Lowassa to strike back ; Mbowe to quit chairmanship?

Je itakuwa bora kwa Chadema kuwa na uongozi mpya kabisa kuelekea Uchaguzi Mkuu au kubadilishana vyeo mbalimbali kwa sababu mabadiliko yoyote yatakayofanyika wakati huu ndiyo yataamua Chadema inafanya nini kuelekea 2010.
 
mambo yote ni timing tu. timing ikiwa mbaya hata a-strike back vipi impact
kwa mlengwa itakuwa kiduchu. kuipata hiyo timing kunahitaji umakini na uelewa wa hali ya juu ya mwenendo wa siasa za hapa nyumbani.
 
kikwete naona alikosea 'kumtosa swahiba-wake' kwa mtindo ule.alitakiwa AFE NAE TU,AMBEBE MPAKA MWISHO auajiuzulu nae.kuna uwezekano mkubwa tu swala la richomond j.k alikuwa analijua
 
hili suala la Lowasa mi linaniumiza kichwa.msifurahie burudani lowasa akinena juu ya richmonduli.anaweza asipate hata hiyo nafasi meaning this is Tanzania and Shit happens.vitu kama ajali za barabarani,pressure.wabunge wangapi wamekufa kwenye ajali tokea 2005.personaly this can be a tragic event..mi naona Richmonduli ni Movie nzuri sana.mwanzo kutamu,kati panasisimua.mwishoni je?tungoje bubu aongee.na alishasema bungeni wamemuonea.na akiongea na Jk yuko involved kwenye movie bac hata mwakyembe na kamati yake ni mafisadi..maana hata wao walisema kuna mambo waliyatoa kuinusuru serikali.Mungu Ibariki Tanzania.
 
"Nimetafakari sana kwa niaba ya wananchi wangu wa jimbo la Monduli na kwa niaba ya chama changu Chama Cha Mapinduzi....." EL siku alipojiuzuru. Kama EL bado anaamini katika filosofia/falsafa ya kutafakari mambo kwa niaba ya chama chake (kitu ninachoamini bado anafanya) hawezi hata siku moja kurusha mashambulizi dhidi ya JK (M/kiti wa chama chake). Ni Mrema pekee yake aliweza kuondoka akiwa na umaarufu kumzidi Bosi wake (AHM). Waliobaki wote, Kilango, EL, Mwakyembe mbali ya kuwa ni wanaCCM lakini pia wanamaslahi binafsi yanayweza kuathirika iwapo wataamua kuondoka CCM au kusema kitu cha kuhatarisha ustawi wa M/kiti.

kwa Mfano EL kuwageuka akina JK anakuwa anaweka kwenye risk mafao yake anayoendelea kupata kama PM mstaafu, Mama Kilango hawezi kumuweka rehani mumewe mwenye dhamana kubwa ya kimapato ndani ya chama na WM mstaafu. Wakati huo huo watoto wao wanategemewa kugombea ubunge huko Mtera dingi atakapo stafu. Kama huyu mama Mheshimiw akifyatuka tofauti sana basi nafasi ya vijana wake kupewa uwakilishi na labda hata uwaziri inakuwa mashakani.

Mwakyembe pamoja na ukali wote na mbwembwe za kusoma report ya tume ya Bunge hawezi kutoka Chichiem kwasababu anaamini miradi yake ya Umeme haiwezekani kutekelezeka kama hujakingiwa kifua na wakulu wa nchi wanokubali kupindisha sheria upewe mkopo au grant kutoka benki au mashirika ya pesa.

Kama utakumbuka vizuri kuna kipindi Mwakyembe alikasirika sana, akasema kuna mambo ambayo hawakuyaweka kwenye report yao na kama yangewekwa wazi nchi ingetikisika. Unadhani ni mambo gani hayo? Lazima ujue Mwakyembe sio mjinga kusema ile sentensi, Mwakyembe anajua wahusika wote vizuri sana, inawezekana anajua kuwa kuna mkubwa zaidi ya Mh. EL alihusika kwa njia moja au nyingine.

Pia Makyembe na akina Stella walijua kuwa ni lazima wakinusuru CHAMA na M/kiti wake. Kwani wangesema yote maana yake wengi zaidi wangejiuzuru au serikali kuvunjwa na uchaguzi mkuu uitishwe na Uchaguzi mkuu ukiitishwa katika hali kama ile CHAMA kingepoteza ushindi (assume utakuwa huru na wa haki). Kwa hiyo wakabana baadhi ya mambo. (Kidumu Chama Chetu!)

Ndio maana kipindi cha EL kilipokatishwa hakulalamika, ndio maana maelezo ya RA yalipokataliwa bungeni hakuyatoa kwenye media au kwa public ingawa angeweza kufanya hivyo, kwani hayakuwa mali ya bunge tena.

Kwa Ujumla sitegemei wala sioti EL kutoa tamko litakalo mpinga au kumpaka matope JK. Utatu wao usio mtakatifu yaani JK, EL na RA hauvunjiki kwa moto wa kuni, unahitaji moto wa makaa ya mawe wa kupepewa na mafeni yanayozungushwa na injini za jeti. Na malaika wanaotumika madhabahuni kwa hawa waheshimiwa ni akina Chenge, akina Karamagi, sijui kama Mgonja hayumo humu? Hawa ni wamoja wenye kunia mamoja amini amini nawaambieni. na siku zote wanasema Zidumu Fikra sahihi za m/kiti.

Akina Manyika, akina Hosea wanashindikana kutupwa kwenye tanuru la moto hata ikibidi basi nje kwasababu wanajua mengi mno, kuwatupa nje ni kurisk kuvuja kwa sensitive informations. Mwanyika sio mwanasheria aliyesomea sheria kindergaten, anajua fika nini kiliendelea kwenye sakata la Rich-Mond. Lazima mjue huu sio uzembe wa kawaida kuna more than uzembe ukizingatia issue yenyewe ilivyokuwa hot, mpaka watu wanataka kutengeneza mvua, kwa hiyo lazima alipitia documents zote na alijiridhisha kuwa zile kampuni zilikuwa feki na ni kampuni za kuja kuchoto vijisenti vya watanzania. kwanini hakuchukua hatua, eidha aliogopa kwa kuwa iliwahusu wakubwa au alikuwa mshiriki kama kaka yeke aliyemtangulia bw. VG cent alivyoshiriki deal kibao inc. Meremeta, TANGOLD. Unaona?

Na Bw. Hosea alipopeleleza aligundua kabisa pamoja na kuwa hao TAKURU walikuwa wameota meno manne tu, lakini haimaanishi walikuwa hawana macho. Actually walikuwa wanaona lakini hawawezi kutafuna. Kwa hiyo waliona na wakawastua wahusika kuwa tunaona. Inawezekana walifungwa mdomo wasibweke au waliingizwa kwenye kundi la hao wanufaika. Mbwa akishakuwa analala na binadamu ndani ya nyumba huyo sio mbwa wa ulinzi tena anabadirishwa hata jina anaitwa Petty. Ukitaka kujua wewe jiulize kwanini sasa haleti ma-issue tunayoyalalamikia kila siku kama ya TRL wakati sasa ana meno 24 na amekuwa mkubwa mpaka tunamuita TAKUKURU na sio TAKURU?? (Wizi Mtupu!)

Kuhusu Mh. Mbowe kuachia ngazi ya Uenyekiti, Binafsi sijui sana uwajibikaji wa ndani wa CHADEMA. Kwa mfano CCM wapo makini sana kwenye masuala ya nidhamu ndani ya chama chao, wanademokrasia ya kukubaliana hata kama ni jambo litakalo muua mmoja (km Nnauye) au kumjenga na kumlinda mmoja hata kama ni mchafu (Km Mzee VG Cent).

Kama Madai ya marehemu Chacha Wangwe (RIP) ni ya kweli basi ningependekeza CHADEMA wakubali kubadili safu nzima ya uongozi wa juu (sio lazima kuwaacha nje hata kubadilishana) na kuunda upya kamati zao. Na kukubaliana kuanza upya ujenzi wa demokrasia watakayo hama nayo kwenda kwenye kuongoza nchi watakapo pewa ridhaa ya watanzania. Wakubali kuwa Nchi hii haitakuwa kama ilivyo sasa, baada ya mabadiriko kutakuwa na uwezekano wa chama kutoshnda zaidi ya 50% miaka ijayo, kwa hiyo hali ya demokrasia ya kusikilizana na kuheshimiana itahitajika sana, hasa kusikiliza maoni ya walio wengi. Nchi hii Pindi CCM Itakao ng'olewa madarakani uwezekano wa chama kutawala miongo miwili mfululizo huko mbeleni utakuwa ni mdogo mno. Ni wale tu watakaoweza kuprove kuwa wanaweza kufanya tofauti ndio watakaokuwa na nafasi.

Kama Madai ya Chacha Wangwe hayakuwa ya kweli ningependekeza CHADEMA wamwache Mh. Mbowe katika nafasi ya uenyekiti wa chama na agombee Ubunge kama wengi wanavyomuunga mkono. Mgombea wa nafasi ya Urais (Mwingine) afahamike mara moja iwe kwa njia na vikao halali vya chama (kama sheria inaruhusu) baada ya Mkutano mkuu. Lakini pia tungeweza kuanza kumjua kwa njia zisizo rasimi kama sheria ya uchaguzi hairuhusu kumtangaza mgombea mwaka mmoja kabla.

Hii itamaanisha kuwa sio lazima mwenyekiti wa Chama awe mgombea wa Urais na pia itamsaidia mgombea wa Urais kuacha majukumu ya kuratibu uchaguzi mikononi mwa watu wengine na lisiwe jukumu lake binafsi kama zilivyo kamati za Arusi. Maana mwenyekiti wa Chama atawajibika kuhakikisha Chama Chake kinashinda kwa hiyo kutakuwa na mkakati wa kichama zaidi na sio wa kimgombea.

Lakini kubwa kupita yote ni majibu ya serikali juu ya Tuhuma zote hizi ilizopewa hivi karibu. Ukiusoma vizuri waraka wa kanisa katoliki utakuta zile ni tuhuma za wazi dhidi ya serikali na chama tawala kushindwa kutawala na kuwaendeleza watanzania kiuchumi, kiafya, kielimu na nyanja zingine muhimu na sio watu binafsi inavyotafsiriwa na wengi. Waraka unaonyesha bayana kushindwa kukua kwa demokrasia, unaonyesha bayana ufisadi na ubadihirifu wa mali za umma, kujilimbikizia madaraka na kushinwa kuwajibika kwa watendaji wa ngazi zote za serikali.

Ukisoma Report ya MJJ ya Downs, Report ya MJJ ya meremeta hapo hutakuwa na la kusema ila kujua kuwa nchi hii haina wenyewe ilishapigwa mnada siku nyingi na sisi tunaopiga kelele ni kama mbuzi wanaosubiri kugeuzwa mishikaki.

Kwa hiyo mimi ningependekeza wanaharakati badala ya kusukuma EL kutoa majibu yatakayowasambaratisha (kitu ambacho hakiwezekani) msukumo uwekwe kweye hizi hoja na tuhuma zilizotolewa. Huku hawana majibu. Inahitajika nguvu kubwa zaidi ofcourse, lakini huku ndiko kwenye faida iliyowazi, huku ndiko kuna kazi hata baada ya kupewa dola. Kazi ya kuanzisha upelelezi mpya na huru ma tuhuma zote, kufungua kesi za makosa ya jinai, kuwakamata na kuwafungulia kesi wale wote waliohusika na makosa yanyohusiana na uvunjaji wa haki za binadamu (against humanity au sijui wanziita attrocities) nadhani watahitajika kupelekwa ICC. Pia kurudisha mali zote zilizopolwa na warohi wachache na baadaye kutafuta njia za kuziba mianya yote ya kuibiana kiana aina na pia kujenga jamii watu walio sawa na huru na wanaofaidi matunda ya nchi yao.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Last edited:
Ila Mbowe angepata nafasi ya kuwa Rais,
Naamini tungepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kwa mawazo yangu,.
 
Chadema wangempa uenyekiti Lowassa ili agombee urais akitokea chama cha upinzani nadhani hapa uchaguzi ungekuwa wa moto zaidi..LOL

Akiingia upinzania tu atapandishwa kizimbani kwa utajiri mkubwa aliojilimbikizia tokea akiwa pale AICC mpaka alipomalizia na uwaziri mkuu. Hii ni move ambayo nafikiri hata akilini mwake haipo. The only solution litakuwa kujizuru siasa.
 
- Lowassa ana tatizo moja kubwa sana la binafsi, ni kwamba anamu-under-estimate sana Muungwana, inapokuja kwenye power na popularity, mpaka leo haelewi kwamba mwenziwe anaishi just for those two things,

- Hivi karibuni nilipata bahati ya kuongea na "mtu" mmoja toka wizara ya maji, anawajua wote wawili vizuri sana tena kuliko, ndiye aliyeniambia hata sababu ya conflict ya Mwandosya na Muungwana, yaani ilianzia kwenye demu, akanitajia na jina la demu ambaye nilimfatilia na kuhakikisha mwenyewe kwamba yupo pale maji mpaka leo hii, sitamtaja jina kwa leo,

- Akasema inapokuja kwenye power na popularity, Muungwana ni moto wa kuotea mbali sana, sawa habari ni nzito sana jinsi Lowassa anavyojitayarisha kurudi, na sio siri tena maana ni wazi kabisa na hata viongozi wetu wanaokwenda kujigonga gonga huko nyumbani kwake saa za usiku kwa siri, lakini ni mbio za sakafuni tu!

- Maana soon atagundua kwamba rais wa Tanzania ana nguvu za ajabu sana kisheria, ninamuonea huruma sana Lowassa.

Respect.

FMEs!
 
Ila Mbowe angepata nafasi ya kuwa Rais,
Naamini tungepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kwa mawazo yangu,.

Inategemea watu walio mzunguka, sera za chama zinalenga nini na commitment yake yeye mwenyewe katika kuwatumikia wananchi na kuendeleza nchi yake.

Pia inategemea Baraza lake la Mawaziri ni la watu wa aina gani? Wapo kwa maslahi yao ama kwa maslahi ya wananchi/taifa? Je, ana uwezo wa kuwanyooshea vidole na kuwadhibiti pindi wakishindwa kutekeleza majukumu yao?

Pia inategemeana na composition ya Bunge. Kama ni Bunge mchanganyiko ambapo hakuna chama chenye wabunge zaidi 50% ama 66% [ikitegemeana na voting system inayotumika ili kupitisha hoja], serikali lazima itakuwa makini katika hoja zake na utendaji wake kwa kuwa ikifanya kinyume lazima Bunge liwadhibiti.
 
Ndugu wana JF,

Jambo kubwa na lenye gharama kama la Richmond ni lazima linahusisha viongozi wa ngazi za juu katika serikali. Hapa nina maana kwamba suala la Richmond lilijulikana kwa Raisi, Waziri mkuu, waziri wa madini na nishati mwanasheria mkuu wa serikali, waziri wa fedha na Tanesco. Hili halikuwa suala la kununua na kuuza machungwa pale sokoni kariakoo.

Lowasa amebebeshwa mzigo katika hili suala kimakosa. Mwenye makosa katika hili ni mwenye madaraka na mamlaka ya mwisho, nani mtajaza jedwari wenyewe.

Kama tume ya Dr Mwakyembe ingelifuata haki ingelimwita Lowasa na kumuuliza kwanini aliyatenda yale aliyoyatenda. Lakini Lowasa hakupewa nafasi hata kidogo na pia tumeona hata alipojaribu kujieleza kwenye TV mara tu baada ya kujiuzulu kipindi kilitolewa hewani. Lowasa hana makosa huo ni ukweli usiofichika. Kwanini tume ya Mwakyembe iliacha kuanika kila kitu kama si kufichiana siri?.

Wakati umefika kwa Lowasa kupewa nafasi ya kujieleza ili tukaweza kuelewa nini hasa kinafichwa katika suala zima la Richmond.
 
JK loosing to Lowassa, or facing any noticeable opposition from Lowassa within the party that he chairs will be a clear indication that Tanzania has been under the leadership of a moron.
 
- Lowassa ana tatizo moja kubwa sana la binafsi, ni kwamba anamu-under-estimate sana Muungwana, inapokuja kwenye power na popularity, mpaka leo haelewi kwamba mwenziwe anaishi just for those two things,

- Hivi karibuni nilipata bahati ya kuongea na "mtu" mmoja toka wizara ya maji, anawajua wote wawili vizuri sana tena kuliko, ndiye aliyeniambia hata sababu ya conflict ya Mwandosya na Muungwana, yaani ilianzia kwenye demu, akanitajia na jina la demu ambaye nilimfatilia na kuhakikisha mwenyewe kwamba yupo pale maji mpaka leo hii, sitamtaja jina kwa leo,

- Akasema inapokuja kwenye power na popularity, Muungwana ni moto wa kuotea mbali sana, sawa habari ni nzito sana jinsi Lowassa anavyojitayarisha kurudi, na sio siri tena maana ni wazi kabisa na hata viongozi wetu wanaokwenda kujigonga gonga huko nyumbani kwake saa za usiku kwa siri, lakini ni mbio za sakafuni tu!

- Maana soon atagundua kwamba rais wa Tanzania ana nguvu za ajabu sana kisheria, ninamuonea huruma sana Lowassa.

Respect.

FMEs!

Naam Kikwete ni kiongozi dhaifu sana na hii inatokana na jinsi alivyoingia madarakani mwaka 2005. Na udhaifu huo uko wazi kabisa ndiyo maana Lowassa na mafisadi wengine wanakuwa kiburi cha kuitingisha nchi kama haina mwenyewe.

