Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

kanda2

JF-Expert Member
Apr 22, 2007
1,318
72
Aliyewahi kuwa mbunge wa Bukoba mjini kwa tiketi ya CUF na naibu katibu mkuu, bwana Lwekatare inasekana yuko kwenye hatua za mwisho kujiunga na CHADEMA.

Hali hiyo imekuja baada ya mkutano mkuu wa CUF uliofanyika mwishoni wa Februari kuchagua viongozi mbali mbali na baada ya hapo kuna nafasi za kuteuliwa, bwana Lwekatare alikosa nafasi yake ya naibu katibu mkuu.

Lwekatare amekosa uvumilivu wa mzee Kawawa wa kupanda na kushuka kimadaraka?
 
Aliyewahi kuwa mbunge wa bukoba mjini kwa tiketi ya cufna naibu katibu mkuu, bwana lwekatare inasekana yuko kwenye hatua za mwisho kujiunga na chadema.

Hali hiyo imekuja baada ya mkutano mkuu wa cuf uliofanyika mwishoni wa february kuchagua viongozi mbali mbali na baada ya hapo kuna nafasi za kuteuliwa, bwana lwekatare alikosa nafasi yake ya naibu katibu mkuu.

Lwekatare amekosa uvumilivu wa mzee kawawa wa kupanda na kushuka kimadaraka?

NI tetesi briking nyuzi au unauliza? source????
 
Hii move si nzuri kwa Bwana Lwakatare kwasababu kujitoa kwake CUF na kujiunga na CHADEMA itakuwa ni kutafuta cheo na si kutetea maslahi ya wananchi.Kwanini Lwakatare ajitoe CUF baada ya kuenguliwa katika safu za uongozi wa juu.
CUF ni chama chenye nguvu zaidi Zanzibar kuliko huku bara,maamuzi mengi makubwa yanafanywa na viongozi wajuu kutoka Zanzibar pengine Lwakatare kaonekana hana manufaa tena kwa chama.
 
Aliyewahi kuwa mbunge wa bukoba mjini kwa tiketi ya cufna naibu katibu mkuu, bwana lwekatare inasekana yuko kwenye hatua za mwisho kujiunga na chadema.

Hali hiyo imekuja baada ya mkutano mkuu wa cuf uliofanyika mwishoni wa february kuchagua viongozi mbali mbali na baada ya hapo kuna nafasi za kuteuliwa, bwana lwekatare alikosa nafasi yake ya naibu katibu mkuu.

Lwekatare amekosa uvumilivu wa mzee kawawa wa kupanda na kushuka kimadaraka?

Mhh hii kweli au nyepesi nyepesi za mitaani? Kama jamaa anataka kweli kutoka atakuwa kachemsha ilitakiwa hiki kitu akifanye mapema otherwise ataonekana kituko kuwa alikuwa after madaraka. Inabidi afikilie mara mbili.
 
Lwakatare atanufaika zaidi kwa Chadema kutokana na kuyumba kwa CUF,akijiunga Chadema ni pigo kwa CUF ambayo haina mbunge Bara.
 
i support the move for the benefit of himself. Mana mwelekeo wa kafu/CUF siuelewi, hata sasa wananchi tunashindwa kuelewa mwelekeo wao
 
Kama ni kweli...kwani ni lazima uwe na cheo kwenye chama cha siasa kucontribute for transformation????!Hainiingii akilini!!
 
Ukisoma vizuri alama za nyakati, CUF imepoteza mvuto wa kitaifa na kimkoa. Mgombea mtarajiwa yeyote mwenye kupiga hesabu vizuri hata kama anao mtaji wa wapiga kura, kugombea kupitia CHADEMA ndiyo turufu yenye uwezekano mkubwa wa kushinda ubunge.
 
Tatizo mnashindwa kuielewa CUF ,CUF demukrasia ipo na jambo zuri kuwa hawapapatikii viongozi ,wala hakuna anaebembelezwa ,wanakuja wanaondoka ,ila Chama wanakiacha pale pale ,hebu jiulizeni wangapi wamebwaga manyanga na bado CUF inapeta ,haijatetereka wanachokidai CUF ni uchaguzi wa haki hakuna jingine ,wanachokidai CUF ni Katiba Mpya ,wanachokidai CUF ni Tume mpya ya Uchaguzi ,wanachokidai CUF ni mahakama Huru ,wanachokidai CUF ni viongozi kutokuwepo juu ya sheria.

