M23 waua Meja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - UN Yalaani!

Kuna jamaa mmoja wa m23 aliandika kwenye mitandao kuwa, wanajeshi wa JWTZ wamekufa wengi tu, alipotoa hiyo taarifa, hawa UN walikuwa bado hawajaeleza kama kuna mwanajeshi yeyote amekufa...

Haya maswala yananitia shaka sana. Sidhani kama kuna swala la muhimu sana linalotupelekea tukapigane vita huko zaidi ya kimbele-mbele tu kinachotupeleka huko....

Umefika wakati kila mtu abebe msalaba wake na sio kutwishana misalaba isiyokuwa na mbele wala nyuma. Mimi naamini, kwa tabia ya viongozi wetu ya kuficha-ficha mambo, unaweza kuta JWTZ wengi tu wanauliwa huko lakini watu wapo kimya tu...

Hakuna sababu ya JWTZ kupigana hiyo vita, na wasifikili kwamba hayo ni mazoezi tu... Hiyo ni Gorilla war....
nahisi ni kweli, juzi nilikuwa na mtu mmoja alitoka rwanda, inasemekana wanajeshi wengi wtz wamekufa hoko congo,ila ipo under carpet. na hawapo chini ya UN walipelekwa kinyemela kusaidia jeshi la congo. ndo hilo hasa limerecandle misiunderstanding kati ya Kagame na mh. km kuna mwny info km hzo plz!
 
Ni wakati muafaka sasa wa Rais wetu kuwapeleka wale wataalam wa pale Sangasanga japo watano (5) tu ... what is M23 bana...??? unless otherwise wanajeshi wetu wanauawa na UN peacekeeng force kujustfy uwepoji wao!!!
 
Amani haiji ila kwa ncha ya upanga, aluta continua. Kwenye vita yoyote lazima mambo kama hayo hutokea kwenye battlefied. Hatutakaa kwa amani kama jirani wanapigana wao kwa wao. RIP SOULDIER.
I concur, Hatuwezi kuanza kulalama na kukata tamaa kama kwamba hatukujua kuwa vijana wetu tuliwapeleka kule wakalinde amani; na ya kuwa ikiwapasa kuwa mstari wa mbele lolote, vikiwemo vifo, laweza kutokea. He/she has done her part on earth! RIP Soldier
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Tukubaliane Tanzania ilipeleka wanajeshi wake DRC chini ya mwavuli wa UN kulinda amani huko.Ni wazi kabisa unapoingia vitani suala la kufa au kujeruhiwa haliepukiki.Inashangaza wapo baadhi ya waTanzania wanaposikia habari za wanajeshi wetu kufa wanaanza kulalama utadhani waliambiwa wanajeshi wetu wanakinga dhidi ya risasi na mabomu.

Tuwape moyo wanajeshi wetu tusiwape nafasi maadui kwa kudandia propaganda dhaifu.Tujiulize wanajeshi wa merekani wangapi wamekufa Iraq au Afghanistan ?.Niko nyuma ya JWTZ, Niko nyuma ya uamuzi wa serekali wa kupeleka wanajeshi wetu DRC,tumechoka kulea wakimbizi njia sahihi ya kumaliza tatizo la wakimbizi Tanzania ni kushiriki kuitafuta na kuilinda amani ya DRC.

BIG UP SANA.

Hapo ndipo uone kuwa neno UZALENDO ni la mdomoni kwa watu wengi si kwa vitendo. Inawezekana hata baadhi ya viongozi wetu neno hili ni mdomoni tu. Vita ikirindima wanatimka mbio kurudi nyuma. Sisi tulipiga risasi wengi wa waoga hawa kwenye vita vya Kagera.
 
