SoC03 Lugha ya Taifa(Kiswahili Sanifu) hatarini kuanguka

Stories of Change - 2023 Competition

Kaka Ibrah

Member
Sep 6, 2022
83
63
kiswahili.jpg

Chanzo picha: www.globalpublishers.co.tz

UTANGULIZI
Kiswahili ni lugha ya kibantu iliyotokana na mchanganyiko wa baadhi ya maneno kutoka katika makabila mbalimbali ya nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa uchache. Lakini pia baadhi ya maneno ya kiarabu yamesaidia katika kuundwa kwa lugha ya Kiswahili. Lugha hii hutumika kama lugha ya taifa nchini Tanzania. Katika miaka kadhaa nyuma lugha hii imeshika hatamu na kuvuka mipaka hadi nchi jirani za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.

KUKUA KWA LUGHA YA KISWAHILI
Hapo mwanzo lugha ya Kiswahili ilikuwa ikitumika katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki kama vile Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Tanga na Pwani kwa upande wa Tanzania, pia Mombasa na Lamu kwa upande wa Kenya. Lakini baadae kilikua na kuzidi kusambaa katika sehemu zingine za ukanda wa maziwa makuu (Afrika Mashariki) kama vile Burundi, Kongo DRC na Sudan ya Kusini. Kwa sasa lugha hii tayari imeshakita mizizi na kuzidi kupendwa mpaka nchi za mbali kama vile Ujerumani, Uturuki, Oman, Japan, Uchina, Uingereza, Iran, India na hata Australia. Vilevile pia katika jumuiya ya umoja wa nchi za kusini mwa Afrika (SADEC).

Yapo mambo kadhaa yaliyo pelekea kukua na kusambaa kwa lugha ya Kiswahili, mambo haya ni kama:

Biashara;
Maendeleo ya biashara miongoni mwa watu yamesaidia pakubwa kukua na kusambaa kwa Kiswahili. Watu kutoka taifa moja ama jingine wamelazimika kujifunza lugha ya Kiswahili, hasa pale wanapohitaji kuja kufanya biashara ndani ya nchi yetu ya Tanzania kwa muda mrefu zaidi. Hii imewezesha Kiswahili kuendelea kupanuka kwa mataifa mengine zaidi kutokana na haja za wageni kuja kuwekeza hapa nchini.

Runinga na Redio; Njia ya runinga na redio ni moja kati ya njia ambayo imekuwa ni yenye nguvu zaidi hasa katika zama hizi katika kusaidia kukua na kusambaa kwa lugha hii ya Kiswahili. Runinga na redio zetu hapa nchini hulusha vipindi mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili ambako watu wa nnje ya nchi huweza kufikiwa pia na kupata vitu vipya ndani ya Kiswahili. Lakini pia zipo redio kadhaa katika mataifa ya ughaibuni ambazo hulusha vipindi mahususi kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kiswahili, mfano; China Radio International (CRI Kiswahili), Radio France International (RFI Swahili), TRT Swahili (kutoka Uturuki), Radio Iran, Radio Japan na zingine nyingi. Uwepo wa hizi runinga na redio, kwa ujumla zimepelekea mapinduzi makubwa ya lugha ya Kiswahili ulimwenguni.

Mitandao ya kijamii; Uwepo wa mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp, Telegram na Facebook, imechangia kwa kiasi chake pia katika kukikuza Kiswahili kwa watu tokea nchi tofautitofauti duniani. Wadau na walimu walio wazalendo wa taifa letu, wamekuwa wakiunda majukwaa maalumu huko kwa ajili ya kufundisha Kiswahili. Watu tokea nnje ya nchi wasiohafamu Kiswahili huvutiwa na kujiunga na hayo majukwaa kwa ajili ya kuelimika zaidi.

Filamu na sinema za maigizo; Njia hii imekuwa ni chachu kubwa katika kuikuza lugha ya Kiswahili. Kwa sasa nchi yetu ya Tanzania inawabunifu wengi wa kuandaa filamu na sinema za maigizo kwa lugha ya Kiswahili, jambo ambalo limekuwa ni jema sana hasa katika kukitangaza Kiswahili kwa mataifa wengine ambao hupenda kufuatilia filamu hizi za kitanzania. Pia hapa wachambuzi wa filamu (MC/MCs) zitokanazo na lugha za kigeni, huweza kuzitafsiri hizo filamu kwenda katika lugha ya Kiswahili ambapo wengi huvutiwa nazo. Na hapo ndipo huwa mwanzo wa mataifa kujifunza Kiswahili na kisha kukua na kusambaa.

