M23 waua Meja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - UN Yalaani!

MKUU NA KUUNGA MKONO KWA HILO 100% Ni upumbavu kupeleka wanajeshi sehemu ambayo Kimsingi wanakuwa and tihgt control na hawawezi kujibu mashambulizi iwezekanavyo au strategic attacks huu ni upumbavu hamna namna nyingine tunavyo weza kuuita.

Kwa nini wasipewe amri ya kumshambuli moja kwamoja badala yake kuna kuwa na urasimu wa ovyoovyo mara waishiae hapa au pale ni narudia tena anayedhani kwamba Jeshi letu liko kule na ni Salama anajidanganya .Wote sisi ni wazalendo lakini hatuwezi kuchanganya uzalendo na uzandiki watu wameuwawa Sudan tumesikia Kulaani..kulaani..kulaani... ndo imetoka hivyo..sasa inatokea Kongo kama tumekwenda kupambana na M23 ilikuleta amani Kongo tupambane nao na tupewe unconditional mandate basi ! moja kwamoja ijulikane ...waache kurembaremba tatizo nivita vya kimaslahi zaidi...vinginmevyo vijana wetu warudi nyumbani...

Walikufa wakipigana Msumbiji....walikufa wakipigana Angola ...tulipambana kusaidia Zimbabwe,Uganda na Afrika ya Kusini hasara ya mali na uhai tuliyopata inatosha we have no more blood to be sheded


Agreed! Ni upumbavu UN kuingiza askari vitani wamefungwa mikono. Very stupid. Turuhusiwe kupigana. Kama Uganda na Kenya wataingia upande wa Rwanda waje na izuke tu vita ya SADC na EAC hapo.
 
Naona tatizo la wazi kabisa katika ushiriki wa JWTZ na majeshi ya South Africa. Kama UN wanataka kuwepo na amani DRC yapo mambo ambayo wangefanya maana wanajua kabisa ufadhili wa M23 unatoka wapi. Pili, JWTZ tunapeleka Jeshi kwa maslahi ya nani?! Kuna haja gani ya kupeleka Jeshi frontline wakati sheria za UN zinakubana kupambana na adui ambaye yeye anaweza kukushambulia bila vikwazo vyovyote.

Nchi za Ulaya na Marekani zina mipango ya ajabu sana, kama unakumbuka vita ya Angola, walipoamua hiyo vita iishe Savimbi alikufa kama kuku na vita ikaisha. M23 haina nguvu za kupambana na UN kinachofanyika ni kupoteza muda tu. Kuwa mwanajeshi haina maana kuwa uhai wako upo ili ufe tu hata pasipo sababu ya msingi. Wanajeshi wa JWTZ wanaapa kuilinda mipaka ya Tanzania na sio mipaka ya DRC.

Kama UN wanataka kuwamaliza M23 wangelisaidia jeshi la DRC na sio kuchukua askari nchi za nje.
 
RIP MAJ.MSHINDO, kuna watu nawashangaa sana humu, tangu mwanzo ilishasemwa mission ya congo ni tofauti na Darfur.na ndio maana hata majeneza special yalipakiwa kwenda goma.when you are in warzone, anything can happen at any time, kama hao waliorushiwa artillery wakiwa kwenye ngome..., cha maana ni kutowavunja vijana moyo..., rather support them 100%. mambo mengine mnayoandika hapa hao m23 wanayasoma na wakiona sisi wenyewe tunaanza kufarakana kwenye mitandao wanajua ni reflection ya general public, therefore wataendelea na guerrilla tactics kama hii walofanya.na trust me, hakuna tactic inayovunja morale ya wapiganaji kama guerilla tactic.adui anajificha then anatumia single opportunity kuwadhuru then anajificha tena, anaweza kufanya mashambulizi matatu tu kwa mwezi mzima lakini yakawa na devastating psychological affect kama tusipowapa moyo wapiganaji wetu.niwakumbushe wale wanaohoji kwanini tupo goma, usalama wa taifa letu goes beyond our borders....., jirani asiye salama eventually ni threat kwako.
 
Vita ndiyo vilivyo lazima kuwe na casualties. Pole nyingi sana kwa wafiwa. Rest in peace commander!!!

Casualtieas wakitetea nn GOMA na BUKAVU?Anakufa afisa wetu kwa shughuli isiyo tuhusu kabisa!