ndo mambo ya vita hayo,kuua au kuuliwa.mlidhan vita ni sherehe??? RIP Homie.no treat no surrender had kieleweke.may The Almighty God who is full of mercy and grace be with you and protect you all the time homies.much respect
 
hii ni vita mkuu ukiwa vitani kufa na kuuwana ni kawaida kwenye vita sio sehemu ya kuuza nyanya wala kuchekeana wacha wanajeshi wafanye kazi yao ya kuondoa kenge hawa ili DRC iwe huru kama ilivyu nchi nyingine
 
Una uhakika kwamba kina Kagame ndio wanawapatia silaha hayo M23? Tatizo la sisi waTz ni wepesi sana wa kusahau. Je, unakumbuka ishu ya "Mapanki ya Darwin". je, unakumbuka vizuri kuwa kuna ndege za kijeshi zilizokuwa zimebeba Silaha, zilizokuwa zinatua kule mwanza-Tz, unakumbuka? je, umeshawai kujiuliza zile silaha zilikuwa zikiishia/kwenda wapi?

So jamaa wameziweka mpaka leo wanazo?
 
Warudi tu nyumbani,idadi usikute ni kubwa sana ila tunafichwa tuh,

Wazungu kwao kuko salama kabisa,wala hatuskii vita vya wao kwa wao kwa sasa,

Kila siku wanachochea tuh Afrika na Middle east,kama ni kuwasaidia waafrika wenzetu inageuka kuwa laana na maafa kwetu ina haja gani?

Kufa wafe wengine,faida wapate wengine,?

Machungu makubwa huenda kwa familia za hao wafiwa,ina huzunisha sana haya mambo,ifahamike na ielezwe kama tunapigana vita na kagame basi iwekwe wazi,iwekwe wazi tuingie nae vita rasmi,sio kusema kwamba tunaenda kulinda aman na kunyang'nya silaha huku tukizid kuangamiza wenzetu kila siku,maisha ni haya haya
 
BIG UP SANA.

Hapo ndipo uone kuwa neno UZALENDO ni la mdomoni kwa watu wengi si kwa vitendo. Inawezekana hata baadhi ya viongozi wetu neno hili ni mdomoni tu. Vita ikirindima wanatimka mbio kurudi nyuma. Sisi tulipiga risasi wengi wa waoga hawa kwenye vita vya Kagera.

Uzuri wa Vita ya Kagera ni kuwa hata Wa Ganda walikuwa Nyuma yetu.
Hii ni technique ya Kumpiga adui kwa kutumia watu wake wenye kujua Mahali alipo na Kumfichua.
War is all about timing.
Hii Congo ipo???
PS.
Naona unatumia nguvu nyingin kuji advertise kuwa ulikuwa Frontline during Kagera War.
Huu ni zaid ya Ushamba kama sio Ulimbukeni ama Uzumbukuku
 
MD25 Tukiweza kuistabilize Congo tutafaidika na mengi sana.Congo ni moja ya nchi kubwa kabisa Afrika na kwa rasilimali na population ni mtaji tosha kwetu. Population na rasilimali za Congo ni zaidi ya nchi zote za EAC ukiziunganisha ukitoa Tanzania.

Najua inawezekana kupeleka jeshi Congo hatuna malengo ya uchumi zaidi ya kutumika na mataifa makubwa (kwa mazingira ya viongozi wetu wa sasa) lakini vyovyote vile amani yao inafaida kwetu kiuchumi.


Mkuu hapo kwenye RED... Mkuu nakushangaa sana na sijui haya mawazo unayatoa wapi. Wewe unazungumzia rasilimali za Congo ziinufaishe TZ? Hivi ni kitu gani hawa Congo ambacho wanacho sisi hatu? Ni madini gani yapo kule ambayo Tz hayapo? Tena sisi hadi tuna mafuta. Na kwa upumbavuu wetu sisi waTz, tumewasusia waChina huo mradi wa gasi. Wachina walivyokuwa na busara hadi Casual Labours, wamewatoa China. Je, vijana wetu waende wakafanye kazi wapi sasa?