Hili linapatikana katika Katiba mpya ,sasa tukubalini kuwa CUF iendelee na viongozi wenye busara ila siku ikipata kiongozi mvuta bangi basi mjue amani itatoweka nchi hii na kuwa kumbukumbu na wafuasi wa Sultani CCM watatafuta pa kujificha lakini wakuwa smoked out popote watakapokimbilia.Huwakuti CUF kupigia makelele hujuma za ufisadi kwani wanajua kwa hapa tulipo itakuwa tunapoteza nguvu zetu na hakuna ambalo litamuathiri mtawala CCM zaidi ya kubadilisha na kuweka uoza mwengine. Hayo mambu yakikubalika kubadilishwa ndipo hapo kuwanadi mafisadi kutapata nguvu za kisheria na sheria kufuatwa na wahusika kuwajibishwa kisheria sio mtu anajiuzulu ndio habari kwisha.

Nchi imetulia na kuvumilia mengi yafanywayo kibabe na Sultani CCM ,CUF hadi hivi sasa au leo ni Chama kinachoshikilia wananchi wengi na kimeweza kuwaweka chini ya control yake ,nasema tena siku akitokea kiongozi wa CUF na kuamua kuanzisha mapambano na serikali basi yatakuwa mapambano ya kweli sio mchezo na hilo CCM wanalielewa ,wanajuwa kuwa CUF ni Chama hatari kwa ufisadi wao ,maana ukishakuwa na wananchi wanaokusikiliza na waliotayari kwa lolote basi wewe ni wa kusikilizwa na kuheshimiwa na kama hufanyiwi hivyo iko siku utafungulia wananchi wapambane na serikali iliyopo madarakani ,hilo sio jambo la mchezo ni roho kwa roho,kutakuwa hakuna usalama wala jeshi ni mapambano tu,ambush kila kona ,maana itakuwa sio piga tajame bali ni piga ni kupige.

Hawa viongozi hawatakuwa na uhuru tena wa kutembea na mashati na tai ,maana uvumilivu wa wananchi utakuwa haupo tena anytime anaweza kujitolea mwananchi na kufanya kweli tumeona ndogondogo ambazo zimetokea mbele ya mtu anelindwa na mabunduki na walinzi kanzu mmoja kavamiwa miguu tukio la pili kalambwa mtu kibao ,sasa hatujui tukio la tatu litakuwaje ,we wacha wafuasi wa sultani wacheze na amani wakiambiwa badilisheni hiki ,hatutaki wakiambiwa tunataka hiki hawataki basi walitakalo limeanza kuonekana kidogokidogo nalo ni kwa wananchi kushindwa kuvumilia na hapo inakuwa rahisi kuwaamuru kwa lolote lile.Ikiwa wafuasi wa CCM wanachukua chao mapema naona zamu ya wananchi nao kuwahi kulinda chao imekaribia.
 
Ukisoma vizuri alama za nyakati, CUF imepoteza mvuto wa kitaifa na kimkoa. Mgombea mtarajiwa yeyote mwenye kupiga hesabu vizuri hata kama anao mtaji wa wapiga kura, kugombea kupitia CHADEMA ndiyo turufu yenye uwezekano mkubwa wa kushinda ubunge.

CUF imo ndani ya nyoyo za wananchi,wanachama wengi wa CUF wameamka kimawazo na hawamthamini kiongozi zaidi ya Chama Chao hivyo wananchi wanaimani kuwa viongozi wamewekwa na wao na kiongozi akiondoka huwa hawababaiki nguvu zilizotumika kumfanya huyo alieondoka awe mashuhuri ndio hizo hizo zitakazotumika kumuinua mwengine na huo ndio mtaji wa CUF ,ni rahisi kuubadili moyo wa kiongozi kuliko moyo wa mwanachama wa CUF na hiyo ndio hazina ya CUF.
 
huyo lazima aondoke, amecheza na Maalim Seif. Yeye alitarajia apige kelele za CUF kutumia fedha nyingi kujijenga Zanzibar pekee badala ya bara halafu wamuache. Ndio maana pamoja na wajumbe wa bara kumpa kura nyingi na kumfanya aongoze kati ya waliopigiwa kura kwenye baraza la uongozi na kumzidi hata Haji Duni bado ametoswa!. Maalim Seif alimwambia wazi Lipumba asipendekeze jina lake. Huyu hakugombea akashindwa bali jina lake halijapendekezwa kabisa na mwenyekiti wao kwa kushauriana na katibu mkuu. Kimbelembele chake cha kupinga upemba ndani ya CUF ndio kimemponza. Kila siku ilikuwa kulilia tu chama hicho kijijenge bara kumbe wenzake wana ajenda nyingine kabisa

...........ndiyohiyo
 
Mimi naona asiende Chadema maana na mimi nilikuwa na mpango wa kwenda huko kwenye jimbo lake kugombea u MP kwa tiketi ya Chadema. Si kutakuwa na conflict of interest? LOL wakati uchaguzi unapowadia watu wa Daresalama na ulaya na Marekani pia uja majimboni kutafuta kula.(No nilitaka kusema kura)
Karibu Lwakatare usitie shaka tutagombea wote kwenye chama kwanza na kisha atakayeshinda ndiye atagombea rasmi kwa tiketi ya chama. Nikishinda mimi utajaribu unavyoweza kunipigia kampeni na ukishinda wewe nitakusaidia kukupigia kampeni. LOL
 
Mwanachama yeyote ambaye ni Kiongozi wa chama hicho, akikihama chama chake kwa kukosa uongozi, akahamia kwenye chama kingine, huwa anapoteza heshima yake kwa namna moja au nyingine.

Viongozi makini, huacha vyama vyao na kuunda chama kipya kingine ili kusuma ajenda mpya anayoihisi kuwa itakuwa na msimamo wenye maslahi ya nchi na wananchi wake. Kwa namna ambayo Kwame Nkrumah alivyofanya baada ya kuona wazee ndani ya chama wanakwenda kigoigoi.

Vinginevyo, Bwana Lwakatare atakuwa anaoiongeza orodha ya akina Lwamwai, Kabourou,
Tambwe Hiza na kubwa lao la hama hama Lyatonga Mrema. Wote hawana nyimbo hii leo.
 
CUF imo ndani ya nyoyo za wananchi,wanachama wengi wa CUF wameamka kimawazo na hawamthamini kiongozi zaidi ya Chama Chao hivyo wananchi wanaimani kuwa viongozi wamewekwa na wao na kiongozi akiondoka huwa hawababaiki nguvu zilizotumika kumfanya huyo alieondoka awe mashuhuri ndio hizo hizo zitakazotumika kumuinua mwengine na huo ndio mtaji wa CUF ,ni rahisi kuubadili moyo wa kiongozi kuliko moyo wa mwanachama wa CUF na hiyo ndio hazina ya CUF.

Mwiba.

Cuf inashindwa kuthamini mchango wa Lwekatare?kama ilivyoshindwa kumthamini Professor Safari Jumbe.soma maelezo yake kwenye gazeti la Rai www.newhabari.com amesema kuwa CUF upemba umezidi.

Cuf inatakiwa ijikite kwenye mijadala ya kitaifa sio suala la muafaka kila kukicha.kumbukeni NCCR-MAGEUZI walikuwa na wafuasi nyuma yao walipoona hakuna kitu wametimka.unajua kazi aliyoifanya Lwekatare Bukoba? chama sio Pemba tu basi mtakuwa hamna tofauti na Chadema ambao kwao Chama ni Kilimanjaro na hivi sasa timu yote inakazana na majimbo ya Kilimanjaro.

sehemu kama LINDI au MBEYA ambako Cuf na Chadema zilipata support kubwa lakini kama hamuwapitii wanachama mko busy na kilimanjaro au Chake chake basi vyama vyenu vitakosa sura ya utaifa.

CUF mbeya vijijini wamepata kura zaidi ya elfu kumi,kama mkiwapitia kila mara mnaweza kushinda lakini kama akili na fikra zenu ni muafaka tu mtakimbiwa na wanachama wengi.
 
Kama hii ni kweli then!!! I support the move!!! CUF ya kwatu waachie watu wa upande ule mwingine wa bahari
 
Mwanachama yeyote ambaye ni Kiongozi wa chama hicho, akikihama chama chake kwa kukosa uongozi, akahamia kwenye chama kingine, huwa anapoteza heshima yake kwa namna moja au nyingine.

