Lowassa kupigiwa saluti ni sawa?

Sina hakika sana; lakini nakumbuka kuliwahi kuwa na mjadala mzito bungeni wakitaka nao -wabunge wapigiwe saluti!

Wakati wanapeleka muswada wa kuitwa waheshimiwa niliwahi kusema kuwa kuna siku watataka wapigiwe saluti na ikatimia siku kukawa na kitimtim bungeni (tambo za Simpasa), pia nawaambia hawataishia hapo watataka wakistaafu waitwe waheshimiwa wabunge wastaafu, au pia watakwenda zaid ya hapo....
Kuhusu Lowasa kupigiwa saluti nadhani pia tutaiona hata siku akipandishwa mahakamani ambapo atapigiwa saluti na askari jela.....

enewei ni vijimambo tu hivi
 
1. Suala la mafao yao tumeliongelea sana hapa, kwa kifupi tu ni kwamba hutunzwa na taifa mpaka watakapoitwa na Mungu, ikiwa ni pamoja na ulinzi, ni only the last two eeks ndio nimegundua kua Lowassa, anapewa ulinzi tu tena ambao ni very conditioned, hii ilikuwa ni badaa ya kuondoka kwake kwenye power, alipofika Airport ya Dar wananchi walianza kumzomea na kumtishia tisshia wakimuita fisadi,

- Kwa vile ilikua arudi kwenye kikao cha bunge, alimpigia simu Spika akidai kua hawezi kurudi bungeni bila kua na ulinzi, ndipo alipopewa walinzi.

Mkuu FMES, heshima mbele!

Mara baada ya kutangaza kujiuzulu Lowassa alirudi Dar akitokea Dodoma siku ya Jumamosi ya tarehe 9 Feb 2008 mchana. Alipofika Airport Dar alilakiwa na familia, ndugu, jamaa na marafiki, ambapo waliondoka pamoja kwenda nyumbani kwake Masaki. Katika kuondoka Airport, msafara wao uliongozwa na polisi wakitumia gari moja la Land Rover na pikipiki yenye king'ora iliyokuwa mbele!

Ulinzi huo wa polisi pamoja na king'ora ulikuwepo pale Airport hata kabla ya Lowassa kutua hapo uwanjani! So suala la kuomba ulinzi kwa Spika hilo halikuwepo! Lowassa hakupata kuzomewa na wananchi pale Airport ya Dar! Alipokelewa like a "hero" na hao jamaa zake. Na msafara wake ulipiga king'ora barabarani like a "Prime Minister"!

2. According to wanaohusika ambao nimewahi kuwauliza sana kuhusu hili suala, ni kwamba kitabu cha serikali cha mafao ya mawaziri wakuu hakina category ya waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu na bunge kwa kashfa za rushwa, ndio maana hata hilo la walinzi liliamuliwa kwa dharura kutokana na hivyo vurugu ya airport ama sivyo niliambiwa asingepewa kabisa.

Lowassa anapata mafao yake kama kawaida, nenda kaulize tena Lowassa hakulazimishwa kujiuzulu!
 
tatizo waandishi na editors wa habari ndo wanaochagua ipi iwe habari. sasa wao waliona wavute watu zaidi kwa kumwonyesha lowassa akipigiwa saluti kutokana na mashibu ya nyuma.
ila infact nawapongeza kwani lowasa kama mbunge wa eneo lile alistahili coverage nzuri. nafikiri hata watu wa monduli walivutiwa kumwona mbunge wao akipewa shavu na media kwani huenda anajitahidi kutimiza ahadi zake. infwakti anawatemeblea mara kwa mara zaidi ya kwenda marekani.
nawasilishaaaa.
 
.... lakini lililonishangaza ni kuwa wakati habari ilimhusu Rais kutoa kamisheni kwa wahitimu wanajeshi, hakuonekana Rais akipigiwa saluti wala kukagua gwaride, mara picha inaonyeswa Lowasa akisalimiana na makamanda na kupigiwa saluti. Sasa nilitegemea coverage imhusu Rais lakinihaikuwa hivyo...... nafikiri kulikuwa na shida katika hiyo habari. Unajua mtangazaji naye alicheka mara baada ya hiyo habari.