Vita halali tuliyowahi kupigana TZ ni vita vya Kagera tu;tuliwatuma vijana wetu waende kutetea mipaka yetu!Hata JWTZ wafe kombania nzima wakitetea mipaka yetu sitalia bali nitawapongeza!

Vita vya Congo havituhusu tunapoteza askari wetu bila sababu yyt ya maana!Inaniuma sana!
 
jipeni moyo askari wetu,Jehovah azidi kuwalinda na kupigana upande wenu

pamoja
 
tumeenda drc kulinda amani kwa sababu bunge letu lilikubaliana na mikataba ya umoja wa mataifa kulinda amani popote duniani..ndio maana hata liberia, sudan na lebanon tulipeleka majeshi....kama tunataka kujitoa tuanze na bunge letu kupitisha ovyo kila mikataba inayowekwa mezani bila kuuliza maslahi ya taifa..ndio maana nchi kama marekani ilikataa kutia saini mkataba wa umoja wa mataifa kulinda mazingira wa kyoto japan...think big broo.

Anyway..tupo vitani..the best way sio kugombana na kulaumiana..ni kupeana mbinu za kushinda vita na tuta-count losses after the victorious won wars....

Strategy no-1. Tukate supply ya silaha kwa m23..ambayo ni rwanda. Lets wage a war with rwanda na tumtoe pk then tuone hao m23 watakimbilia wapi kama sio kwa m7


strategy no-2. Kila vita ina-gharama zake kubwa tuu..ndio maana marekani huwa hapigani vita sehemu ambayo haiwezi kumlipa gharama za vile vita...hii vita inalipa na ukimtoa pk inakuwa rahisi kulipwa chetu na drc kupitia madini aliyokuwa anachukuwa kagame na m23 wake in exchange for peace tutakayoiweka huko goma..plus tunaikalia rwanda kupunguza tension kwa east africa for atleast 5 years mbaka nchi itapopata kiongozi wa kidemokrasia kama sisi na wenzetu kenya...in doing soo tunatuma sms kwa jirani uganda na m7 atafuta ndoto zake zinazokaribiana na zile za amini dada.

Guys am soooo sorry to tell the truth in a broad daylight.

Correct Again! Nimependa zaidi shaded areas. Lakini hili wazo lako linayo potential ya kuzusha vita kati ya EAC na SADC, ingawa sijaona economic value ya Kenya kupigana upande wa Rwanda. Vita vingi zinakuwa na uhusiano wa political-economy ya eneo kama ulivyobainisha correctly. Hata Uganda hawana economic benefits katika kuisaidia Rwanda kwenye vita ikiwa kubwa kihivi tunavyotaka iwe. Rwanda ni wapumbavu sana kudhamini hii vita. Nakubaliana nawe dawa tuhamishie hii vita Kigali waonje gharama ya kulinda raia ndani ya nchi yao, kujua DRC inavyosumbuka. The sooner the better!

UN wafungue kamba mikono wamewafunga askari wa JW na SADF, na wengine waliopo pale.
 
Isiwe vita ya kulinda amani, ila vita ya kushambulia kuwaondoa hao waasi wa M23.
 
RIP Kamanda......kile ninachokiona sasa ni vita ya M23 na jeshi la Tanzania,kama kweli Mr Kagame anawasaidia hao jamaa kwanini tusiamini kwamba amewaamuru sasa mashambulizi ayageuzie kwa wanajeshi wetu,hili suala la DRC nadhani linahitaji hekima na ulinzi wa Nchi zote za Africa katika ukanda huu,hili suala la Tanzania na South Africa pekee kupeleka wanajeshi linanitia shaka kuwa Watanzania tunajitengenezea maadui zaidi,kwanini Uganda na Kenya wao hawana wanajeshi huko?Ngoja tuendelee kuangalia huku tukiomba ndugu zetu warudi wakiwa salama.
 
Mkuu M23 ni matawi tuu.
Kuhangaika na M23 ni kupoteza wakati na Maisha ya watu.
Mzizi ni Kagame...hivi inachkua siku Ngapi kumshughulikia Kagame

kagame hawezi kushughulikiwa moja kwa moja. lazima m23 isababishe na kusafisha njia ya kummaliza kagame. Rais wa Burundi amesita kujiunga na akina kagame na uhuru kuitenga TZ. hakuenda Mombasa bali akaja mapumziko ya siku 3 Dar. ameondoka jana kurudi Burundi.
02.jpg
 
ninaamini wanajeshi walioko Sudan wapo kwa mwavuli wa UN kweli;


em jiulize mkuu, kama UN wasingekuwapo Congo, Kikwete asingepeleka wanajeshi?
Kama UN isingekuwepo halafu JK akapeleka wanajeshi kule,ingekuwa ni tofauti kubwa sana.Mataifa mengine pengine nayo yangejitokeza wazi kusapoti hao waasi.Hawawezi kufanya hivyo wazi wazi kwasababu ya mwavuli wa UN wanaoutumia wanajeshi wetu,wasouth,Malawi nk.