Viongozi makini, huacha vyama vyao na kuunda chama kipya kingine ili kusuma ajenda mpya anayoihisi kuwa itakuwa na msimamo wenye maslahi ya nchi na wananchi wake. Kwa namna ambayo Kwame Nkrumah alivyofanya baada ya kuona wazee ndani ya chama wanakwenda kigoigoi.

Vinginevyo, Bwana Lwakatare atakuwa anaoiongeza orodha ya akina Lwamwai, Kabourou,
Tambwe Hiza na kubwa lao la hama hama Lyatonga Mrema. Wote hawana nyimbo hii leo.

Kwaminchi kuanzisha chama cha siasa sio rahisi kama unavyofikiria. Sheria haiko conducive na kuna vikwazo visivyo na msingi vingi sana yote haya katika kudumisha ukiritimba wa madaraka kwa chama tawala. Vilevile inahitajika pesa. Ni savings gani anazo bwana Lwakatare kutokana na mshahara wake wa cuf itakayomwezesha kuanzisha chama? Ni nani kati yetu seriously ambaye yuko tayari kumchangia? Kwaminchi uko tayari kuchangia kupanua wigo la demokrasia tanzania?

Sera za Cuf na Chadema hazitofautiani sana na ndio maana wanaongea lugha moja bungeni. Sana sana ni kwenye suala la muungano ndipo wanapotofautiana. Na hili ndilo lililosababisha Muganyizi avuliwe madaraka Cuf. Cuf na Chadema ndio vyama pekee vya upinzani ambavyo vimedhihirisha kwa nyakati tofauti kwamba vimeshakuwa institution; Pamoja na mengi mtu akiondoka havitetereki na mtu akiingia hapewi cheo kama zawadi au hongo.

Hivyo Lwakatare kuhamia Chadema kisiasa anacheza karata zake sahihi kabisa. Hangeweza kuendelea kukaa Cuf kwani alikuwa ana agenda tofauti na chama. Hangeweza kwenda ccm kwa kuwa hayuko kwenye siasa kwa sababu ya njaa.

Lwakatare alishindwa na Kagasheki kwa kura chini ya 200 katika uchaguzi uliopita. Kulikuwa na utata katika kujumlisha matokeo na malumbano kuzuka wakati wa kutangazwa mshindi hadi mtu akapigwa konde. Anao madiwani wanne katika halmashauri. Wagombea udiwani wake wote isipokuwa mmoja walishindwa kiutatanishi hivyo hivyo. Lwakatare alikuwa anakubalika Bukoba mjini 2005 hilo halina ubishi. Lwakatare bado ni jina kubwa Bukoba na bado linauzika. Kimsingi Lwakatare bado ni asset.

Cuf wameshindwa kuliona hili kwa kuwa wao agenda yao kubwa ni kujenga chama pemba. Swali ni kwamba anahamia Chadema na Cuf ya Bukoba? Anahamia Chadema na Cuf ya Kagera?

Kama ni hivyo litakuwa pigo kubwa sana Cuf kwani Kagera ni moja ya ngome zake zilizosalia Bara. Kama Chadema watamtumia Lwakatare na kutumia propaganda ya "vita vya upemba na ubara ndani ya Cuf" na kuwachukua viongozi wa Cuf bara hilo nalo litakuwa pigo lingine kubwa sana na litadhoofisha sana Cuf bara. Muganyizi alikuwa anakubalika sana ndani ya Cuf kwa wale wasio na msimamo mkali wa kidini ndani ya chama. Tusubiri tuone.
 
Rwakatare alipokuwa CUF alikifanya chama hicho kisionekane cha kidni (cha kiislam), sasa kama akijitoa ndio kitakuwa chama cha kidini haswa. CUF inaelekea kuzimuni
 
Hebu kuweni na upeo mkubwa wa kufikiria wazee!

Mmesahau kuwa Shaibu Akwilombe alitoka CUF akaingia CHADEMA, nini kilifuata baadaye!

Lwakatare aende popote hata saidia upinzani. Na acheni kudanganyana juu ya ubora wa CHADEMA kwa kusoma kwenye maelezo ya JF. Mnajiongopea wenyewe. Ubora wa chama ni kwenye mikakati ambayo Chadema haina zaidi ya publicity kibao ikiwemo humu!

Hao CUF kinachaowaumiza si Upemba au propaganda yeyote ila UBAHILI. Wakiwekeza vya kutosha kuimarisha chama huku bara, watakuwa juu.

NN
 
Back
Top Bottom