Lowassa anasafishwa!

Kama nilivyosema kule KLH kwamba $152,000.00 au Tshs152,000,000.00 zinazo lipwa kila siku kwaajili ya umeme hewa ni mali ya SISIEMU kwa ajili ya Uchaguzi wa 2010.
Najua fika hawawezi kuingia BOT na kuunda Kagoda Agricultural nyingine,SISIEMU wanachota fedha za kampeni ya 2010 kupitia mradi hewa wa Richmond ambao sasa umechukuliwan na Dowan.

Lowassa anageuzwa shujaa mbele ya macho yetu ili njama zao za kutuibia mchana kweupe ziendelee.

Kwa nini apewe muda kwenye TV ya TAifa kujieleza?
Kwanini haendi channnel 10 akapigwe maswali ya unya unya?

Najua Lowassa ni msanii by Profession ndiyo maana sasa ameamua kucheza mchezo wa kuigiza kwenye TV ya Taifa lakini akisaidiwa na MH Jakaya mrisho Kikwete.

KWa mtaji huu nadhani sasa SISIEMU wanatubashia hadharani jambo ambalo hatukubali kabisa.Wanatuibia mamilion ya $$$ kila siku halafu wanatumia vyombo vya kitaifa kama TV na magazeti kujisafisha?

Yule mwimbaji wa Kenya aliimba Pesa ni maua lakini INAUA.

Naona MH Kikwete umejiweka maua ya Richmond ili Ujiue. Hongera.

Baada ya Lowassa kuongea utumbo wake kwenye hiyo TVT naamini kwa dhati kabisa kwamba heshima ya TV hiyo itashuka chini ya kiwango kikubwa.

Mzee Mwanakijiji nakumbuka ulielezea kuhusu Agenda 21.

Bila shaka utekelezaji wa makubaliano haramu ndani ya Agennda 21 ndiyo umekwisha anza kwa Lowassa kupewa wasaa wa kujieleza katika TV ya Taifa na mamilioni kumwagwa kwenye vyombo vya habari kama TV na magazeti.

Hivi ninyi SISIEMU hamjiulizi kwamba kwa nini Joseph Mobuto Seseko Kuku Wa Zabanga akiwa hai aliikimbia Congo na katika ufu wake mabaki ya mwili wake yamezikwa Morocco pamoja na ukweli kwamba alikuwa na fedha kuliko fedha walizo kuwa nazo wacongo wote kwa pamoja, kwa sababu pato lote la kila siku la serikali ya Congo lilikua likiingia kwenye personal accont yake????

Mobuto na Mifedha yake yuko wapi???
Wanae wako wapi??
Wajomba zake wako wapi??
Rafiki zake wako wapi??

Nani yuko nyuma ya Agenda 21?

Hisia zangu zinanielezea wazi kwamba Persident Jakaya Mrisho Kikwete yumo ndani ya Timu hiyo ya Agenda 21.
Agenda 21 ni lazima kiwe kikundi cha kiharamia kinacho taka kutajirika kwa hila zozote zile ili kianzishe utawala wa kimatabaka unaongozwa na wezi wakubwa wa mkoa wa Arusha kama akina Nyari na viongozi lukuki ndani ya idara za serikali na mashirika ya umma wanaiba na kuuza ardhi ya Tanzania kwa wageni ili kukidhi hamu yao ya Kishetani.

Agenda 21 ni Mafia au Yakuza ya Tanzania na mimi nikiwa Mtanzania na mmoja wa wanachama wa JF sitakubali mtandao huo wa Kiharamia Uchukue nchi. Zaidi siko tayari kuongozwa na maharamia.

Nadhani kuna wakati itabidi tuchukue hatua moja mbele zaidi ya hapa na kuwaonyesha Mahabithi hawa kwamba fedha zao ni bure mbele ya mikakati ya wananchi.

Kuna siku tutawanyonga hadi mfe kwa udenda utokao midomoni mwenu kwa tamaa ya utajiri na mamlaka.

Who are in Agenda 21???

Huu ni wakati wa kujenga mkakati wa nguvu kabisa wa kuiondoa SISIEMU madarakani once and for all. SISIEMU wamechoka kukalia kiti nadhani matako yao yanawauma kwa unene utokanao na kufakamia rushwa na hela za wizi.

Lowassa anarudi kwenye safu na kuoshwa kwa sabuni ya mshindi!

Hii itafanya kambi nzima ya SISIEMU ijipakaze na kunuka.
Waheshimiwa wa SISIEMU,Dhambi hii ya pili ya kuruhusu Haramia na Mwizi mkubwa Lowassa aitwe shujaa itawagaharimu uhai wenu kidogo mliobakiwa nao kisiasa.

Kwa tabia yenu ya dharau mtaziba masikio yenu na kuendelea na ratiba kana kwamba kila kitu ni shwari lakini muda ukifika kila mtu atachukua junia lake la dhambi na kuelekea ahela.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA
 
Na Askofu KKKT haoni aibu..Naskia EL huwa anatoa fungu kubwa sana kanisani!

Huyu naye ni fisadi wa sadaka.

Maaskofu wengi ni wahalifu wakubwa na ndiyo maana siku zote ni watu wakujipendekeza kwenye system yenye michuzi hata kama system yenyewe inauka kwa uoza.

Hawawezi iga mfano wa akina TUTU askofu mstaafu wa kanisa Anglikan huko SA?

