

Republican na Democratic vya nchini Marekani wakihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 6 mwaka huu nchini humo, ambapo chama cha Demcratic kinawakilishwa na Rais wa sasa wa Marekani Rais Barack Obama na chama cha Republican kinawakilishwa na Bwana Mitt Romney.

Makamu wa Kwanza wa Rais aliwasili nchini Marekani tarehe 02 mwezi huu kwa ziara ya kikazi. Katika uwanja wa ndege wa New York alipokelewa na Balozi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvaku Manongi na huko Mjini North Carolina alipokewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani bibi Mwanaidi Sinare Maajar. ZIARA YA MAALIM SEIF MAREKANI INAENDELEA | Mzalendo.net
 
Back
Top Bottom