Lowassa to strike back ; Mbowe to quit chairmanship?

This will officialy divide CCM into two camps as the party moves towards general election next year. The recent announcements about possible canditates are just a preludes of the oncoming collision between Lowassa's camp and Kikwete's.

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa amesema hajafikiria wala kutangaza kokote kuwa ana mpango wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010, licha ya kuwepo taarifa kuwa anaweza kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho kuvaana na Rais Jakaya Kikwete.

Lowassa, ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu baada ya kutajwa kwenye kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Richmond Development (LDC), ameshawahi kuwania nafasi hiyo ya juu ya kuongoza nchi mwaka 1995 wakati Benjamin Mkapa alipoibuka kidedea kwenye chama hicho tawala na baadaye kushinda urais.

Mwaka 2005, Lowassa hakuingia kwenye mbio za urais ndani ya CCM kutokana na kile kilichoonekana kuwa ni kumwachia Kikwete, lakini tangu aachiwe uwaziri mkuu amekuwa akichukuliwa kama mtu ambaye anaweza kupambana na rafiki huyo mkubwa kuwania kugombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya CCM.

Hata hivyo, Lowassa, ambaye ameshashika nafasi mbalimbali kwenye serikali za awamu ya pili, tatu na ya nne, alisema hajafikiria wala kumwambia mtu yeyote kwamba ana mpango huo ambao unaweza kusababisha mvutano mkubwa kwenye chama hicho tawala.

Akionekana mchangamfu, waziri huyo mkuu wa zamani alijibu maswali ya Mwananchi bila ya kusita, lakini akiweka tahadhari.

"Sijafikiria wala kutangaza popote jambo hilo unalouliza (la kugombea urais). Niacheni jamani nipumzike," alisema Lowassa alipoulizwa kuhusu habari zinazozidi kusambaa kuwa atapambana na rafiki yake Kikwete mwaka 2010.

CCM imekuwa na utamaduni wa kumteua mshindi wa kiti cha urais wa chama hicho kumalizia kipindi cha pili na hivyo kukaa ikulu kwa miaka kumi, lakini wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kuwa utamaduni huo unaweza kukiukwa mwakani kutokana na misuguano inayoendelea ndani ya chama hicho.

Tayari mbunge wa Maswa, John Magale Shibuda ameshatangaza azma yake ya kupambana na Rais Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

Lakini, Lowassa alisisitiza msimamo wake akisema: "Nakuheshimu sana (alimtaja mwandishi kwa jina) na mimi naomba uheshimu privacy (faragha) yangu, sijafikiria hicho kitu wala kutangaza, nasisitiza."

Lowassa alifafanua kuwa "hata hao unaowasikia wakisema (kuwa anataka kugombea urais 2010), wana vyanzo vyao wenyewe... mimi sijazungumza na mtu yeyote".

Mbunge huyo wa Monduli, ambaye amekuwa akiibuka hadharani kwa nadra tangu aachie madaraka hayo ya mtendaji mkuu wa serikali, alilalamika kuwa amekuwa kimya siku nyingi na ameacha mambo mengi yakiandikwa dhidi yake, lakini akasema: "Sasa, niacheni nipumzike jamani."

CCM imekuwa kwenye jitihada kubwa za kutuliza makundi yanayoonekana kuimarika ndani ya chama hicho, likiwemo kundi ambalo linatuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi na kikundi kinachoonekana kuungwa mkono kinachojinadi kwa jina la makamanda wa vita dhidi ya ufisadi.

Lowassa, ambaye aliachia uwaziri mkuu huku akilalama kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea wakati kamati teule ya Bunge ilipoundwa kuchunguza kashfa ya Richmond na hatimaye kumtaja kwenye ripoti yake, amekuwa ni mhanga wa kundi linalotuhumiwa kwa ufisadi, huku baadhi ya makamanda wa vita hiyo wakitaka afikishwe mahakamani.

Rais Kikwete, ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM, ameelezwa kuwa mtu anayevutwa shati na makundi hayo mawili, hali ambayo inaonekana kutikisa utendaji wake. Lakini katika mazungumzo na wananchi aliyofanya katikati ya wiki iliyopita, Rais Kikwete aliweka bayana msimamo wake kuwa hana urafiki wala undugu katika vita hiyo ya ufisadi na kuvitaka vyombo husika kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi baada ya kuridhika kuwa wanastahili kufika kwenye chombo hicho cha sheria.