Fahari ya kufahamu Kiswahili; Baadhi ya watalii wanapofika nchini hupenda kujifunza walau misamiati au mambo kadhaa ya lugha ya Kiswahili, mfano; salamu, jinsi ya kumkaribisha mgeni nyumbani kwako, jinsi ya kuomba kitu flani au msaada kutoka kwa mwingine, nakadharika. Wapo ambao pia kwa matamanio yao binafsi hutamani kujua lugha hii na hivyo hulazimika kujifunza kwa njia ya mtandao (Online). Hii nayo imefanya Kiswahili kukua na kuenea katika sehemu zingine za dunia.

Kila inapofika tarehe 7 Julai huwa ni siku ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili duniani. Lakini kuna hatari kubwa mbele yetu kama hatutoiheshimu lugha yetu katika namna jinsi ya kuituma kwa ufasaha. Lugha hii haitumiki kwa usanifu tena. Kadri jinsi muda unavyo zidi kusonga mbele, ipo siku tutakuja adhimisha siku hii kwa masikitiko badala ya furaha, na kama kutakuwa na furaha basi ni furaha ya kinafiki.

Je; ni mambo gani haya ambayo yanaashiria anguko kubwa la lugha ya Kiswahili:

Lugha za kigeni kupewa kipaumbele;
Lugha za kigeni kupewa kipaumbele zaidi imesababisha kuathiri pakubwa lugha ya Kiswahili katika ufasaha wake. Maneno mengi yameweza kuvuviwa kutoka katika lugha hizi na kusababisha kuathiriwa hata kwa mazungumzo ya kawaida tu kati ya mtu na mtu. Kiingereza na Kifaransa ni miongoni kati ya lugha ambazo zimepelekea kuathiriwa kwa Kiswahili fasaha hapa nchini.

Ukosefu wa walimu wa Kiswahili fasaha; Katika karne ya 20 nchi yetu ilikuwa na walimu wazuri wa lugha ya Kiswahili waliokuwa wakijua vizuri Kiswahili fasaha. Waliweza kufundisha kwa ustadi mkubwa wanafunzi ambao nao baadae walikuja kuwa walimu wazuri katika kipindi cha karne ya 20 mwishoni na katika karne hii ya 21 mwanzoni. Lakini kadri jinsi siku zinavyo zidi kusonga mbele, walimu wenye uwezo wa kufundisha Kiswahili fasaha wanazidi kupungua, na hii ni kutokana na kwamba hata wao wanaathiriwa pakubwa kwa kuthaminishwa kwa hizi lugha za kigeni nchi mwetu Tanzania.

Kutafsiri filamu na sinema za Kiswahili kwa lugha za kigeni; Kwamfano, utakuta filamu ama sinema imechezwa kwa lugha Kiswahili kisha badala ya kuiuza hivyohivyo ili na wao wakatafsiri kwa lugha zao, tunajikuta tunawatafsiria tena kwa lugha za kigeni kama vile Kiingereza. Hii desturi kamwe haiwezi kukikuza Kiswahili katika viwango vya kimataifa badala yake ni kukididimiza dimbwini kabisa na kubaki kuwa watumwa tu wa lugha za wengine.

Matumizi ya Kiswahili cha mtaani katika maeneo yasiyo rasmi; Siku hizi tunaona Kiswahili cha mtaani kikitumika tu pasina wasi hata katika maeneo ambayo si sahihi kitumike huko. Mfano, katika vipindi maalumu vya redioni au katika runinga (Serious Programs). Waandishi ama watangazaji hawana uelewa tena juu ya hili. Katika vipindi maalumu ambavyo vinapaswa Kiswahili fasaha kitumike, wao wanabatilisha wanafanya kutumia hata Kiswahili cha mtaani wakisahau kuwa wanasikilizwa na watu wa aina mbalimbali. Zipo sehemu zingine ambako Kiswahili cha mtaani si vyema kitumike lakini kinazungumzwa, mfano; bungeni na hospitalini.

