kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
10th February 2010
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, ametoa ruksa kwa malori, kenta, magari ya wazi kuwasafirisha wanafunzi wanaosoma nje ya Jiji.
Alitoa agizo hilo jana akiwa katika ziara ya kukagua shule za sekondari wilayani Ilala.
Lukuvi alisema vitatolewa vibali kwa magari yatakayoomba kutoa huduma hiyo kupitia kwa mkuu wa wilaya ili Polisi wa Usalama Barabarani wasiyakamate.
Aidha, alitoa wito kwa watu binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga mabweni kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule zao.
Lukuvi alitembelea shule ya Msongola, Kivule Abuu, Jumaa, Vingunguti pamoja na Gerezani ambapo wanafunzi walimueleza kuwa wanakabiliwa na matatizo ya usafiri, uhaba wa walimu na ukosefu wa mabweni.
Akiwa katika Shule ya Sekondari Abuu Jumaa, Lukuvi aliwakuta baadhi ya wanafunzi wamekaa chini na Sekondari ya Kivule wakiwa wamekaa kiti kimoja wanafunzi wawili lakini kila mmoja na dawati lake.
Alimuagiza Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bernard Mkali, kuorodhesha majina ya wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa shule za mbali kuwapa uhamisho kuanzia leo ili waepukane na adha hiyo.