Lowassa kupigiwa saluti ni sawa?

MyTanzania

Senior Member
Sep 9, 2008
106
8
Habari wan JF.
Kuna suala moja ambalo ningependa kulileta ndani ya JF ili wadau mlitolee maoni yenu.Jana nilikuwa naangalia habari kutoka channel moja ya hapa nchini Rais alikuwa Monduli katika shughuli ya kijeshi ambapo niliona Viongozi wa JWTZ wakimpigia saluti Mr. Lowassa.
Hivi itifaki inaruhusu mtu aliyeondoka madarakani kwa namna ya Lowassa kupigiwa saluti na wakuu wa jeshi?
Au alipigiwa kama waziri mkuu mstaafu?
Kweli Lowassa ni anastahili hadhi ya uwaziri mkuu mstaafu?
Au alipigiwa kwa hadhi ya ubunge?(If at all wabunge wanastahili saluti)
Maswali ni mengi hayana majibu kwa suala la huyu bwana,naomba wana JF mnielimishe kwa hilo kwani kwa mtazamo wangu naona si sahihi.
 
Sina hakika sana; lakini nakumbuka kuliwahi kuwa na mjadala mzito bungeni wakitaka nao -wabunge wapigiwe saluti!
 
Na mimi nilibahatisha kuona hiyo habari, lakini lililonishangaza ni kuwa wakati habari ilimhusu Rais kutoa kamisheni kwa wahitimu wanajeshi, hakuonekana Rais akipigiwa saluti wala kukagua gwaride, mara picha inaonyeswa Lowasa akisalimiana na makamanda na kupigiwa saluti. Sasa nilitegemea coverage imhusu Rais lakinihaikuwa hivyo. Hata kama wabunge nao wana haki ya kupigiwa saluti lakini nafikiri kulikuwa na shida katika hiyo habari. Unajua mtangazaji naye alicheka mara baada ya hiyo habari.

Nafikiri Rais angeonyeshwa akikagua gwaride na akipigiwa saluti.
 
Sidhani kama ana hadhi ya kupigiwa saluti huyu. Maana hata gwaride la mgambo hastahili. Huu ni uelewa mdogo wa majeshi yetu. Kuna wakati niliwahi pia kuona mfanyabiashara mmoja anpigiwa saluti na askari polisi. Uelewa wa medani za kijeshi ni mdogo sana.
Watakuja kunyofoka mikono kwa saluti ambazo hazistahili kwa mawaziri wastaafu na walioko madarakani.
 
Yumo kwenye kundi kuuubwa la Mawaziri Wakuu wastaafu. Hakufukuzwa kazi!

Kwenye hili kundi la wastaafu hayumo kimafao, maana ni yeye peke yake tu ambaye hapewi full mafao, kupigiwa saluti ninaamini imetokana na ubunge wake period!
 
Mhh vitu vingine vinatakiwa visichukuliwe juu juu! inawezekana hiyo ina maana nyingine labda kama mawaziri wakuu wastaafu/na waliojiuzulu wanastahili kupigiwa saluti.
 
Mkuu FMES,

sifahamu full mafao ya waziri mkuu lakini si vibaya tukayajua kupanua tu wigo wa ufahamu na pengine si vibaya tukafahamu huyu EL kwanini anapata mafao kidogo kuliko mawaziri wastaafu naamini na waliojiuzulu wako kwenye kundi moja humo humo.
 
Wanajeshi wanapoingia ndani ya bunge ni lazima wapige saluti anyways na kutoa kofia, ambayo wanaweza kuirudisha baadaye,

mbunge ni kiongozi wa taifa anayestahili saluti ya kijeshi, vipi wakuu hatukupitia JKT nini?
 
Field Marshal,nadhani askari wanapiga saluti bungeni kwa maana ya kumpigia spika kama kiongozi wa muhimili mmojawapo wa dola,kama ilivyo kwa jaji mkuu na rais,lakini si kwa maana ya mbunge mmoja mmoja.
Ule mjadala wa wabunge kutaka kupigiwa saluti uliisha juujuu bila wao kukubaliwa.Inabidi hawa askari wetu waelimishwe katika hilo maana inafikia mahali wanakiuka itifaki.Saluti kijeshi inamaana kubwa zaidi ya kuinua mkono.
 
sifahamu full mafao ya waziri mkuu lakini si vibaya tukayajua kupanua tu wigo wa ufahamu na pengine si vibaya tukafahamu huyu EL kwanini anapata mafao kidogo kuliko mawaziri wastaafu naamini na waliojiuzulu wako kwenye kundi moja humo humo.

1. Suala la mafao yao tumeliongelea sana hapa, kwa kifupi tu ni kwamba hutunzwa na taifa mpaka watakapoitwa na Mungu, ikiwa ni pamoja na ulinzi, ni only the last two eeks ndio nimegundua kua Lowassa, anapewa ulinzi tu tena ambao ni very conditioned, hii ilikuwa ni badaa ya kuondoka kwake kwenye power, alipofika Airport ya Dar wananchi walianza kumzomea na kumtishia tisshia wakimuita fisadi,

- Kwa vile ilikua arudi kwenye kikao cha bunge, alimpigia simu Spika akidai kua hawezi kurudi bungeni bila kua na ulinzi, ndipo alipopewa walinzi.

2. According to wanaohusika ambao nimewahi kuwauliza sana kuhusu hili suala, ni kwamba kitabu cha serikali cha mafao ya mawaziri wakuu hakina category ya waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu na bunge kwa kashfa za rushwa, ndio maana hata hilo la walinzi liliamuliwa kwa dharura kutokana na hivyo vurugu ya airport ama sivyo niliambiwa asingepewa kabisa.
 
Field Marshal,nadhani askari wanapiga saluti bungeni kwa maana ya kumpigia spika kama kiongozi wa muhimili mmojawapo wa dola,kama ilivyo kwa jaji mkuu na rais,lakini si kwa maana ya mbunge mmoja mmoja.

Mkuu nilipokuwa JKT nilifundishwa kuheshimu kwa saluti viongozi wote wa ngazi ya taifa, kuanzia mbunge na kuendelea,

Unayoyasema siyajui ila ninajua kua mara ya mwisho hivi karibuni nilienda na mbunge mmoja kwenye kambi ya Jeshi Lugalo, nikaona anapigiwa saluti tena mpaka na brigadier wa jeshi,

Kuhusu bungeni, hata Spika akiwa hayupo ni wajibu wa wao kupiga saluti anyways, wanapoingia ndani ya lile jengo!
 
Na mimi nilibahatisha kuona hiyo habari, lakini lililonishangaza ni kuwa wakati habari ilimhusu Rais kutoa kamisheni kwa wahitimu wanajeshi, hakuonekana Rais akipigiwa saluti wala kukagua gwaride, mara picha inaonyeswa Lowasa akisalimiana na makamanda na kupigiwa saluti. Sasa nilitegemea coverage imhusu Rais lakinihaikuwa hivyo. Hata kama wabunge nao wana haki ya kupigiwa saluti lakini nafikiri kulikuwa na shida katika hiyo habari. Unajua mtangazaji naye alicheka mara baada ya hiyo habari.

Nafikiri Rais angeonyeshwa akikagua gwaride na akipigiwa saluti.

Bwana Mavanza kamwe usifikiri hiyo coverage ya EL ilikuwa bahati mbaya, bali ilipamgwa iwe hivyo kuendelea kumsafisha na wahusika wamechukua chao kwa kazi nzuri waliyomfanyia, kumbuka kuwa EL huwa hakati tamaa kama fisi
 
Huyu kwa sasa ni Waziri Mkuu Mstaafu. Hakuna anachonyimwa. Kihadhi yuko sawa na SAS, Msuya, Waryoba, Cigwiyemisi, FTS, Rashid. Na ndiyo maana akapigiwa saluti. Wabunge hawapigiwi SALUTI ingawa waliomba hivyo.
 
Kwenye hili kundi la wastaafu hayumo kimafao, maana ni yeye peke yake tu ambaye hapewi full mafao, kupigiwa saluti ninaamini imetokana na ubunge wake period!

Kwa vile mjadala uliozuka bungeni kuwa Mbunge apigiwe saluti au la haukufikia mwafaka kuwa apigiwe saluti, basi Lowasa, kwa nafasi yake ya Ubunge hastahili kupigiwa saluti. Isitoshe yeye si Waziri Mkuu Mstaafu kama walivyo akina Sumaye, Warioba, Msuya n.k. Yeye alijiuzulu kutokana na kujihusisha na ufisadi wa Richmond; kwa kweli tunaweza kusema kuwa alilazimishwa kujiuzulu na, hatutakuwa tumekosea kusema kuwa "alifukuzwa" au 'aliwajibishwa?' Laiti kama angeendelea kuwa WM huenda kashfa ya jengo la UVCCM na ile aliyokuwa anataka kuanzisha ya 'mvua za kutengeneza' zingemfikisha pabaya. Kamwe hastahili saluti ya wapiganaji wetu.
 
Bwana Mavanza kamwe usifikiri hiyo coverage ya EL ilikuwa bahati mbaya, bali ilipamgwa iwe hivyo kuendelea kumsafisha na wahusika wamechukua chao kwa kazi nzuri waliyomfanyia, kumbuka kuwa EL huwa hakati tamaa kama fisi

Kwa uelewa wangu mdogo wa habari, hii ya EL kupigiwa saluti ndiyo habari yenyewe. Kama ya MTU kumng'ata MBWA!
 
Kati ya Watanzania milioni 40 hivi CCM haina mbadala ya aina ya kina Lowasssa? (Ama kweli wamefilisika CHADEMA na CUF amkeni mtupe mbadala haraka kabla ya mwisho wa mwaka huu).

KWELI mzee ana uswahiba na pengine alimpa ahadi jamaa kwamba baada yake yeye ndiye atakayekuwa rais. Lakini yaliyokwishatokea lazima iwe funzo kwa watu wanaotaka kutawala nchi kwa udugu na urafiki badala ya kutawala kwa kutumia watu wenye uwezo kufanya kazi zilizopo. Inatisha jamani nchi hii ni ya 226 kimaendeleo duniani yaani baada yetu ni malawi, sierra leone, gaza strip na somalia! Aibu sana hii. Lakini ndio uongozi wa aina hii ambao haujui kutafuta bali kutumia tu. Na watatumia mpaka wanaifilisi Hazina kama Wamarekani walivyofanya huko kwao. Nyie ngojeni muone tu!

LAANA ya Babu sio mchezo. hata afanye nini mpaka mamilioni yake yaende na mkondo wa mito baharini........ aache ndoto haendi popote na sisi aliyokwishatufanyia yametukinaisha. Hatumtaki. Labda kama jamiirorums ni yanawe au wafadhiliwa wake ndio mnampigia kampeni ndogo ndogo?

Lowassa kupigiwa saluti ni sawa?
 
1. Suala la mafao yao tumeliongelea sana hapa, kwa kifupi tu ni kwamba hutunzwa na taifa mpaka watakapoitwa na Mungu, ikiwa ni pamoja na ulinzi, ni only the last two eeks ndio nimegundua kua Lowassa, anapewa ulinzi tu tena ambao ni very conditioned, hii ilikuwa ni badaa ya kuondoka kwake kwenye power, alipofika Airport ya Dar wananchi walianza kumzomea na kumtishia tisshia wakimuita fisadi,

- Kwa vile ilikua arudi kwenye kikao cha bunge, alimpigia simu Spika akidai kua hawezi kurudi bungeni bila kua na ulinzi, ndipo alipopewa walinzi.

2. According to wanaohusika ambao nimewahi kuwauliza sana kuhusu hili suala, ni kwamba kitabu cha serikali cha mafao ya mawaziri wakuu hakina category ya waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu na bunge kwa kashfa za rushwa, ndio maana hata hilo la walinzi liliamuliwa kwa dharura kutokana na hivyo vurugu ya airport ama sivyo niliambiwa asingepewa kabisa.

Lowassa is always an interesting topic at JF, na mimi ni mmojawapo iliyonivutia leo. Tunakuamiania Field Marshall kwa facts, lakini ulichoandika hapo juu is PURE NONSENSE, simply bullshit.

Hivi unafikiri huo Lowassa anaishi kwenye kisiwa chake mwenyewe, na wetanzania hatumuoni kila siku, jamani kwa wenzetu mlio mbali na nchi, muulize tu kidogo ku-verify.

1. Lowassa anao ulinzi tangu siku amejiuzulu pale bungeni, na wale walinzi hata hawajabadilika, ni wale wale aliokuwa kwenye uwaziri mkuu. Eti anampigia simu spika kuomba ulinzi???.Sijui unataka tufikirie spika amekuwa nani nchi hii.

2. Nenda kwenye official ceremonies zote, siku zote amekuwa addressed kama Waziri Mkuu Mstaafu, labda utuambie kingine.

Cha msingi jamani, tuongee with facts, tusionee watu kwaajili ya hisia zetu, lakini naendelea kukuheshimu Mhe Field Marshall, siku njema.
 
Na EL hakulazimishwa kujiuzulu jamani! Tusipindishe historia ya NCHI yetu tena kwa tukio ambalo halina hata mwaka mmoja. HANSARD zipo, magazeti yapo,....
 
Back
Top Bottom