Lusekelo: Kawafananisha ma-dr. Wa tanzania na wauaji wa albino!!

Ndyali

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,661
948
Mchungaji Lusekelo awaponda
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Kibangu jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amewafananisha na wauaji wa albino madaktari waliogoma wakiishinikiza serikali iwatimizie madai yao.
Lusekelo aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema wanachokifanya madaktari hakina tofauti na watu wanaofanya mauaji ya albino ili wapate fedha zaidi ambazo hazina baraka za Mungu.
Aliongeza kuwa, madai hayo ya madaktari ni sawa na ufisadi zaidi ya ule uliofanyika katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje Benki Kuu (EPA).
“Madaktari wanafanya uuaji…. wanawaadhibu wananchi wasio na hatia, wao wanaidai serikali, sasa kwanini wanawaacha wagonjwa wafe ili kushinikiza kupata fedha zao?” alisema.
Aliongeza kuwa madaktari wanatakiwa kufahamu kuwa hicho wanachokidai kitawalazimu wananchi watozwe kodi kubwa jambo ambalo litawazidishia ugumu wa maisha.
Alisema madaktari wanapaswa kumuogopa Mungu na kurejea kazini kwani binadamu wanaishi kwa kutegemeana, hivyo wataalamu hao wasijione ni muhimu kuliko watu wengine.
Mchungaji Lusekelo alisema madaktari wamefanya dharau kubwa kukataa kuonana na waziri mkuu kuzungumzia madai yao.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

My take: Tapeli mkuu huyu anayetumia jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo,kuwatapeli watanzania ana usafi wowote wakuwakoromea Ma-Dr. wetu kwa kuwalinganisha na wauji wa Maalbino? Au ndo janja ya agent wa Shetani huyu kutafuta kulindwa na serikali ya magamba?
 
Angekuwa na roho wa Mungu angetoa sauti ya unabii, kwa kukemea dhuluma na ufisadi wa kupindukia Tanzania. Lakini kwa sababu ya majivuno na kujikweza, shetani anamtumia kwa kasi ya ajabu kwa wakati huu!! Na zile baraka alizokuwa nazo mwanzoni zinaendelea kupotea!! Ataendelea kuwa gizani kwa sababu ya kufuru na majigambo!! Ni kwa huruma tu ya Mungu, ataangaziwa mwishoni kabisa, kwamba mpakwa mafuta duniani na mbinguni ni mmoja tu, Yesu Kristo!!
 
Huyu anatafuta atoke vipi? CCM wameamua kutumia viongozi wa dini kupiga propaganda. Madaktari bingwa Mgomo wenu usikome
 
mbona hata yeye anawaibia waumini wake, kwani wizi nao si uuaji, aache kuangalia kibanzi kwenye macho ya madaktari wakati macho yake yana boriti. Nabii wa uongo.
 
Huyu ni Mnafiki mkubwa.
Kashiba sadaka za waumini wake anajirpokea tu.
Kwa matamshi ya namna hii naamini hata kondoo wa bwana zizi mwake wako hatarini.
Hapa USA Watumishi wengi wa bwana wajiitao wachungaji wamekubuhu sana katika kuwashambulia kondoo wao kwa makucha na meno yao bila huruma. Wanabaka kondoo waume kwa wake, wanavuta bangi, wanabwia unga zaidi wanatumia Fedha itolewayo na kondoo wanyonge kutanua Ki Hollywood.
Huu Mchungaji Lusekelo hamwogogopi Bosi wake ndiyo maana anachambua issue hii KiCCM.

Lumuhoma Lulo!

Mchungaji Lusekelo awaponda
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Kibangu jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amewafananisha na wauaji wa albino madaktari waliogoma wakiishinikiza serikali iwatimizie madai yao.
Lusekelo aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema wanachokifanya madaktari hakina tofauti na watu wanaofanya mauaji ya albino ili wapate fedha zaidi ambazo hazina baraka za Mungu.
Aliongeza kuwa, madai hayo ya madaktari ni sawa na ufisadi zaidi ya ule uliofanyika katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje Benki Kuu (EPA).
“Madaktari wanafanya uuaji…. wanawaadhibu wananchi wasio na hatia, wao wanaidai serikali, sasa kwanini wanawaacha wagonjwa wafe ili kushinikiza kupata fedha zao?” alisema.
Aliongeza kuwa madaktari wanatakiwa kufahamu kuwa hicho wanachokidai kitawalazimu wananchi watozwe kodi kubwa jambo ambalo litawazidishia ugumu wa maisha.
Alisema madaktari wanapaswa kumuogopa Mungu na kurejea kazini kwani binadamu wanaishi kwa kutegemeana, hivyo wataalamu hao wasijione ni muhimu kuliko watu wengine.
Mchungaji Lusekelo alisema madaktari wamefanya dharau kubwa kukataa kuonana na waziri mkuu kuzungumzia madai yao.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

My take: Tapeli mkuu huyu anayetumia jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo,kuwatapeli watanzania ana usafi wowote wakuwakoromea Ma-Dr. wetu kwa kuwalinganisha na wauji wa Maalbino? Au ndo janja ya agent wa Shetani huyu kutafuta kulindwa na serikali ya magamba?
 
Huyu Antony Lusekelo naye mbona amezidi kujipendekeza. Mbona yeye haoni anavyoua watu kwa kuwaongopea kuwa wanakwenda peponi wakati anacholenga ni kuwatoa sadaka na kula yeye na mke wake? Lusekelo anabidi akue aache utoto na kuendekeza njaa.
 
mwiz tu huyu magari ya kifahari ndo huduma ya kinabii eti. hata kanisan kwake kuna wahitaj wengi tu anawasaidiaje. drs siku akija anga zenu mwambieni arudie maneno aliyosema hapo juu.
 
Mchungaji na hummer/VXV8/Range Rover, muumini anapiga mkuki wa jero apeleke kwa mchungaji
 
Awaambie hapo wagonjwa waende kwake akawaponye, kama anavyoponya hao wengine. au kama vipi atie timu muhimbili akafanyie maombi pale, sio mbwe mbwe za kwenye TV
 
Lazima ajipendekeze kwa serikali kwa sababu pale kanisani kwake inatakiwa kupita barabara. Kwa kujipendekeza huko huenda serikali ikapitisha kwingine kwa kudhani kwamba wanatakiwa wamlinde mwenzao.
 
Angekuwa na roho wa Mungu angetoa sauti ya unabii, kwa kukemea dhuluma na ufisadi wa kupindukia Tanzania. Lakini kwa sababu ya majivuno na kujikweza, shetani anamtumia kwa kasi ya ajabu kwa wakati huu!! Na zile baraka alizokuwa nazo mwanzoni zinaendelea kupotea!! Ataendelea kuwa gizani kwa sababu ya kufuru na majigambo!! Ni kwa huruma tu ya Mungu, ataangaziwa mwishoni kabisa, kwamba mpakwa mafuta duniani na mbinguni ni mmoja tu, Yesu Kristo!!

Nilikuwa namuona kama mmoja ya watu wazuri waliosimama kuwainspire watanzania maskini kwa kuwapa moyo walipokuwa na shida chini ya kivuli cha dini,kwa kuwa dini ndio kivuli na mwamvuli mzuri wa binadamu yoyote anapokuwa anashida za kidunia ukimbilia na kuomba nafasi ya kuponya nafsi yake japo kazuridhika mwili ana akili yake.

Kanichefua sana sana sikutegemea hakika neema ambayo Mungu alionekana kumpa,itamkimbia hakika!!!!!!.Hivi usawa huu mbunge anaomba sitting allowance ya 200000 na dokta anayepewa overtime ya shillingi 10000 leo Mzee wa Upako anashabikia kweli na kusimama kuwatukana madokta wanaowatibu albino waliokatwa mikono na hao hao wenye puma ya imani ya kukata vioungo vya albino wawe viongozi na kupata utajiri.

Hakika sasa Mungu anaongea na watanzania kupitia Madaktari na si viongozi tena wa dini.
 
Kwa nini mwandishi wa Tanzania Daima alichagua kuongea na Lusekelo. Kama kilichokuwa kinatafutwa ni maoni ya kiongozi wa dini nadhani mtu kama Pengo angefaa. Ninahisi Lusekelo mwenyewe alimtafuta mwandishi.
Inavyoelekea ,ktk Tanzania, kila kiongozi wa dini , hata wachovu wa kutupwa wa fikra , wanajiona ni political commentator.
 
Back
Top Bottom