Utunzi mbovu wa mashairi (nyimbo) kwa baadhi ya wasanii; Mfano wasanii wanaofanya mziki wa Hiphop na hasa zaidi wale wanaofanya mziki wa kizazi kipya (Bongo fleva). Hawa nao wanapaswa kulaumiwa kwa kusababisha anguko la Kiswahili fasaha ndani ya nchi yetu Tanzania. Ni tofauti na wasanii wa zamani kipindi mziki unachipukia ambao walijitahidi kuzingatia vyema misamiati ya Kiswahili wakati wa utunzi wao. Mfano akina Selemani Msindi (Afande Sele), Joseph Haule (Professor J), Maalim Nash (Nash MC), na baadhi kadhaa. Lakini baadhi ya wasanii wa hivi karibuni wanaipoteza heshima ya lugha ya Kiswahili kwa utunzi mbovu, hata mtu mgeni nchini akisema asikilize wala hawezi akaelewa kinachoongelewa. Mfano wa wasanii hawa ni Mabantu, Marioo, Zuchu na wengine wengi.

NINI KIFANYIKE ILI KUKINUSURU KISWAHILI FASAHA DHIDI YA ANGUKO HILI

(a) Kuhamasishwa kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili fasaha kwa wingi zaidi katika maeneo yote.

(b) Baraza la sanaa na michezo Tanzania (BASATA) kuhakikisha nikapitia kazi zote wa wasanii kwa kukagua kazi zao kama zipo katika utunzi wenye ustadi makini.

(c) Makampuni yanayo miliki filamu na sinema za kitanzania kutoruhusiwa kutafsiri filamu hizo kutoka lugha ya Kiswahili kwenda katika lugha za kigeni. Chamsingi waandaaji wajitahidi kucheza filamu bora ili ziweze kuuzika katika soko la kimataifa hata pasipo kuwa zimetafsiriwa, kwani watatafsiri kwa lugha zao.

(d) Serikali ianzishe jukwaa maalumu la kitaifa la lugha ya Kiswahili ambako mtu awaye yote ataweza kujisajili na kushiriki masomo ama mijadala mbalimbali juu ya lugha ya Kiswahili pekee, ili kuendelea kupeana maarifa zaidi juu ya namna ya matumizi sahihi ya Kiswahili fasaha. Itafaa zaidi kama jukwaa hilo litaweza kupatikana katika mitandao ya kijamii maarufu hapa nchini, mfano; Facebook, YouTube na Instagram.

(e) Serikali iweke shinikizo la lazima kwa vyombo vya habari vyote nchini kuwa na vipindi vya lugha ya Kiswahili. Hapa wataalamu wa Kiswahili watakuwa wakialikwa redioni ama katika runinga (TV) kwenda kutoa somo juu ya mada itakayokuwa mezani siku hiyo.

HITIMISHO
Iwapo kama mambo haya yatazingatiwa kikamilifu; hakika tutakiokoa Kiswahili dhidi ya anguko kuu. Hii itasaidia kukipaisha Kiswahili fasaha katika mataifa mengine. Itasaidia kukifanya Kiswahili cha nchi yetu kutambulika kama ndicho Kiswahili pekee kinachozungumzwa kwa ufasaha ulimwenguni kote. Iwapo Kiswahili kikitumika vizuri na kwa ufasaha itatengeneza heshima ya nchi yetu na hakika kama taifa tutalamba asali iliyojificha sirini mwa lugha ya Kiswahili.

"Kipende Kiswahili kama unavyopenda maadili, kupenda asili ndipo penye wingi wa fadhili".
 
Nakukaribisha wewe kuweza kusoma na kupigia kura yako katika andiko hili ili mkombozi ufanyike juu ya lugha yetu tamu ya Kiswahili. Sehemu ya kupigia kura ni hapo chini mwisho wa chapisho kuna sehemu imeandikwa vote, bonyesha hapo na kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umepiga kura yako.
 
View attachment 2669532

Wasomi wetu na viongozi wa ngazi za juu (wafanya maamuzi) ambao tunategemea au tuliwategemea kuita na kuendesha mjadala wa kitaifa ili mwisho wa siku tukubaliane na kwenda na lugaha ya kiswahili katika kufundishia kuanzia msingi, sekondari hadi chuo kikuu, ajabu wao ndo wamekua waoga, kimya kami vile kuna maslahi fulani wanapata kwa kuzishikiria lugha za kigeni. Lugha mama ni maarifa
 
Ni kweli kaka tatizo viongozi wetu
 
Back
Top Bottom