Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotakiwa wajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi wamekutana na uongozi wa juu wa chama chao, na taarifa zinasema bado mvutano haujaisha kati ya pande mbili hizo.

Taarifa za hakika zimeliarifu Raia mwema kwamba walikutana na makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, wiki iliyopita, na kwamba mmoja wao, Edward Lowassa, Bado ana donge.

Habari zinaeleza kwamba Lowassa (Mbunge wa Monduli), Rostam Aziz(Mbunge wa Igunga) na Andrew Chenge (Mbunge wa Bariadi magharibi) waliitwa ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Dar es Salaam wakitakiwa kutekeleza uamuzi wa NEC.

Lakini habari kutoka kwa watu wa karibu na Lowassa zinaeleza kwamba mwanasiasa huyo amebainisha kwamba hakubaliani na uamuzi wa NEC.

“Mzee (Lowassa) amesema kwamba aliitwa na kwamba alitakiwa kuachana na suala la urais ili mambo yaishe, lakini amewaambia uamuzi wowote kisiasa ni haki yake kikatiba, na hivyo hakubaliani nao” anasema Mbunge mmoja ambaye yuko katika kambi ya Lowassa akiongeza:

“Ila wajue kwamba wao wakimwaga mboga sisi tunamwaga ugali”. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, Rostam Aziz na Chenge wanaonekana kulegeza kamba katika suala hilo.

Anasema mbunge huyo “Rostam amesema wazi kwamba hawezi kushindana na Rais aliye madarakani hata kama watakuwa wameonewa.

Chenge anakubali tu kwasababu anaona hana jinsi.

Lowassa bado moyo wake ni mzito”…………………………………………………………………………………………………….Gazeti lilipotaka

Lowassa alizungumzie suala hilo alijibu “No coment, No coment, No coment”

Taarifa ambazo Raia mwema limezipata zinaeleza kuwa tayari viongozi hao ambao wote ni wajumbe wa NEC na walihudhuria kikao kilichoazimia wajiuzuru, wameshakabidhiwa barua rasmi za kuwataka wajiuzuru zikirejea uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.


Source:

Raia Mwema June1-June7, 2011
 
Lowasa ni kikwazo kikubwa sana kwa JK, kitu kingine ambacho kitakuja kumgharimu JK ni undumi la kuwili alio kuwa nao. Akiwa na Lowasa anaongea vitu vingine, na akiwa na Mukama anaongea vitu vingine.

Sasa hii kitu mbaya sana, ndio maana lowasa alimshangaa Mukama kwa maneno aliyokuwa anamwambia,"Lowasa:

"Nimeongoea na JK akuniambia maneno haya ambayo wewe unaniambia hivi sasa"

Sasa hii kitu ndio itakayo kuja kuleta madhara. Na ni mbaya sana kuwa changanya watu hasa marafiki zako na hii pia ni angalizo kwa NAPE.
 
lowassa usikubali komaa naye bora muumbuke wote

Na huko ndiko tunako elekea,lowasa anafanya kila njia ili kuweza kumuaribia JK hasa kitika serikali yake,ndio maana kwa sasa Lowasa ana mtumia sana kubenea ili kuweza kuwaharibia wakina sitta na mwakyembe ili tu aweze kuyumbisha serikali ya jk.Na kwa hili atafanikiwa tu maana inaonekana amejipanga,hata ukisoma mwanahalisi ya leo kuna kitu unaweza gundua,Mwanahalisi wanachokifanya kwa sasa ni kuwapiga Mwakyembe na Sitta kwa ishu ya CCJ toleo lililopita na toleo la wiki hii mada nyingi ni zile zile.Wanaanza kwa kuwapiga mapacha watatu kidogo halafu wanahamia kwa Sitta na mwakyembe na hili ndio dhumuni la mwanahalisi kwa sasa.
 
Mimi nadhani Lowassa kama Mwanasiasa mkongwe alitakiwa a-step down tu, kwasababu system haimtaki tena kwasababu kaichafua. sasa akimwaga ugali yeye itamsaidia nini? afanye kitu ambacho kitamfanya arudishe heshma yake na siyo kuwa na "moyo wa tukose wote"
 
magamba kwa magamba,sio mchezo. hata kama ni urafiki but rais km rais lazime awe na maamuzi magumu. haiwezekani kuchekacheka na watu ovyo ovyo. rais muda mwingine inatakiwa unatoa maamuzi hata ya kuua mtu/watu ambao ni raia wako. rais sharobaro,lazima uyumbishwe.
 
