Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Lowassa hawezi kamwe kuwa raisi, jiulize ni kwanini alijiuzulu uwaziri mkuu kwanza.

Wakuu
kweli Lowassa ana madudu aliyo yafanya, lakini tuangalie tangu ameondoka madarakani ni kwa kiasi gani mambo ya mesambalatika.
Nina mkumbuka lowassa aliyengo'oa mabati ya mwarabu aliyekuwa amechukua uwanja wa mnazi mmoja enzi za Rais Mwinyi.
Lowassa alikuwa waziri wa Ardhi. Namkumbuka Lowassa ambaye kama waziri mkuu tulisia watendaji serikalini wakufukuzwa wenine kusitafishwa, leo hata watu wakitandikwa risasi zilizo nunuliwa na kodi yao wenyewe hakuna anayechukuliwa hatua.

Pamoja na mapungufu mengi ya Edward na kuondoka madarakani nadhani kumwemwazili mkuu wetu kwa kiasi kikubwa inaelekea kana kwamba yeye ndo alikuwa mtawala wa nchi.

Kilichomponza ni uroho, tamaa za kujilimbikizia mali. Jambo ambalo hivi sasa tukimtafuta nani mwema au mzuri ktk watendaji wetu wa leo tukianzia juu hadi wachini kabisa tusije shangaa asipokuwepo wa kuanza kumrushia mawe (kurusha mawe nimechukulia mfano wa Yesu alipo wauliza anayejiona ni safi hana kosa awe wa kwanza kumrushia mawe mtuhumiwa aliyekuwa ameshitakiwa kwake).

Mwisho, tunalo tatizo watanzania hatuna viongozi makini kwa sasa,Mungu atusaidie.
 
Tungekuwa kwenye nchi za wenzetu, haya yanayotokea sasa tungekuwa tumesha yasahau siku nyingi.

1. tuhuma za ufisadi - watu wangekuwa wamesha fikishwa mahakamani siku nyingi,
2. kiongozi kushindwa kuongoza - vote of no confidence siku nyingi,
3. matumizi mabaya ya ofisi ( hata kama ni tuhuma tu) - huna kazi

Ndio maana wenzetu wanaendelea na kutuacha tumesimama. Watanzania tunasubiri nini?

Nakubaliana na wewe wala usiende mbali ,hapa hapa kwa jirani zetu waganda hivi sasa makamu wa Rais [Bukenya] wao aliyetemwa juzi na M7 hivi sasa anangoja kupelekwa mahakamani kujibu mashitaka ya matumizi mabaya ya ofis!! Sisi hapa bado tunakenua meno tu na nchi inadidimia.
 
Lowassa hawezi kamwe kuwa raisi, jiulize ni kwanini alijiuzulu uwaziri mkuu kwanza.
jiulize wewe, mtu muovu anajiuzulu? hapana anaogopa kushitakiwa, la sivyo kina Nahodha na Mwinyi mdogo, Ngeleja wangejiuzulu, nae kikwete angejiuzulu, sasa lowassa amejiuzulu kuwapeni nafasi mumchunguze kama ameiba, mbona ridhiwani na babake hawafanyi? Lowassa ni Msafi na ndio nyundo pekee ya kuokoa nchi hii, kumbuka hata mwinyi mkubwa aliwahi kustaafu uwaziri baada ya kupata skendo kama ajali hiyo ya lowassa, je urais hajaupata?
 
Kiukweli... Nchi inahitaji kichwa cha Dr.slaa peke yake. Tusiendelee kuwapamba hawa wala nchi eti walifanya ya msingi, hebu jiulize kwanini walijilimbikizia mali za walipa kodi wenye kipato cha chini na kusahau maslahi ya taifa? Lowasa hatufai hata kwa chumvi,wala sukari... Na wanatakiwa kuulizwa cortini siku moja
 
hii timu ya lowasa sasa hivi imekuja kwa kutumia kivuli cha dr slaa, nimewaona sana na kampeni zao mitandaoni kama facebook wanasema rais wa 2015 ni lowasa au dr slaa (ccm vs chadema), hawamtaji dr kwa mema ila ni kupunguza ukali wa neno lowasa for prezidaa 2015
 
Lowassa ndie nyundo pekee ya kuokoa tanzania, kwanza ni mkali balaa, nyerere hakumpenda kwani shahidi wa sokoine, na pia anajua kilichomuua sokoine yaani ile ajali ya kidizaini baada ya sokoine kuwa tayari kuingia ikulu na kuleta mabadiliko ambayo nyerere hakuyapependa
 
Kiukweli... Nchi inahitaji kichwa cha Dr.slaa peke yake. Tusiendelee kuwapamba hawa wala nchi eti walifanya ya msingi, hebu jiulize kwanini walijilimbikizia mali za walipa kodi wenye kipato cha chini na kusahau maslahi ya taifa? Lowasa hatufai hata kwa chumvi,wala sukari... Na wanatakiwa kuulizwa cortini siku moja

Lowassa pesa aliyokuwanayo ni yake na yote halali asilimia 100, nyie Dr slaa analipwa posho nzuri na anastahili, je akiwekeza na Familia yake hiyo posho na kuwa pesa nyingi nae Dr slaa ni Fisadi? acha akili ya mtu mweusi hiyo, Lowassa ana kibarua na biashara kwa miaka 40 sasa, ndio aendelee kuwa masikini ali aaminike?
 
