Lowassa kujitoa CCM?

kweli hiyo ni ndoto ya mchana hawezi kuhama chama maana hata yeye anajua kitachomtokea..... lakini tetesi hizi kama niza kweli basi achukue experience kwa Mrema kwanza kabla hajaendelea
 
Kama kweli songas wanakomba posho ya 200m kwa siku na kiwira watakomba 300m kwa siku wakati mabwawa yetu yanataka kupasuka kwa kuzidiwa na maji basi napata hisia ya kuwa lowasa kaonewa, kwani isingechunguzwa RDC tu bali mchakato mzima wa mikataba ya tanesco.

wabunge walijaribu kuzuia hoja hiyo isiibuliwe na zitto na kupata umaarufu zaidi kwa kuitoa wao kwanza ili zitto atakapoongea ionekane hana jipya. Mama kilango hakuteleza ulimi kusema sio kila hoja imsubiri zitto! ndilo lililokuwa akilini mwake

Tukumbuke kuwa hata Dowans hawako Iran wala Kuwait zaidi ya kuonekana wakimiliki mgahawa mdogo saizi ya mamalishe huko uk lakini hakuna anayehoji hilo! wala mwakyembe hakwenda iran kuwatafuta.

Tusisahau kuwa kunawahandisi wa tanesco waliomwambia waziri mkuu kuwa ingelichukua miaka 15 kwa mvua za elinino kulijaza bwawa la mtera na kidatu jambo ambalo hata mtoto wa chekechea asingekubaliana nalo.

Pia nawasiwasi wabunge wetu walitaka kuzima rasimu ya ubiafsishaji wa huduma ya umeme, IPS wao wangefanya kazi kibiashara na kupeleka umeme palipo na umuhimu wa kweli. Sote tunajua kuwa gia kubwa wabunge wetu kwa wananchi ni kuwaletea wananchi umeme maji na barabara bila kujali tija iliyopo maeneo husika. hivyo walijua wakimng'oa karamagi na Lowasa hoja hiyo itakufa.

Nakumbuka 1987 niliwahi kusubiri kuunganishiwa simu kwa masaa nane bila mafanikio! leo hii napata huduma hii bure siku za wikiend! natumaini sikumoja nitapata umeme kama ninavyopata huduma ya simu! leo tigo kesho zantel!
 
Mimi namshauri atoke Chama ili kuzidi kujisafisha ,hayo yatakayofuata baadae ni kuikubali siasa.
Kuna tofauti kubwa itapatikana ukilinganisha na akina Tambwe ,huyu mtu ni kuachana na CCM mbona akina Mrema mpaka leo bado wamo ,na ndivyo inavyotakiwa awachane na CCM kwani sasa Tanzania kuna vyama vingi tu vya siasa,Na kwa vile anaona hakutendewa haki kama ni kweli basi awachane na CCM ,tatizo kama ni kweli alikuwa mshiriki wa dili la richmond basi bora aozee huko huko.
 
Kuna tetesi zimeenea kwamba Mh E Lowassa asipo pewa channel ya madaraka tena huenda akajitoa CCM na kujizatiti kwa ajili ya 2010 au 2015...leteni habari zaidi

wadau ,kabla sija wa member hapa ,nilikuwa napenda sana kufuatilia mijadala humu jf,tafadhali tuna omba wadau mtu asi come up na stori ya kutunga tuu,kwani kuna watu wapo nje huku hivyo kwa namna moja au nyingine munatutoa off trck(poteza).mjue mkiacha magazeti mitandaoni ni jf tunategemea kwani kuna muda tunakosa imani na radio na magazeti ya tz kwa sababu ya kuwa sio wawazi kutokana na sababu za kuogopa chombo kufungiwa,ni hayo tu wajumbe,hizi ni kali za wajumbe wenu
 
Si dhani kama anaweza kujitoa chichiemu(CCM).Kwani anataka asafishwe ndani ya chama ili atimize azma yake ya kuwa Rais baada ya Muungwana(JK).
Na hii unaweza kuipata kwakuangalia maneno yake ya hivi karibuni ambapo anajifananisha na Mzee Ruksa.
Nawasilisha.
 
Hana ujanja wa kukimbia ccm watabanana hapohapo mpaka kieleweke,unafikiri hajui yaliyowakuta waliotangulia.sisi tumjadili kwa ufisadi wake ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake na wale wote walihusika ktk kufanya maisha yetu yazidikuwa magumu.

..labda ameguke na wenzake. si wako kadhaa,au?
 
inabidi aanishe chama chake chamafisadi .. kitapata kura nyingi kwa wananchi wetu hasa wa vijijini ambao huongeka kirahisi
 
Back
Top Bottom