Tanzania ndo ingekuwa directly(or maybe through some kind of a coalition) kama tungepeleka majeshi bila UN kuwepo.

Kuna tofauti kubwa sana btn the current situation(s) ukilinganisha na nyakati zile tulipokuwa tukipeleka wanajeshi kwenye ukombozi wa mataifa mbali mbali ya Afika hususan kusini.
 
Huyu Kagame ni mtu jeuri sana na jeshi letu bila kwenda mapema kummaliza kulekule Kongo alikuwa na mpango wa kuja kuvamia huku.

Mi naamini Tz kuamua kwenda kule hawajakurupuka ila wanajua wanachokifanya isipokuwa sisi wanannchi wa kawaida ndio tusiojua undani na kimsingi hatupaswi kujua undan huo. Uamuzi wa serikali ni sahihi kabisa
 
Huyu Kagame ni mtu jeuri sana na jeshi letu bila kwenda mapema kummaliza kulekule Kongo alikuwa na mpango wa kuja kuvamia huku.

Mi naamini Tz kuamua kwenda kule hawajakurupuka ila wanajua wanachokifanya isipokuwa sisi wanannchi wa kawaida ndio tusiojua undani na kimsingi hatupaswi kujua undan huo. Uamuzi wa serikali ni sahihi kabisa

wewe naye! hao wanajeshi hawajui kitu wao ni kutii amri tu,tena hivi wameanza kugoma kwenda frontline kwa sababu ya vifo vingi vya ndigu zao,habari kama hizo hamzipati,hata wao hawajui wanapigania nini yani ni kikwete peke yake anaye jua.
 
Hivi lazima TZ ipeleke vikosi huko wanakopeleka?
Ni muhimu kufanya hivyo kwa sababu usipomuua nyoka anayemsumbua jirani yako,ipo siku atahamia kwako na kuleta usumbufu mkubwa!
Vifo vitani nia jambo la kawaida,cha msingi ni kufikia malengo na kupunguza idadi ya vifo!
 
Naona tatizo la wazi kabisa katika ushiriki wa JWTZ na majeshi ya South Africa. Kama UN wanataka kuwepo na amani DRC yapo mambo ambayo wangefanya maana wanajua kabisa ufadhili wa M23 unatoka wapi. Pili, JWTZ tunapeleka Jeshi kwa maslahi ya nani?! Kuna haja gani ya kupeleka Jeshi frontline wakati sheria za UN zinakubana kupambana na adui ambaye yeye anaweza kukushambulia bila vikwazo vyovyote.

.

Vitu vingine kabla hujandika fikiria au soma na wengine wansema nini na ujifunze.

jeshi hili ni tofauti na lile la sudan na leban na pia lilopo sasa lenye watu zaidi ya 10,000 ndani ya Congo lakini halina Meno.

Hili ni special kwa ajili ya kuwapokonya Silaha WAASI na kwa sasa waaasi walio kimbelembel ni M23 nadhani utakubaliana na hili.

sasa tulia usikilizie M23 wakinyolewa kwa kipigo cha Mbwa mwizi na ni kimya kimyaa!
 
Tatizo watu hampendi kuambiwa ukweli,hii vita haina maana yoyote kwa watanzania,wanakufa bure kwa sababu ya masilahi ya jk na zuma tu,tena sio huyo meja tu,kuna wengi sana wamekufa wanaficha,wamemtaja meja kwani ni mtu wa cheo kikubwa huwezi kuua meja wengine aliokua nao wakasalimika,yani makopolo na private niwengi wamekufa,halafu wewe unaleta vya uzalendo,mala unga sijui nini,ukweli mtaujua si muda murefu.
Mkuu Mkamantare mbona wanasema artillary shell iliwadondokea wakiwa nadhani wamelala/pumzika, tangu lini Makopolo na Maprivate wakalala sehemu moja na Ma Afisa wa jeshi?
 
Back
Top Bottom