Angekuwa kiongozi jasiri huo mtikisiko unaondelea ndani ya nchi yetu tangu aingie madarakani wala usingekuwepo. Sasa Lowassa na timu yake wamenusa damu na wanataka kufanya kweli na wakiamua hivyo basi nchi kweli itawaka moto maana kama walivyosema waswahili kwamba wangombanapo mafahari wawili basi ni nyasi ndizo zitakazoumia.
 
Wakati umefika kwa Lowasa kupewa nafasi ya kujieleza ili tukaweza kuelewa nini hasa kinafichwa katika suala zima la Richmond.

Mkuu Kidatu,

Ninakubaliana na hoja zako na kwamba wote uliowataja walikuwa wanafahamu. Kamati ya Mwakyembe ni kweli haikutenda haki kwa kutomhoji EL kwa kuwa ofisi yake ilionekana kwamba iliingilia mchakato wa Richmond.

Kumbuka kwamba Lowassa hakuhukumiwa na Ripoti ya Mwakyembe bali alijihukumu mwenyewe kama alivyoombwa na ripoti kwamba ajipime. Waliohukumiwa ni Msabaha, Karamagi, Mwakapugi, Mrindoko, Mwanyika, na Hoseah. Wote hao waliitwa kujieleza mbele ya kamati na maelezo yao ndiyo yaliyosababisha kamati ika-recommend watimuliwe.

Swali la kujiuliza ni kwamba, kama Lowassa alikuwa msafi kwenye hilo dili ilikuwaje akakubali "kuachia ngazi" kirahisi? Lowassa akiwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni alikuwa na nafasi ya kuomba hata saa nzima ama mawili ili aweze kujitetea yeye na serikali yake.

Baada ya kupangua hoja zote za Kamati Teule angeweza kuiumbua Kamati Teule na hapo angeweza kuachia ngazi akiwa shujaa mwenye heshima zake na hiyo ingemjenga sana kisiasa kuliko kile alichokifanya. Kwa sasa njia ya kurudi kwenye siasa za ngazi za juu ni ngumu sana na JK + watu wake wanaendelea kushindilia misumari ya moto kila kukicha na yeye hana tena platform ya kujitetea, hata akiitisha Press Conference usije ukashangaa hairushwi na TV station yoyote.

Ungekuwa ni wewe ungekubali kubebeshwa mzigo ambao siyo wa kwako na ukubali kuwajibika kwa makosa ambayo siyo ya kwako? Kwa kifupi yawezekana kabisa EL na best wake RA ndiyo walikuwa vinara wa hilo dili na walimshirikisha JK ili kupata baraka zake na akawapa go ahead. Sasa dili limebuma nani wa kulaumiwa? Wahusika wakuu, facilitators ama god father?
 
Wakuu zanguni,
Ama kweli Jamatin kaingia Gorro!
Huyu Lowassa mbona anakusumbueni sana!..Hivi kweli watu bado mnatabia kama za Waganda ambao kila siku wanaendelea kumlilia Idd Amin hata baada ya majanga yote yaliyowahi tokea. Hivi kweli kuna mtu anaweza kufkiria Uganda ingekuwaje leo kama Idd Amin angeendela kuwa rais wa nchi hiyo!

Huyu ndiye Lowassa, mshenzi mmoja alotuingiza hasara kubwa leo hihi amekuwa chaguo la wananchi hata katika mazungumzo!.. Hivi kweli kama Jk asingemwondoa Lowassa katika nafasi ile hii Tanzania ingekalika kweli?.. I mean guys jaribuni kufikiria Lowassa akiwa waziri mkuu na ile scandal nzima ya Richmond sijui imezimwa vipi, hivi kweli hicho chama CCM kingekuwa na sauti kwa wananchi au hata hapa JF...

Wakuu zangu, Lowassa ni mtu wa kusahaulika, Ijipange atakavyo huyu mtu tumfute kabisa ktk kumbukumbu zetu..Huyu ni mtu alopewa kila nguvu ya madaraka na JK. Huyu ndiye alichagua mawaziri karibu wote wa JK, ndiye aliyepanga secretariat ya CCM, ndiye alotufungashia mikataba kibao mikubwa na midogo kwa kutumia nguvu ya wadhifa wake.
Matokeo, kanya anapolia chakula..tena basi akiwa na bahati kajiuzuru hata kabla ya kuhojiwa tuhuma hizo, na ajabu bado ati yupo bungeni ambako anatakiwa kujibu maswali mengi muhimu sana, leo ati anajipanga kurudi ktk uongozi na anapewa sifa zote...Bila shaka wapo wanamtaka na kuomba Mkapa arudi kugombea Urais kwani sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo!
 
Back
Top Bottom