Maajabu ya Manispaa ya Arusha yanayotakiwa kuigwa na mikoa mingine

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,907
Yafuatayo ni maajabu niliyoyaona manispaa ya Arusha yanayotakiwa kuigwa na manispaa zingine

1.Manispaa imepiga marufuku watu wa manispaa ya Arusha kunywa pombe mchana.Baa zinafunguliwa saa kumi.Ukienda mchana hakuna atakaye kupa pombe ,Kuna askari wanazunguka ukikutwa unakunywa pombe muda wa mchana faini yako mnywaji ni Elfu hamsini na mwenye baa faini yake ni shilingi laki tau kwa kila kichwa kitakachokutwa kimeshikilia chupa ya pombe.Hivyo hupati pombe Arusha baa yoyote mchana.

Ukienda ukiwauliza wahudumu wanakwambia Magufuli kaagiza kuwa ole wako ukutwe unakunywa pombe saa za kazi utamkoma

2.Mji wa Arusha ni msafi mno nimeshangaa nimepita maeneo mengi au walisafisha kwa sababu ya ziara ya Magufuli sijui lakini mji msafi sio mchezo

Kingine kilichoniacha hoi ambacho hakitakiwi kuigwa na mikoa mingine ni kuwa Idadi ya BAA manispaa ya Arusha ni kubwa kuliko idadi ya maduka ya dawa za binadamu.Ni shida kupata duka la dawa lakini baa ni hapo na hapo tu.
 
Ilikuwa mwanzoni mwa utawala wa Mh Magufuli ndio watu waliogopa kunywa pombe. Zunguka majira ya kuanzia saa sita utakuta walevi kwa kwenda mbele kwenye sehemu zinazouza chakula
 
Kama hakuna idadi kubwa ya maduka ya dawa, ni kiashiria kuwa biashara hiyo hailipi, wananchi wanasiha njema. Tofauti na ule mkoa wa wala viwavi jeshi!
 
Kuna jambo zuri ambalo umesahau kuliorodhesha linalowahusu wakazi wa Arusha mjini, nalo ni KUIKATAA CCM a.k.a Chama Cha Machafuko. Yaani ukifika Arusha pale stendi ya mabasi utakuta waendesha bodaboda kibao wakiwa na magwanda ya Chadema. Ukipita kwenye mitaa iliyo mingi ya Arusha kama Mianzini, Ngarenaro, Sombetini, Mbauda, Sakina, Ngara mtoni na hata Njiro kule kwa wenye nazo ni kawaida sana kukuta vijana na wazee wakiwa kwenye magwanda ya Chadema. Kuvaa shati/fulana yenye nembo ya CCM ukiwa A-city ni sawa na kuwatukana wakazi wake.
 
Back
Top Bottom