Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Edward Ngoyai Lowassa (fisadi pacha) amerudi kwa kishindo kutoka ughaibuni alikoenda kwa ajili ya matibabu ya macho. Amewajulisha adui zake wa kisiasa, nafikiri ndani ya CCM, kuwa yuko tayari kwa "mapambano". Alikunja ngumi kama ishara ya kuonesha kuwa yuko "fit and fine" (buheri wa afya); na akatamba kuwa atayathibitisha hayo huko Arumeru Mashariki.
Nape na wenzake wamekuwa wakipiga kelele kwa kumtaja Lowassa kuwa ni kati ya "wanachama wachafu" wanaopaswa kuacha nafasi za uongozi ndani ya CCM, kama njia mojawapo ya kukisafisha chama; au kama wenyewe wanavyosema, "kujivua gamba". Rostam Aziz, aliyekuwa Mbunge wa Igunga, yeye katangulia kujivua nafasi zake zote za uongozi katika chama ili "aachane na siasa uchwara". Pacha mwingine Andrew Chenge, maarufu kama Mzee wa Vijisenti, yuko kimya anasubiri yeyote amguse ili alianzishe; yaani wamwage ugali, naye amwage mboga. Lowassa yeye amewazidi wote kwa ujasiri. Ana roho ya paka. Ameonesha wazi kuwa anataka kuwa "Rais ajaye". CCM kimeonesha kumgwaya. CCM kiko kimya.
Lowassa aliporudi jana, ametamka wazi wazi kuwa anayemzushia kuwa afya yake ina mushkeli basi akaone kuwa yuko "fit and fine" huko Arumeru Mashariki. Ninahisi alimaanisha kwenda kumpigia debe mkwewe, ambaye amempigania kwa "remote ya rushwa" mpaka akapata nafasi ya kugombea kwa tiketi ya CCM.
Ni wazi kuwa CCM, hii ya sasa, haitakuwa na uwezo wa kumzuia mtu iliyemtangaza mchafu kupanda jukwaani kumnadi mgombea wao. Nape na "walokole" wenzie watafyata mkia. Nina imani kuwa Jumamosi hii, watatuma ujumbe mzito wa kwenda kumpa pole "mzee" na safari na kumtaka hali, na ZAIDI, kumuomba asaidie kutoa chochote ili wakabiliane na "chama ambacho William Sarakikya hakipendi". Watamsifu; watamwambia uko "fit and fine"; mzee unaonekana "una afya kuliko wakati mwingine wowote". Watampamba; naye atawapa chochote. Mwisho kabla ya kuaga watamwomba wiki ijayo akawasidie jukwaani. Watamwambia "mzee tumechunguza na kuona unakubalika". Atacheka kidogo, na atawajibu "sawa".
Lowassa wiki ijayo atapanda jukwaani. Atamnadi mkwewe. Nape na wenzie watakula matapishi. Watakaa kimya. Ila moyoni watajisemea "MWENYE NGUVU MPISHE".
Mie nikimwona Lowassa jukwaani wiki ijayo nitakumbuka maneno ya kwenye kitabu cha KULI; "YANA MWISHO".