Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Lulu akiwa anaingia Mahakamani jana | Tuesday, May 08, 2012 12:52 PM ELIZABETY MICHAEL lulu jana aliiomba Mahakama ya Hakiumu Mkazi Kisutu kuhamisha kesi kwenye mahakama ya Watoto kwa kuwa umri wake hauruhusu kesi hiyo kusikiliziwa katika Mahakama hiyo |
Hayo aliyasema jana wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na kuzua minongono na mijadala na kuzuka kwa utata kuhusiana na umri wake Lulu anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba aliyefariki mwezi uliopita Lulu anatetewa na mawakili wapatao watatu ambao wanaongozwa na Keneth Fungamtama akisaidiana na Wakili Peter Kibatala na Fulgence Masawe. Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa, mteja wao huyo ana umri wa miaka 17 hivyo, kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Watoto. Mawakili hao walidai wana uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa huyo. Wakili Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni Yule aliye chini ya umri wa miaka 18 Hivyo kwa upande wa Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliwaomba wapewe muda zaidi kuhusiana na uchunguzi wa hilo na upepelezi dhidi ya mashitaka hayo yanaendelea hayajakamilika Na kutilia mashaka cheti hicho kwani cheti kilichowasilishwa Mahakamani kinasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo kwa jina la Elizabeth Michael. Tunaomba tupewe muda tuweze kuchunguza zaidi kuhusu umri wa mshtakiwa Hata hivyo Wakili mtetezi wa Lulu alijibu hilo na kudai kusomeka kwa Diana Elizabeth ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili. Hakimu Mkazi Augustina Mbando mara baada ya kusikiliza mashauri kutoka kwa pande zote mbili na mazingira ya kesi ilivyo na ilivyogusa jamii, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa tena. Awali ilidaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba. |