Mkuu usiongee kabisa kuhusu rasilimali, Je, hizi za kwetu zimetusaidia nini hadi leo hii uone kuwa rasilimali za Congo zitatutoa kimaendeleo?

 
hii habari JWTZ kama tumeamua kwenda vitani kongo lazima wawe responsible kukanusha au kukubali mara moja propaganda kama hizi
 
Hivi mlivyokuwa mkiunga mkono askari kwenda kule mlidhani wanakwenda Picnic?
Acheni kuwa na mioyo ya sabani kutepeta ndani ya maji na hivyo kulitisha jiwe eti lisiguse maji, unapojiunga na jeshi unakuwa ume sign kifo.
Kikubwa askari wetu wawe katika nidhamu halisi ya kivita, hiyo ni vita rasmi, msitarajie vinginevyo. Ila msisahau kufanya Documentaion ya kile mnachopigania ili mje kutuonyesha vita na ushindi huo una impacts zipi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi, kama ni just an opportunity ya majeshi yetu ku practice mafunzo bila ya nchi kuingia ghalama, pia tujuzwe hilo.
 
Mods hivi hakuna njia ya kuwapa ban hawa manyang'au M23 wa Rwanda wanaoamua kuanzisha psychological war hapa JF?

Naamini vita hivi ni vyetu wote na JF tunaweza kupigana kwa kutoa ban mara moja kwa maadui walioingia hapa.

Wale washindi wa matusi kwenye topic za CCM vs CDM hapa nadhani tunawahitaji sana, hawa wanyarwanda wa m23 wanahitaji huduma za washindi wa matusi JF. They need it now!
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Tukubaliane Tanzania ilipeleka wanajeshi wake DRC chini ya mwavuli wa UN kulinda amani huko.Ni wazi kabisa unapoingia vitani suala la kufa au kujeruhiwa haliepukiki.Inashangaza wapo baadhi ya waTanzania wanaposikia habari za wanajeshi wetu kufa wanaanza kulalama utadhani waliambiwa wanajeshi wetu wanakinga dhidi ya risasi na mabomu.

Tuwape moyo wanajeshi wetu tusiwape nafasi maadui kwa kudandia propaganda dhaifu.Tujiulize wanajeshi wa merekani wangapi wamekufa Iraq au Afghanistan ?.Niko nyuma ya JWTZ, Niko nyuma ya uamuzi wa serekali wa kupeleka wanajeshi wetu DRC,tumechoka kulea wakimbizi njia sahihi ya kumaliza tatizo la wakimbizi Tanzania ni kushiriki kuitafuta na kuilinda amani ya DRC.


Mkuu,
Ni kweli kwamba kwenye vita kuna kufa au kupona,ama kujeruhiwa na kupata ulemavu,

Hata hao wamarekani hivyo vita vya iraki hadi hivi sasa wanavilaani kwa maafa yaliwawapata ndugu zao,

Hakuna kile Bush na Adminstration yake walichosema kuwa ni Weapons of Mass Destruction wala Direct connection between Saddam's Adminstration with Alqaeda Extrmists,damu zimemwagika bure tuh kwa interests za mafuta ambayo kwa kias kikubwa wamefanikiwa,

Na huko Afghanstan umeona kwa sasa wanaona wakae wayamalize kuepusha mauaji zaid,

Hii vita inayoua jamaa zetu huku sisi inatupa manufaa gani??na ielezwe wazi tumeenda vitani au kulinda amani??

Kama vitani tuelezwe tunapigana na nani na kwa faida gani,haya ni majesh yetu na wanaokufa huko ni ndug zetu.,au wewe huna ndugu huko??sisi tunao wengi wamepelekwa huko,tunaskia uchungu kweli kweli,

Hatuwez kupoteza uhai wetu kwa maslahi yasiyo ya taifa na sababu zisizowekwa wazi,tunalinda aman au tumeingia vitani??