Jamani hivi kuna watu wako serious kabisa wanataka Lowasa awe rais wa nchi hii tena 2015 tu? Kweli? Yaani kweli kabisa mnafikiria na mnataka awe rais wa Tanzania?
 
.
Ee Mola endelea kunipa uhai ili niweze kuona madudu zaidi yaliyofanyika kumwingiza JK madarakani...Niweze kuona mwisho wa unafiki wa JK...Niweze kuona mihtasari ya mikutano ya siri iliyoongozwa na EL kupanga njama za kukwapua fedha za EPA ili JK aingie madarakani..Niweze kuona CCM ikimeguka mapande matatu..Niweze kupata ukweli wa chanzo cha chuki ya JK kwa Cigwiyemisi, Mkapa na Dr Salim..Niweze kupata ukweli kuhusu uhusiano wa JK, RA na Kagoda..........Aaamin!
Ameeeeeeeeeeeen! Mungu atutunze mpaka tuyaone yote hayo. Yaani kila kukicha mambo mapya na magumu zaidi yanaibuka
:dance:
 
Mmmmmh mimi kwwli kwa mwenendo wa sasa wa serikali mi naona kuna mvutano mkubwa sana wa mambo yafuatayo.

1. kuna kundi ambalo linaona kweli wameshindwa kuongoza serikali na hawastahili so wanataka kujivua gamba serikalini kabisa........nadhani hata JK anataka sema hasemi tu.

2. kuna kundi ambalo wanaona wameshindwa kuongoza kabisa ila wanagangamala tu kibongobongo butua liende.

3. kuna wale wenzangu na mimi ambao hata ukiwasha moto machoni mwao hawaoni... wenyewe wanaona wako sawa kabisa na wanaongoza vizuri so nao wanagangamala na upuuuzi wao.

IPO SIKU MKULIMA ATASHIKA JEMBE NA ALIME KICHWA CHA MTU NDIPO TUTAMBUE KUMBE ANAHITAJI HAKI
Mkuu Hapo kwenye Red nakugongea thanks kabisa, hata mm nimeshachoka mkuu
 
Mmoja kati ya hao akiwa rais, itabidi vijana tuingie msituni! Wote ni mafisadi wasio na maadili na wana agenda ya ukanda!
 
Ee Mola endelea kunipa uhai ili niweze kuona madudu zaidi yaliyofanyika kumwingiza JK madarakani...Niweze kuona mwisho wa unafiki wa JK...Niweze kuona mihtasari ya mikutano ya siri iliyoongozwa na EL kupanga njama za kukwapua fedha za EPA ili JK aingie madarakani..Niweze kuona CCM ikimeguka mapande matatu..Niweze kupata ukweli wa chanzo cha chuki ya JK kwa Cigwiyemisi, Mkapa na Dr Salim..Niweze kupata ukweli kuhusu uhusiano wa JK, RA na Kagoda..........Aaamin!

sala yako inafanyiwa kazi,utapata majibu hv karibuni
 
2015 kuna uwezekano wa Dr Slaa kushinda kama atapewa nafasi na Chadema, lakini kama ikishinda CCM tuombe iwe Lowassa, hatuangalii chama, tunamtafuta mtu jasiri tu
 
2015 kuna uwezekano wa Dr Slaa kushinda kama atapewa nafasi na Chadema, lakini kama ikishinda CCM tuombe iwe Lowassa, hatuangalii chama, tunamtafuta mtu jasiri tu

Lowassa kwa chama gani???.... CCM hawamtaki mbona hamuelewi?
 
Mmoja kati ya hao akiwa rais, itabidi vijana tuingie msituni! Wote ni mafisadi wasio na maadili na wana agenda ya ukanda!

Kama babu Pinda hajatia mguu Zanzibar sehemu muhimu kabisa ya Tanzania, naona anaogopa nae huyu mlegevu kuliko hata kikwete, ndio maana akiona mgonjwa au albino analia badala ya kuunguruma kama Lowassa, yeye alikuwa anaenda Zanzibar mara 3 au 4 kwa mwaka na alikubaliana nao sana.
 
Rais ni Lowassa, kwanza ni mkali na ana uzoefu kuliko Dr Slaa
Ndugu yangu sisi hatutafuti mbwa hadi awe mkali, tunataka kiongozi ambaye ni mwadilifu, mchapa kazi na mwenye uelewa wa mambo ya kiuchumi na kisiasa ili iwe ni rahisi kupanga nini viwe vipaumbele, sio Lowasa aliyetaka atuletee mvua toka thailand.
 
asilimia 60 ya wapiga kura watakaopiga kura 2015 hawatafanya jambo linalostahili na linalohitajika na tanzania
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom