Waziri mkuu wa zamani aliejiuzulu kwa kashfa ya Richmond na mbunge wa Monduli mh Edward Ngoyai Lowassa,ndie mwanasiasa ambae amekuwa akitajwa sana na kuandikwa na vyombo vya habari kwa takriban wiki mbili sasa!
Hii ni baada ya tar 1/1/2014 akiwa Jimboni kwake Monduli ktk sherehe za mwaka mpya,akizungumza na wageni waalikwa alisema kuwa safari yake imeanza baada ya mateso ya muda mrefu!
Tumesikia baadhi ya viongozi wa Ccm wakilumbana kuhusu Kauli za mh Lowassa,,hata wengine wamediriki kusema wazi wazi kuwa Lowassa anavuruga Chama na hata wakaenda mbali zaidi na kudai kuwa hana sifa ya kuwa kiongozi,,wala kuwa Amiri jeshi mkuu na Mwenyekiti wa Ccm!
Sijui na wala Siamini km kuna siku mh Lowassa ameitisha Waandishi wa habari na kutangaza nia yake ya kugombea Urais!
Ninajua mh Lowassa anajiandaa na anayo nia ya kuwa mgombea kwa Ccm na siku moja awe Amirijeshi mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama!
Lakini kiukweli itakua vigumu sana kwa mh Lowassa kuwa Rais wa Tanzania,hii inatokana na kwamba hakubaliki na Watanzania walio wengi nje na ndani ya Ccm!
Lakini pamoja na haya bado baadhi ya Wana Ccm wanachanganyikiwa na jitihada hizi za Lowassa hata kuwafanya wawe wanatoa matamko juu yake.
Nachojiuliza ikiwa Lowassa hajatangaza kuwa atagombea Urais ni kwanini basi viongozi wengi wa Ccm wanahaha?
Hajatangaza hali iko hivi je siku akitangaza itakuaje?
Mwenye jibu anisaidie!