Nafikiri Rais angeonyeshwa akikagua gwaride na akipigiwa saluti.

Mhhh!(Spin Docs),haya bwana picha za mkuu wa shughuli hizo hapo... naelekea kufikiri hao waandishi wanalao jambo...
 

Attachments

  • CIDF.jpg
    CIDF.jpg
    54 KB · Views: 100
  • 8D6U0175.JPG
    8D6U0175.JPG
    34.8 KB · Views: 95
Kitendo cha askari kutumia kiganja cha mkono kumpigia saluti mtuhumiwa wa ufisadi badala ya kutumia kiganja hicho kumchapa kibao cha uhakika huyo mtuhumiwa wa ufisadi mimi sikielewi.

Labda wanajeshi wa vyombo vyote vya usalama watuambie ni lini watawapigia saluti wananchi na kusikiliza kilio chao na kuacha kuwapigia saluti watuhumiwa wa ufisadi na mlezi wa watuhumiwa wa ufisadi.
 
Aliyejiuzulu kwa kashfa inakuwaje anakuwa kama aliyestaafu kwa heshima?

Kujiuzuru kwa EL kulitokana na Watendaji wa chini yake kuvurunda na yeye kutoliona hilo mapema na kulichukulia hatua (ndivyo tulivyoelezwa). Kama enzi zile Mzee Mwinyi. Ni kweli kiasi gani labda tuombe akina Mwakyembe waseme yale ambayo hawakuyasema!
 
Kujiuzuru kwa EL kulitokana na Watendaji wa chini yake kuvurunda na yeye kutoliona hilo mapema na kulichukulia hatua (ndivyo tulivyoelezwa). Kama enzi zile Mzee Mwinyi. Ni kweli kiasi gani labda tuombe akina Mwakyembe waseme yale ambayo hawakuyasema!

Ndio maana nimesema alijiuzulu kwa kashfa. Tunaweza kuipamba na kuimeremetesha tuwezavyo ukweli utabakia hivyo ni kuwa Waziri Mkuu alijiuzulu kutokana na yeye mwenyewe (ofisi yake) kuhusishwa na kashfa iliyolisababishia Taifa hasara kubwa. Kwamba walioko chini yake "kuvurunda na yeye kutoliona mapema na kulichukulia hatua" hapo ndipo ilipo kashfa yenyewe. Lowassa hakustaafu. Kustaafu na kujiuzulu siyo kitu kimoja isipokuwa kwenye mawazo ya watawala wa Tanzania.
 
Ukishajiuzuru kwa mtindo huo, kwa neno moja unaitwa MSTAAFU. Anaweza kurudi kama ZUMA au MWINYI au kwa staili atakayoona inafaa kwa wakati huo.
 
Ukishajiuzuru kwa mtindo huo, kwa neno moja unaitwa MSTAAFU. Anaweza kurudi kama ZUMA au MWINYI au kwa staili atakayoona inafaa kwa wakati huo.

Umesema kweli kwani hivyo ndivyo anaitwa... lakini ukweli ni kuwa aliyejiuzulu siyo mstaafu. Ni sawasawa na kusema kuwa mwiba siyo mwiba kwa vile tu uko karibu na waridi na badala yake kusema kuwa ni kasehemu katawi kalikochongoka ambako kanatumika kama ulinzi wa asili wa mti...
 
Ukishindwa uchaguzi je? Au ukiondolewa kwa mapenzi ya aliyekuteua kama ilivyotokea kwa Rashid wakati ule?
 
Kuna multiple combination of factors hapa ambazo zimekuwa ignored hadi sasa.
Kwanza mmesahau kuwa Taifa limegawanyika kwasasa....Ni mpasuko mkubwa na ndio maana kuna wanaodai hata baadhi ya maeneo nchini wabunge wa huko wanaheshimiwa kuliko mkuu wa nchi.
Habari hii ina mielekeo kadhaa...Lowassa ofcourse anaji position..At the same time kama JK alikuwa huko ni sawa na kuonyeshwa kuwa hiyo ni territory ya mwingine...Kwamba huko amwachie Lowassa.
Si mnaona ulinzi hata wa waziri mkuu utadhani ni ukanda wa vita huko ziarani ama hata ni sehemu inayotawaliwa na waasi?
Kwa hiyo Lowassa kapigiwa saluti huko Munduli...JK naye atapigiwa saluti huko kibaha nk.
Mbeya ni ngumu,Tarime na Kilimanjaro ndio usiseme...Sasa kama si sheria za nchi kuiweka dola mikononi mwa watawala...Basi ni kama hakuna serikali moja...Na hivyo mimi nashangazwa na nyie mnaoshangaa kuwa Lowassa kapewa kipaumbele na hishma zaidi ya JK...Si afadhali hakukuwa na mawe?
 
Kuna multiple combination of factors hapa ambazo zimekuwa ignored hadi sasa.
Kwanza mmesahau kuwa Taifa limegawanyika kwasasa....Ni mpasuko mkubwa na ndio maana kuna wanaodai hata baadhi ya maeneo nchini wabunge wa huko wanaheshimiwa kuliko mkuu wa nchi.
Habari hii ina mielekeo kadhaa...Lowassa ofcourse anaji position..At the same time kama JK alikuwa huko ni sawa na kuonyeshwa kuwa hiyo ni territory ya mwingine...Kwamba huko amwachie Lowassa.
Si mnaona ulinzi hata wa waziri mkuu utadhani ni ukanda wa vita huko ziarani ama hata ni sehemu inayotawaliwa na waasi?
Kwa hiyo Lowassa kapigiwa saluti huko Munduli...JK naye atapigiwa saluti huko kibaha nk.
Mbeya ni ngumu,Tarime na Kilimanjaro ndio usiseme...Sasa kama si sheria za nchi kuiweka dola mikononi mwa watawala...Basi ni kama hakuna serikali moja...Na hivyo mimi nashangazwa na nyie mnaoshangaa kuwa Lowassa kapewa kipaumbele na hishma zaidi ya JK...Si afadhali hakukuwa na mawe?

Mawe wanabeba walevi na watu wadogo, yeye mkubwa mawe ya nini? Labda abebe kitu kingine!!
 
Mawe wanabeba walevi na watu wadogo, yeye mkubwa mawe ya nini? Labda abebe kitu kingine!!

Huko Mbeya kuna kina Mwandosya...Hatukuona saluti kwasababu tukio lilikuwa tofauti..Badala yake ni mawe.
Kila jimbo limechoshwa na utawala wa serikali kuu na inatakiwa waje wazalendo wa kuyaunganisha tena majimbo haya la sivyo itakuwa ngumu kuwa na sirkali madhubuti....Hii ni very serious mamdogo.
Sikumaanisha kuwa Lowassa ampige mawe JK...Ila hata saluti aliyopewa yeye ni si jiwe kubwa tu? Vipi kuhusu wale wazee na walimu? Nao walevi tu?
Mzigo ni mzito kwa JK kuitawala nchi yote na ndio maana unaona wale waliochaguliwa huko majimboni mwao ndio wanaopewa respect zaidi yake kwasababu Taifa halitawaliki tena na ufisadi umemshinda nguvu mkuu wa nchi.
Hujasikia hata Mh Rais mwenye anawaishwa ikulu kabla ya giza kuingia?
Hii ni kama akiwa nje ya Dar....So unaweza kuona kuwa hatawali nchi nzima as of now.
 
Lowassa is always an interesting topic at JF, na mimi ni mmojawapo iliyonivutia leo. Tunakuamiania Field Marshall kwa facts, lakini ulichoandika hapo juu is PURE NONSENSE, simply bullshit.
Hivi unafikiri huo Lowassa anaishi kwenye kisiwa chake mwenyewe, na wetanzania hatumuoni kila siku, jamani kwa wenzetu mlio mbali na nchi, muulize tu kidogo ku-verify.

Mkuu ahsante sana kwa ujumbe wako, ni majuzi tu alikuwa anahaha nchi moja majuu akiomba asaidiwe kupata chumba cha hotel ama sivyo angelala nje, infact hata gari la kumchukua airport kama sio msaada wa jamaa yangu angeishia kuchukua tax, sijawahi kuona mawaziri wakuu waliostaafu, wakihangaika huko majuu namna hii, kama uko karibu naye naomba mkumbushe kua hizo chupa za brandy anazokunywa nzima nzima zitamuuwa karibuni sana, inaonekana yeye na mkewe bado hawajaikubali hali ya kuwa nje ya power,

ilikuwa aibu kwa mama kuhangaika mitaani na texi ndugu yangu tema mate kidogo maana yanayomkuta mkulu sasa ni aibu tupu! wakuu wenziwe husafiri na walinzi wawili sio mmoja kama yeye! Halafu hufanyiwa kila kitu na ubalozi kupitia kwa wasaidizi wao wakuu, lakini sio mstaafu mwenyewe kutafuta hotel au gari la mizigo, that is strange, halafu sio mbaya ukituwekea ulipomuona akiwa na full mafao eti ni wapi huko?


1. Lowassa anao ulinzi tangu siku amejiuzulu pale bungeni, na wale walinzi hata hawajabadilika, ni wale wale aliokuwa kwenye uwaziri mkuu. Eti anampigia simu spika kuomba ulinzi???.Sijui unataka tufikirie spika amekuwa nani nchi hii.

Baada ya rais kutangaza kuwa amevunja cabinet, wakuu wote alipotoka ndani ya kikao walikuta magari yao yote yamebadilishwa namba za ngao na kuwa STD, including Lowassa mwenyewe, na walinzi hawakuwepo mpaka alipofika Dar na kukutwa na janga, maneno yako yangekua kweli asingepata joto alipokwenda kanisani bila walinzi, huo ulikuwa ni msaada wa Spika kumnusuru na aibu na wananchi, lakini hata walinzi hakutakiwa kuwa nao, uliyemuona labda ni Serukamba, Lowassa aligoma kuhudhuria bunge mpaka apewe ulinzi hayo nimeambiwa na mbunge mmoja aliyehudhuria kikako cha dharura kusikiliza hiyo hoja, na minutes zote za kikako nimeziona,

Unataka kujua power ya Spika? wewe una cheo gani serikalini mkuu ambaye hujui power ya Spika wetu. Unafikiri mafisadi kwa nini wanalala macho kumtoa Sitta kama hana power yoyote ile inayowakwaza na ufisadi wao? Yaani kumbe hujui kuwa bila Spika mpaka leo Lowassa bado angekua kwenye power?


2. Nenda kwenye official ceremonies zote, siku zote amekuwa addressed kama Waziri Mkuu Mstaafu, labda utuambie kingine.

Waziri mkuu mstaafu haombi kutafutiwa chumba cha hotel kwa kupiga simu mwenyewe, na haombi gari hayo yote hufanywa na serikali, mimi sikujua kuwa haya yote mpaka majuzi niliyaona mwenyewe, akihangaika hata gari la mizigo, labda uwaambie wananchi hapa wengine lakini kwenye hili nimeliona mwenyewe mkulu akihangaika, mwanzoni niliamini kama unavyoamini lakini mpaka majuzi nilipoona kwa macho yangu I wish ningeweza kutoa details zaidi za aibu niliyoina huyu mkulu akiipitia majuzi!

Cha msingi jamani, tuongee with facts, tusionee watu kwaajili ya hisia zetu, lakini naendelea kukuheshimu Mhe Field Marshall, siku njema.

Facts sio wewe tu unayezi-hold, hapana na sio kwamba wewe ukiamua kupinga anything basi unazo facts, hayo ni mawazo mgando yaliyomkuta huyu mkulu majuzi nimeyaona mwenyewe kwa macho, na kuthibitisha kwamba hapewi mafao yote, nimeuona akihangaika kutafuta chumba cha hotel, akihangaika kutafuta gari mpaka msamaria mwema alipojitokeza kumsaidia, infact ilimshangaza hata huyu msamaria mwema kuona huyu mkulu akihangaika hivi, kwa maneno yake mwenyewe akiomba msaada, aliulizwa kulikoni ndipo alipojibu mwenyewe kuwa hapewi all mafao, on that unaweza kusema anything you want I am not moving kwa sababu mwanzoni niliamini kama wewe lakini in the end nimejithibitishia kuwa hapewi, na ikanisukuma mpaka kuandika wkenye gazeti moja hivi karibuni kuhusu hii finding, ambapo pia niliwauliza wahusika wengi sana kutokan na facts nilizoziona.

Kwa kumaliza naomba kukushukuru sana kwamba sasa umekubali kujadili ishus kwa ustaarabu na ndicho nilichokuwa ninakitaka siku zote, mimi ni mwanasiasa wa kweli ndugu yangu kila ninachofanya huwa ninakifanya na goal maalum na hapa hatimaye my goal imefanikiwa, haikuwa rahisi in the process nimepitia yote lakini kwenye siasa tunahukumiwa kwa results, na wako ni mfano wakutosha kuwa ninaziweza siasa.

Naomba tuendelee hivi hivi na ustaarabu wa hoja, ahsante sana mkuu. na heshima yangu kwako ndio imeaanza sasa maana haikuwepo kabisa huko nyuma! Halafu ni wajibu wa kila mfanyakazi wa serikali na chama kumuita mstaafu hebu tumia common sense kidogo iwapo wasipomuita hivyo watamuitaje? Waziri mkuu aliyejiuzulu? au waziri mkuu wa richimond? mambo mengine na wewe tumia busara kuliko chuki na hasira, ni lazima aitwe waziri mkuu mstaafu,

saluti nimeiona ikipigiwa mbunge hospitali ya jeshi Lugalo, hakuna askari wa jeshi Tanzania aneyeweza kupita bia kupiga saluti kwa mbunge hayo mawazo ni pure nonsense, mawili, eihter askari atabana mikono au kusimama kupiga saluti nimeuona Gahu former chief of staff kwenye harusi ya malecela Dodoma, akipigia saluti wabunge ndani ya ukumbi wa harusi, sasa huyu ni mkuu wa utawala, je wale wa chini itakuwaje?

hasira chuki na ukweli huwa haviwezi kuwepo kwenye ukurasa mmoja, mbunge ni mtu mkubwa sana kuliko unavyofikiri na jeshi ni la wananchi, in the future saa ingine tumia busara zaidi kuliko hoja za nguvu, ingawa hongera sana wka progress.

FMES wazee wa Sauti ya Umeme!
 
Mkuu FMES, heshima mbele!

Mara baada ya kutangaza kujiuzulu Lowassa alirudi Dar akitokea Dodoma siku ya Jumamosi ya tarehe 9 Feb 2008 mchana. Alipofika Airport Dar alilakiwa na familia, ndugu, jamaa na marafiki, ambapo waliondoka pamoja kwenda nyumbani kwake Masaki. Katika kuondoka Airport, msafara wao uliongozwa na polisi wakitumia gari moja la Land Rover na pikipiki yenye king'ora iliyokuwa mbele!

Ulinzi huo wa polisi pamoja na king'ora ulikuwepo pale Airport hata kabla ya Lowassa kutua hapo uwanjani! So suala la kuomba ulinzi kwa Spika hilo halikuwepo! Lowassa hakupata kuzomewa na wananchi pale Airport ya Dar! Alipokelewa like a "hero" na hao jamaa zake. Na msafara wake ulipiga king'ora barabarani like a "Prime Minister"!

Lowassa anapata mafao yake kama kawaida, nenda kaulize tena Lowassa hakulazimishwa kujiuzulu!

Vipi mkuu hakukuwa na media walioona haya? Hapo mwanzoni hata mimi niliamini hayo unayosema, lakini ni majuzi tu ndio nikabadilika mawazo kwa niliyoyaona kwa macho yangu, mkuu akiaibika tena sana mpaka kufikia mahali hata mizigo imemshinda namna ya kuifikisha airport.

Kwa maneno yake mwenyewe hapewi mafao yote, hata Mwalimu alipomkabidhi Mwinyi urais pale uwanja wa taifa, alirudi nyumbani bila king'ora mpaka baadaye ndio wakarekebisha, infact walinzi wote walimkimbilia Mwinyi na kumuacha Mwalimu ameduwaa, sasa leo eti unasema Lowassa alipokelewa kwa ving'ora? na matayarisho lakini media ya Tanzania haikuwepo? Duh!
 
Very interesting...

Naona Muungwana anacheka na nyani kwenye shamba la mahindi.

Halafu wakitoka hapo, kina Mkuchika wanadai ooh kubenea mchonganishi, Salva nae
ooh hakuna mwanaccm mwingine anaetaka urais 2010...

Kama wabunge hawapigiwi saluti, hii ni gesture ya kuwa taken seriously.

Labda niulize, Maalim Seif , mwingine aliefukuzwa nae anapigiwa saluti kama Nahodha?
 
Very interesting...

Naona Muungwana anacheka na nyani kwenye shamba la mahindi.

Halafu wakitoka hapo, kina Mkuchika wanadai ooh kubenea mchonganishi, Salva nae
ooh hakuna mwanaccm mwingine anaetaka urais 2010...

Kwa watu kama mimi ambao Tanzania ni taifa letu, ni lazima tujadili na kufuatilia ishus kama hizi, kucheka kwa Muungwana kama ni kweli kupo hakutuziii kujadili maana asiposikia maoni yetu then atasikia in hard way kwa mawe ya huko huko Mbeya, au?
 
Mkuu nilipokuwa JKT nilifundishwa kuheshimu kwa saluti viongozi wote wa ngazi ya taifa, kuanzia mbunge na kuendelea,

Unayoyasema siyajui ila ninajua kua mara ya mwisho hivi karibuni nilienda na mbunge mmoja kwenye kambi ya Jeshi Lugalo, nikaona anapigiwa saluti tena mpaka na brigadier wa jeshi,

Kuhusu bungeni, hata Spika akiwa hayupo ni wajibu wa wao kupiga saluti anyways, wanapoingia ndani ya lile jengo!

mkuu FMES heshima mbele.
Yote unayoongea inawezekana ni kweli kabisa ila hili la salute ndo kuna kosa kidogo.Kama uliona Mwanajeshi anampigia salute mbunge inawezekana mbunge huyo alikwahi kuwa mwanajeshi na kma uliona kwenye harusi mwanajeshi anamsalute sijui nani inawezekana kati ya waliokuwa hapo harusini alikuwepo mwanajeshi wa cheo karibu na wewe hukuweza kumwona.

Mwanajeshi kupiga salute kwenye bunge siyo kuwa anampigia mbunge bali huwa ni ku-salute proceedings ile ambayo ipo na picha ya rais mle ndani.Siyo Bungeni tuu,hata mahakamani hata mahakama ya mwanzo mwanajeshi anapiga salute kabla ya kukaa mara tu aingiapo.Hii haimaanishi kuwa mahakimu wote hadi wa mahakama ya mwanzo hupigiwa salute na wanajeshi bali wanajeshi huwa wanasalute proceedings ile iliyopo huku pia kukiwa na picha ya rais.

Mwisho kabisa tukumbuke kuwa wanajeshi hupigia salute maiti zote mara zipitapo no matter what.Hata kama maiti hiyo ilikuwa ya jambazi.Kwa hiyo mimi Lowassa kupigiwa salute means nothing.
habari ndo hiyo
 
Back
Top Bottom