robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Waziri Mkuu Majaliwa, Asante kwa kufika mjini Bukoba haraka baada ya ajali ya ndege. Hata hivyo kuna ajali nyingi zilizopoteza maisha ya wengi kuliko hata hii ya Precision, lakini hazikupata nafasi ya kiserikali kama hii. Hazikupewa hadhi ya maafa ya kitaifa kwa uharaka. na hasa kutembelewa na kiongozi wa kitaifa kwa umuhimu siku hiyo hiyo na kuahirisha shughuli zingine. Je, hadhi ya marehemu inatokana na aina ya usafiri:

1. Mama wa ajali zote nchini ni May 1996, MV Bukoba ilizama na kupoteza idadi isiyojulikana (zaidi ya 800) ya abiria.
-Hii Waziri mkuu Sumaye aliendelea na safari yake kama kawaida bila hisia.

2. April 2007 Abiria 22 walifariki kwa ajali ya basi la Buffalo likielekea Arusha.
-Hakuna kiongozi wa kitaifa aliyefika eneo la tukio

3. May 2017 wanafunzi 32, dereva 1 na waalimu 2 (jumla 35) wa Lucky Vincent Arusha walifariki kwa ajali
-Hakuna kiongozi wa kitaifa aliyefika eneo la tukio

4. Miezi mitatu iliyopita basi la shule limeua watu 13 mikindani mtwara.
-Hakuna kiongozi wa kitaifa aliyefika eneo la tukio


Ni kweli kwamba thamani ya marehemu ni aina ya usafiri? Kizuri ni kwamba Abiria wa Ndege wameokolewa na mitumbwi ya kasia. Na wasio na ajira za serikali au shirika. Asanteni kwa mawazo yenu.
 
Sasa huoni huo usafiri na wenyewe unawahusu!!

Hao ndiyo viongozi tulio nao. Wamejawa na unafiki na double standard.
 
Binafsi natafakari ni kwa nini nchi nzima inazizima. Ni kwa sababu ni ndege? ni kwa sababu ya watu 22? ni kwa sababu ni Precision? au ..........
Nionavyo sababu ni ndege. Nchi hii hupoteza idadi kubwa tu ya watu ktk vyombo vya usafiri. Kwa nini hatijawahi kuona idadi kubwa ya viongozi wakisimama majukwaani? Sasa limegeuka kuwa ni jambo la kitaifa kuliko makubwa zaidi ya hili yaliyowahi kutokea.
 
Mimi nafikiri labda ni kwa sababu ajali ya ndege hutokea kwa nadra sana.
 
Back
Top Bottom