EL has the constitutional right to vie for the presidency in 2015 if he so wishes. If he refuses to surrender his political party posts voluntarily, CCM can force him out of the party through its normal channels. This move will put EL at a cross-road, and might tarnish his dreams of living in the state house after JK ends his term of office.
 
Kumekucha. Nakaa mkao wa kula ili kuona mechi. Nasubiri kupewa kiingilio. Mechi itakuwa kali sana. ila Mwalimu aliwahi kusema chama imara kitatoka ndani ya CCM
 
I will give my vote to lowassa if he vies for presidency!

Mimi pia ila itabidi kwanza iundwe tume huru(,sio ile kamati ya majungu ya akina Mwakyembe) kuchunguza kashfa zake zote.
 
manake magaamba haya yalikuwa yameanza kukomalia mwilini mwa nyoka wetu, hayavuliki kwa nini?
nasubiri japo gamba la mkiani lijitoe, sioni,
Hivi, (just a thought) mfano lowassa, Rostam, and Chenge wakitoka CCM, tutasema ndio imekuwa safi? au tutaongezea wengine kwenye listi?
 
Lowasa mwagaaaaaaaa! Ndio wakati wa Chama cha Magamba kung'ooka

hawezi mwaga chochote.......anajua nini anafanya.........muulizeni walipokutana na jk siku ile kule zenji jk alimwambia nini katika yale mazungumzo yao?.........

jk ni ndumilakuwili sana na bonge la nafiki lile.........
 
jk anawatuia kina msekwa kuonyesha kuwa kuna kitu kinafanyika halafu nyuma ya pazia anamwita lowasa na kuteta nae............hahhaahh
 
Vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotakiwa wajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi wamekutana na uongozi wa juu wa chama chao, na taarifa zinasema bado mvutano haujaisha kati ya pande mbili hizo. Taarifa za hakika zimeliarifu Raia mwema kwamba walikutana na makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, wiki iliyopita, na kwamba mmoja wao, Edward Lowassa, Bado ana donge.
Habari zinaeleza kwamba Lowassa (Mbunge wa Monduli), Rostam Aziz(Mbunge wa Igunga) na Andrew Chenge (Mbunge wa Bariadi magharibi) waliitwa ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Dar es Salaam wakitakiwa kutekeleza uamuzi wa NEC.
Lakini habari kutoka kwa watu wa karibu na Lowassa zinaeleza kwamba mwanasiasa huyo amebainisha kwamba hakubaliani na uamuzi wa NEC. Mzee (Lowassa) amesema kwamba aliitwa na kwamba alitakiwa kuachana na suala la urais ili mambo yaishe, lakini amewaambia uamuzi wowote kisiasa ni haki yake kikatiba, na hivyo hakubaliani nao anasema Mbunge mmoja ambaye yuko katika kambi ya Lowassa akiongeza: Ila wajue kwamba wao wakimwaga mboga sisi tunamwaga ugali. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, Rostam Aziz na Chenge wanaonekana kulegeza kamba katika suala hilo.
Anasema mbunge huyo Rostam amesema wazi kwamba hawezi kushindana na Rais aliye madarakani hata kama watakuwa wameonewa. Chenge anakubali tu kwasababu anaona hana jinsi. Lowassa bado moyo wake ni mzito.Gazeti lilipotaka Lowassa alizungumzie suala hilo alijibu No coment, No coment, No coment

Taarifa ambazo Raia mwema limezipata zinaeleza kuwa tayari viongozi hao ambao wote ni wajumbe wa NEC na walihudhuria kikao kilichoazimia wajiuzuru, wameshakabidhiwa barua rasmi za kuwataka wajiuzuru zikirejea uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.


Source: Raia Mwema June1-June7, 2011

Ee Mola endelea kunipa uhai ili niweze kuona madudu zaidi yaliyofanyika kumwingiza JK madarakani...Niweze kuona mwisho wa unafiki wa JK...Niweze kuona mihtasari ya mikutano ya siri iliyoongozwa na EL kupanga njama za kukwapua fedha za EPA ili JK aingie madarakani..Niweze kuona CCM ikimeguka mapande matatu..Niweze kupata ukweli wa chanzo cha chuki ya JK kwa Cigwiyemisi, Mkapa na Dr Salim..Niweze kupata ukweli kuhusu uhusiano wa JK, RA na Kagoda..........Aaamin!
 
Mwaga ugali urudishe heshima yako iliyogalagazwa kwanini uaibishwe kwa manufaa ya watu?? Mwaga mwaga tuone wenzio wameshamwaga mboga wewe unangoja nini??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom