Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,442
- 4,153
Kwa mtazamo wangu, Tanzania tumefika mahali tunahitaji kuupindua mfumo mzima wa kifisadi, kuondosha u-mungu mtu na kusimika rasmi misingi ya utawala wa sheria - iwe wazi kuwa hata rais anapaswa kuheshimu sheria na asiwe na uhuru wa kutumia vyombo vya dola kwa maslahi binafsi. Huo ndio mfumo wa ovyo uliojengwa na CCM.
HIVYO, PA KUANZIA ni kuiondoa CCM madarakani ili kwanza kuvunja dhana ya chama dola - kwamba chama kilichopo madarakani kinatumia nyenzo za dola (NEC, TISS, Polisi, BOT, n.k.) kujihakikishia ushindi katika chaguzi. Kumhakikishia mwanasiasa au chama cha siasa ushindi wa kudumu hata iweje ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa.