M/kiti wa mtaa Upanga katugeuza wakaazi mtaji !!

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
Habari wadau,

Naomba nitoe dukuduku langu, kuna huyu mwenyekiti wa mtaa wa CCM kata ya Upanga Mashariki anaitwaa Rukiya A. Riyami toka aukwae uenyekiti 2011, anatukamua sana sisi wakaazi wa Upanga, kila mwezi anataka kila kaya ilipe alf 5 ya kupuliza dawa ya wadudu, anatuchangisha michango mingi, na juzi katuletea barua kuwa kapandisha ada ya sungusungu toka alfu 3 mpaka alfu 5,na mtu akichelewa kulipa anatutumia mgambo na vitisho vingi, sasa mimi najiuliza hivi miezi 2 tu kushika kiti hali ndio hii,miaka 5 itakuaje???

Naomba mamlaka husika zichukue hatua, maana huu ni ufisadi mkubwa kwa wananchi
 
Upanga ulinzi wa sungusungu wa nini,wakati kila mtu yupo ndani ya gati lake,kwanza haya mambo ya sungusungu bado yako hivi?,lakini ndio matunda ya kuchagua CCM hayo...!
 
Huyu mwenyekiti ni mpuuzi sana anakera na hao sungusungu alio waleta amewatoa tameke ni wezi vya kutosha.

Pale mzumbe wanawaliza wanafunzi vilivyo..

Utawasikia kila siku ndomboro ya solo eti wanakimbia mchakachaka huku wanacheck sehemu za kupora ucku.
 
ningekuwa mimi ningewalamba si chini ya elfu kumi kila wiki, kwa sababu wakazi wa upanga/jimbo la ilala lote mnajifanya kuipenda sana ccm
na pia mnaviona vyama vya upinzani ni vyama vya fujo.

mmepitwa na wakati mno, aendelee kuwala tu maana wajinga ndiyo waliwao
 
Halafu wewe unamatatizo, sio wote ni wale wahindi!
 
ningekuwa mimi ningewalamba si chini ya elfu kumi kila wiki, kwa sababu wakazi wa upanga/jimbo la ilala lote mnajifanya kuipenda sana ccm
na pia mnaviona vyama vya upinzani ni vyama vya fujo.

mmepitwa na wakati mno, aendelee kuwala tu maana wajinga ndiyo waliwao
Usifikiri wote tunaokaa upanga ni ccm, au wote ni wahindi.....usiropoke ovyo
 
Wanakupa risiti ukiwapa pesa? kama nini mimi sitoi na wafanye watakavyofanya. Siunalipa Kodi kwani kodi yako inatumika vipi? waulize kuwa Watanzania wanalipa kodi sasa inakuwaje tunachangishwa pesa? je hao wadudu bado hawajafanya? wasijue kuchangisha watu na ripoti pia wakuleteeni. Huu ndio Ufisadi, Hivi Tanzania michango ya kijinga itaisha lini?
 
Nadhani hawa vibaka wa mtaa wa olympio wanapeleka sadaka kwa mama liyami, maana wanavyopora hata mtaa huu haufai kupita ikishafika saa 12 jioni. Inashangaza sana. Au ndo njia ya CCM kuongeza kipato?.
 
Upanga ulinzi wa sungusungu wa nini,wakati kila mtu yupo ndani ya gati lake,kwanza haya mambo ya sungusungu bado yako hivi?,lakini ndio matunda ya kuchagua CCM hayo...!
Ulinzi wa sungusungu umeletwa kivingine wanauita ulinzi jamii shirikishi kila mtaa unaajiri vijana kama 20-30 bila kuwa na uchunguzi wowote na wakazi wanatakiwa kulipa elfu 3 kila kaya kuwalipa mishahara hawa 'vibaka' malalamiko ni mengi na wengine imethibitika wametoka jela karibuni ni taabu tupu,ukikataa unaletewa barua ya mtendaji halafu mahakama ya jiji.
 
huku kwetu kipunguni raha tu hamna cha sungu sungu wa mgambo jamii tukikamata kibaka si tutapiga kiberiti tu. Michango ya nn
 
madarakani ameingia dec 2009 kwa kumbukumbu zangu kwa kusema 2011 unamaanisha nini naomba ubadilishe usemi wako na isitoshe hausiani chochote na upuuliziaji wa dawa ya kuua wadudu. susungusungu kwa upanga ni muhimu sana kwani mitaani tulivamiwa na wezi stadi wa kutumia pikipiki na magari kupora wanafunzi laptop na mikoba ya kina mama, wezi hawa walikamatwa na sungunsungu na kupigwa sana na toka hapo upanga ikawa shwari.
kuhusu kupandishwa malipo ya sungusungu yamefuata taratibu zote za vikao kufikishwa hadi kwa wakazi hata hivyo sio wote tunaolipa sungusungu, wakakwani sungusungu wanalinda mitaani na sio ndani ya mageti ya nyumba za wakazi. nadhani wewe utakuwa si mkazi wa upanga hii.
Mwenyekiti huyu toka ameingia ameboresha vitu vingi kama usafi wa barabara zetu zinasimamiwa na yeye mwenyewe na zinapendeza. MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI. Wakaz wa upanga hatutaki majungu na kabla ya kuandika kitu nakuomba fanya uchunguzi wa kina kwanza na kumbuka CCM ndio imetuweka kwenye amani
 
Back
Top Bottom