- Meanwhile as Chadema is moving towards its general election in a month or so there is a strong indication that Mbowe would finally give up the chairmanship to someone else. However, there are some people who still believe he should lead the party towards general election while others believe that the time has come for a new leadership to lead the party towards victories next year. He is expected to run for a parliamentary seat.

Na kilichotokea baada ya uchaguzi wa Chadema ni nini? Mbowe bado Mwenyekiti.

Nilisema jana kama hatuna mtiririko wa matukio a,b,c... ambao unaweza kututhibitishia pasi shaka juu ya matukio yajayo ni muda tu ndio unaweza kua muamuzi mzuri. vinginevyo tutakua tunadhania (speculate) tu mambo!
 
Last edited:
malaria sugu kama kawaida yako ushaanza na mada zisizokuwa na kicwha wala miguu
 
sheria ya vita ukigundua hila za adui unarudui nyuma kidogo unapanga mashambulizi upya.kwa taarifa yako ms wapinzani wamegundua janja ya ccm,mwaka huu wanajifanya wapo pamoja lakini si kweli.ukitaka kujua ninacho sema angalia nyumba ndogo ya ccm.baada ya karume kumaliza miaka 10 wamechukua fomu wangapi?kwa taarifa yako kikwete akimaliza miaka yake 10 ndio utaona nguvu ya mafisadi,watachukua fomu 100,vita itakuwa kali kiasi kwamba wapinzani watakuwa na kazi kidogo sasa hapo ndio utajua kwa nini kina mbowe na wenzake wamerudi nyuma mwaka huu.najua lipumba atagombea kwasababu lile ni tawi la ccm.2015 kikwete uenyekiti wa ccm hatauweza labda afufuke mwalimu.huu ni ufunuo kwako na wavaa tisheti na kanga wenzako.
 
Italy ni bingwa mtetezi aliyepokonywa utetezi na timu isiyotegemewa ya Slovakia sawa na Kikwete ambaye anatetea kiti chake atakavyopokonywa kiti na mtu asiyetegemewa, ungesema Kikwete anaweza kuwa kama timu ya Italy ingependeza.
 
sheria ya vita ukigundua hila za adui unarudui nyuma kidogo unapanga mashambulizi upya.kwa taarifa yako ms wapinzani wamegundua janja ya ccm,mwaka huu wanajifanya wapo pamoja lakini si kweli.ukitaka kujua ninacho sema angalia nyumba ndogo ya ccm.baada ya karume kumaliza miaka 10 wamechukua fomu wangapi?kwa taarifa yako kikwete akimaliza miaka yake 10 ndio utaona nguvu ya mafisadi,watachukua fomu 100,vita itakuwa kali kiasi kwamba wapinzani watakuwa na kazi kidogo sasa hapo ndio utajua kwa nini kina mbowe na wenzake wamerudi nyuma mwaka huu.najua lipumba atagombea kwasababu lile ni tawi la ccm.2015 kikwete uenyekiti wa ccm hatauweza labda afufuke mwalimu.huu ni ufunuo kwako na wavaa tisheti na kanga wenzako.


hapo kwenye bold subiri wanakuja wenyewe.....
 
Vyama ambavyo havitaweka mgombea Uraisi uwezekanano wa kupata wabunge wengi ni mdogo sana kwa maana hakuna kiongozi wa kuwanadi wenziwe majimboni, kila mmoja atakuwa anapambana kivyake na siyo kama chama. Kama Mbowe angegombea Uraisi japokuwa hatashinda lakini kwa ushawishi wake idadi ya wabunge wa chama chake ingeongezeka sana. Watakaopeta kwenye chama kisicho na mgombea Uraisi ni wale wenye umaarufu binafsi kama Mzee Mapesa anavyopeta mwenyewe UDP.
 
JF....kwa ndoto za alinacha? Unaunganisha suala la Mbowe kugombea ubunge na Lowassa kutaka Urais? Unadhani Lowassa anaweza kwenda chadema? Unadhani nafasi ya kugombea Urais anaachiwa Lowassa....hizi nazo ni ndoto kama ndoto zingine tu..


Uchaguzi utapita na Lowassa hatagombea
 
Nilikuwepo Bungeni wiki mbili za mwisho za bunge la bajeti. Lowasa anatetemekewa huyo! Naambiwa hata kwenye NEC ya CCM pia ana watu wengi sana. Kwa CCM hizi taasisi mbili, yaani, Bunge na NEC zina nguvu na ushawishi mkubwa sana. Ngoja tuone uchaguzi wa mwakani wa CCM kama utaweza kuibadili hali hii. Vinginevyo Lowasa tunaye tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom