M4C yamchanganya akili Waziri na Mbunge Kassim Majaliwa Mnacho Jimboni Ruangwa

Wa poti Ukana Shilungo, ulijumushila?

Nami nimefuatilia nini kinaendelea huko KUSINI, mikoa iliyo nyumba kimaendeleo licha ya kuwa wazalishaji wazuri wa korosho, ufuta na sasa kubarikiwa na neema ya mafuta na gesi. Mfano mdogo tu, Barabara ya KIBITI-LINDI imeanza kuzungumzwa tangu Awamu ya kwanza hadi leo, imekuja miradi mipya kibao maeneo mengine ya Tanzania na kumalizika utekelezaji wake lakini barabara hii hadi leo ni maneno tu. Kilometa 60 zinachua zaidi ya miaka mitatu, wakati maeneo mengi ya barabara yalijengwa chini ya kiwango na hivyo kutakiwa yarudiwe upya.

Hivyo M4C kwa mikoa hii, imekwenda kupandiza chachu kwa wananchi wa mikoa hii kujua kuwa kubaki na chama tawala haitawasaidia kamwe kuondoka katika lindi la umasikini na kukosekana kwa maendeleo. Mikoa hii imekuwa imebahatika kupata viongozi waliopewa nyazifa muhimu serikali na bado hawakuweza kuwa chachu ya maendeleo kwa mikoa husika, zaidi ni wao kuhamia Dar na kurudi mikoani kipindi cha ziara za viongozi au kuja kuomba kura.

Sasa M4C pamoja na kufanya mikutani hii kwa nguvu ya kipekee, pia inasimika viongozi kuanzia Kata hadi wilaya (Uongozi wa Muda) pale ambapo hakukuwa na uongozi ili kuweka na hatimaye kuendeleza uhai wa Chama. Viongozi katika Msafara wamekuwa wakitumia muda mrefu baada ya mikutano ya majukwaani kukutana na viongozi na kuwapatia miongozo ya kuimarisha Chama na maelekezo muhimu kwa mustakabali wa Chama. Kimsingi viongozi katika Msafara wanapata muda mchache sana wa kumpumzika na hiyo yote ni kuonyesha dhamira yao ya nini kimewapeleka KUSINI.

M4C kwa mikoa ya KUSINI, si tu ni mtaji kwa CHADEMA bali imesaidia sana kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa tayari kwa mabadiliko na kuonga mkono juhudi za mabadiliko, wanaelezwa waziwazi nini hasara za kukumbatia Chama kilichowasahau kwa muda wote huo wa uongozi wake. Mikoa hii iliyokuwa sehemu muhimu ya makambi ya wapigania ukombozi barani Africa (kusini mwa Afrika) imekosa hata marafiki toka katika nchi hizo ambazo zilileta wapigaji wake katika mafunzo.

Naambiwa leo wapo Ruangwa na Kesho watakuwa Nachingwea Mjini, natumani kamanda Chitanda ataweza kuwahamasisha vyema ndugu zetu wa maeneo hayo ili wajitokeze kwa wingi katika mikutano hiyo na kuwa sehemu ya M4C.

Naomba kuchangia.

Ilulu, chini ya mlima NAMBAMBO
 
ccm mwaka huu ni kilio kila sehemu wasikilizeni hata leo Jangwani watakuwa wanalia lia tu kabla ya kuja na mimkakati ya ahadi walizotoa wamezifikisha wapi nawanazimalizaje kwa miaka miwli na nusu iyobaki
 
ni kweli ndugu Buto ukombozi umefika,ni sisi watu wa kusini tumekuwa tukikumbatia hili joka linaloitwa ccm.
Nimefurahishwa sana ndugu Ukana Shilungo mana wameifanya kusini ndio ngome yao na wametuona wajinga ila kwa sasa wakati wa kuikumbatia NyinyiM umekwisha. VIVAA KUSINI
 
Back
Top Bottom