Hayo ni matatizo yao,sisi tunayo yetu mengi tuh,let them handle their problems,ama la tusifichane fichane ukweli juu ya hili,ni vita au ni peacekeeping & disarmament??
 
Elimu kuhusu jambo lolote ni muhimu sana kabla hujaanza kulijadili.

Soma haya maelezo kwa umakini, utulivu na utapata mtazamo mpya kuhusu suala la DRC...

Bodi
Nimesema mara Nyingi sana. Tanzania au Afrika mashariki zinapigana vita isiyowahusu. Hizi vita zote au nyingi za afrika zinaendeshwa na mataifa makuu ambayo yanajichukulia raslimali za Congo bure kwa miaka nenda rudi. Madini yapatikanayo Congo ndiyo yanayotumika kutengenezea simu zote za Mkono duniani, na Mabomu makubwa ya kivita duniani. Bomu la Hiroshima, lilitengenezwa na mali gafi toka Congo.liliwaua WaJapani wengi mno.

Utengano wa Nchi zote za Kiafrika zinasababishwa na umilikaji wa haya mali gafi ya Africa. pamoja na madini yote makuu kama dhahabu, Almasi, uranium,Platinum you name it. Kutokana na udhaifu wa Maraisi wetu wasioona mbele na kufuatilia historia ya Ubepari, ukoloni, na uhujumu wa Africa, bado wananunuliwa kwa vijisenti na hao hao watu, na kinyima Africa maendeleo. maraisi wengi wapo raddhi kutoa utajiri wetu mkuu kwa hawa mabepari na kumlimbikiza Mwafrika aliyesoma na kuyaona haya matatizo kinaganaga. Maraisi wetu watatumiwa na hawa vibaraka kuwaua Waafrika wanaopinga uhujumu huo, Kuwanyanyasa, kuwanyima vyeo,na hata kuwabambikiza kesi zisizo na maana na kuwafyatulia risasi hadharani kinyama kwa sababu wanalindwa na hao hao mabeberu na mabepari. Hao Wafaransa mnaowataja ndi walioleta dhana za kivita kuwaua wanyarwanda wakisaidiana na maofisa na maraisi wa Congo wenyewe, wakipigania umiliki wa madini Congo kati yao na Wamarekani.


Congo si maskini. maraisi wote isipokuwa Patrice Lumumba alitetea haki ya Wakongo. Lakini aliuawa na mataifa haya makubwa kwa kutetea madini na utajiri wa Congo. Hakuna raisi mwingine yeyote wa Congo aliyewatetea Wacongo, Wote ni vibaraka watupu. Congo inautajiri wa madini makuu yenye thamani kubwa kuliko nchi yeyote duniani. Vibaraka wanakwenda ubia na mabeberu kuiweka Congo kwenye umaskini kama kuku.


Sasa Tanzania na Malawi na Africa ya Kusini mnatumika kupigana vita msiyoijua. Kwa nini tupoteze Askari wetu kwa maslahi ya Wazungu. Kagame anajua hiyo pia.Tuwatafute maraisi wenye kisomo cha hali ya juu, wenye kujua historia safi ya ugawanyaji wa Afrika kwa manufaa ya mataifa makubwa. Utajiri wa mataifa makubwa mengi unategemea maligafi ya Africa, na wanafanya kila kitu kuibomoa afrika Wakijua wengi wetu ni mambumbumbu hatusomi na kuyafuatilia masuala haya. amkeni Waafrika wenzangu. amkeni Watanzania wenzangu. Tunarudishwa nyuma kimaendleo kwa kutokujielimisha wenyewe , kwa uchu wa pesa, ujinga wa fikra, woga wa kujitetea wenyewe, kama tunavyoona Mawaziri wetu na Maraisi wetu kutokuwataja wauza unga huku wanawajua wote wahusika.


Ukimya, woga, kukosa Ushujaa, majivuno kama binadamu kamili,Kutokujiamini na uduni wa Kielimu na uvivu wa kufikiri, ni Sumu kwa waafica wote na inazidi kutuzorotesha, kutugawa,kutuua, kutuibia, kutufanya tuwe chini ya Wazungu, na kutufanya bado tuwategemee wazungu kwa kila kitu.
 
Wakati mwanajeshi wetu akiuwawa huko Kongo kwa kulinda amani chini ya Mwamvuli wa UN, Rwanda imelizuia baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa kulaani mauaji hayo na kuwawekea vikwazo wahusika.

Rwanda blocked a joint U.S.-French proposal to impose U.N. sanctions on two senior commanders in the M23 rebel group in easternCongo, arguing that the evidence against the men was weak, Rwandan and other U.N. envoys said on Wednesday.

The latest diplomatic wrangling in New York came as U.N. helicopters and artillery attacked M23 rebel positions near the city of Goma in eastern Democratic Republic of Congo on Wednesday in support of an offensive by the Congolese armed forces. One U.N. peacekeeper from Tanzania was killed and three other blue-helmeted troops were wounded.

The United States and France submitted documents to the U.N. Security Council's Congo sanctions committee last week explaining why M23's Colonel Vianney Kazarama, military spokesman for the rebel group, and Erick Mboneza, an M23 commander, should be hit with U.N. sanctions.

Among other things, those documents, seen by Reuters, cite a July Human Rights Watch report that accused Mboneza of ordering the summary execution of a 24-year-old man he said was a thief.
The documents also refer to a U.N. Group of Experts report that says Mboneza and an M23 Colonel Kaina, who is already subject to a U.N. travel ban and asset freeze for his activities in the rebel group, were seen meeting with Rwandan military officers between March and May 2013.

The Group of Experts has repeatedly accused Rwanda of supporting M23, an allegation Kigali vehemently rejects. The cross-border accusations underscore the M23 rebellion's roots in a complex web of local politics and regional conflicts over ethnicity, land and minerals.
Rwanda's deputy U.N. ambassador, Olivier Nduhungirehe, told Reuters that Kigali blocked the proposed blacklisting because it would have undermined regional efforts to bring peace to eastern Congo and Kampala talks between M23 and Congo's government.
He added that the evidence supporting the U.S.-French proposal was "very poor."
Diplomats said Rwanda, a temporary council member, was the only one of the 15 member nations that opposed the idea of blacklisting the two men.

The Security Council's sanctions committee works on the basis of consensus, which means Rwanda was able to singlehandedly block the proposed blacklisting.
In theory, council members could vote on the blacklistings in a Security Council resolution that Rwanda would be unable to block. It was not clear if the council was prepared to do that.

'DEEPLY REGRETTABLE'
Separately, Rwanda has repeatedly rejected council efforts to issue a public statement condemning M23 attacks on U.N. peacekeepers last week, U.N. diplomats said. Rwanda complained that the Western-drafted statement was unbalanced and unfairly targeted the M23 while ignoring attacks by the Congolese army.

Kigali initially criticized the statement for not mentioning shelling onto Rwandan territory last week, though later drafts, all seen by Reuters, did ask for the council condemn the firing into Rwanda.
A new draft of the statement was rejected by Rwanda on Wednesday. A Rwandan delegate said in an email to other Security Council members that it could not support some of the language in the latest draft text.

One council delegation responded to the Rwandan rejection by saying , "It would be the first time when attacks on U.N. peacekeepers are not condemned by the Security Council. This situation is deeply regrettable," according to a copy of the email, seen by Reuters.
But Nduhungirehe said negotiations on a statement were continuing. "We are now close to an agreement," he said.
A 3,000-strong U.N. intervention brigade, with a tough new mandate to protect civilians and neutralize armed groups in the mineral-rich central African nation, sprang into action last week after it accused the M23 rebels of shelling Goma. The violence has been escalating there in recent days.

Rwanda blocks proposed U.N. sanctions for two Congo rebels | Reuters
 
Back
Top Bottom