Mwenzao alikuwa akiandamana sambamba na wapigania Uhuru.
Hawa akina Laizer wanaandama na kupanua midomo yao wakisikia harufu ya Mshiko tu.

Maaskofu wa Dizaini ya Yuda Iskariote.

Kama akina sisi tutaenda kuzimu kwa dhambi zetu hizi na kuungua kwa moto,basi wao akina Laizer wakwenda huko kuzimu na kuchomwa kwa moto wa Lazer na Plasma.
 
Lowassa ni too senior kwenda kuwa balozi...
At most may be kwasababu kuna mwanamtandao UN (Dr. Migiro), kwa mtazamo wangu finyu, Lowassa anaweza pewa kazi ya heshima kusimamia mambo fulani serbia huko etc lakini Lowassa mwenyewe akitaka. Otherwise ni kubanana banana humu humu tu Tanzania.

Kumetolewa highlights kidogo za mahojiano kwenye taarifa ya habari ya jioni leo on TVT kwahiyo kitachorushwa on TVT 8PM GMT ni kitu already recorded... Mahojiano yalifanyikiwa monduli na kuudhuriwa na maelfu ya wananchi wa maeneo ya huko.

Eeeh bwana kwa taarifa yako hata kama Migiro yuko UN hawezi kuwa na influence yoyote ya kumuunganisha Lowassa ilo haliwezekani kabisa...kwani kuna watu kibao wenye uzoefu sana ambao Lowassa kwao ni mtoto...sana sana ana uzoefu wa hapo Tanzania lakini anga za kimataifa hamna kitu....wala usitarajie kitu kama hicho.
 
Lowasa hewani kwenye replay TVT
Aanza kwa kuangusha gunia la lawama kwa Mwanasheria Mkuu,Katibu Mkuu Hazina ,Madini kwamba wao wana husika na hasa mwanasheria kwenye mikataba yote yeye hana lolote bali kubariki.

Asema alimwita waziri Nishati na kumuuliza juu ya uhalali wa kampuni ya Richmonduli maana alisikia maneno mitaani .Lakini waziri alisema inafaa na hakutaka kubadili mwelekeo .

Yupo on sasa anajisafisha .
 
Namuangalia TVT,

Yaani ukimsikiliza ndio utona kuwa yale madai ya kwamba angehojiwa ma Kamati ya Mwakyembe yanazidi kuwa muhimu.Sasa amepata msemo na anaweza kuspin anavyotaka.
 
Lowasa anasema alijua kwamba RDC ni matapeli .Anasema kajiondoa Ukuu kwa ajil ya wadogo .Anasema wanasheria wote walimweleza kwamba mkataba na RDC was perfect.Luhanjo na wengine waliitwa akawaambia lakini wakasema kisheria hatuwezi kuvunja mkataba .Fuatilia .
 
Hii Ni aibu sana kwa kweli. Sawa, na afanye hivyo kwa kuwa fedha za wizi zinamruhusu. Hat hivyo, tumekuwa wajanja na njia yake ya urais au hata ubunge imeshachafuka sana. Hii itakuwa vita kali dhidi ya waandishi au vyombo vya habari vitakavyoonekana kumwegemea sana. Vyombo huru kama JF vitatumiuka ku counter-attack na kuchambua maudhui mabovu ya vyombo hivyo...

It is so painful to see how our trusted countrymen are selling their freedom--and the society's freedom so cheaply to mabeberu...
 
Alikuwa wapi kuwabana wahusika wakati yeye ndo Boss wa shughuli za kila siku ndani ya serikali?

Kibaya zaidi kwa maneno yake alitetea kwamba Richmonduli ni safi ila watu hasa JF tuna Roho za mbegu ya mkorosho.
Hii hii hii!

It is too late to apologize! It is toooooo laaaate!!!!.
 
Ahsante kwa kutuleta hizi habari....kwa karibu wiki mbili sasa alikuwa anafundishwa aseme nini...nina uhakika kama angeitwa kwenye kamati wakati asingesema anayoyasema leo. Na kinachotokea sasa yeye ni kujiosha unaona sasa anaaanza kuwarushia lawama hata viongozi na mafisadi wenzake...hamna lolote hata akijitetea tangu lini mwizi akakubali kwamba yeye ni mwizi...na wezi mara nyingi uwa wana lugha zangu kuliko wale ambao hata hawajawahi kuiba karatasi moja...
 
Kweli Africa we have long way to go , kama mwamdishi anamuuliza Mheshimiwa maswali ya kitoto kiasi kile bila follow up question tumekwisha.
 
Namuangalia TVT,

Yaani ukimsikiliza ndio utona kuwa yale madai ya kwamba angehojiwa ma Kamati ya Mwakyembe yanazidi kuwa muhimu.Sasa amepata msemo na anaweza kuspin anavyotaka.

Pundit....hata kama angeitwa naamimi anayosema leo ingekuwa tofauti na wakati huo...jaribu kukumbuka aliwahi kutetea na sasa anafanya maigizo ya kujisafisha...ni ubabaishaji tu kwa ili hatuwezi kudanganywa..

Unajua hata kama mtu akifumaniwa live naweza kukana kabisa kwamba si yeye....kwa hiyo aojiwe na kamati asiojiwe sisi hayatusaidii sasa hivi. Tunataka pesa zetu za EPA, Richmond zirudi...

Kwa nini akuyasema bungeni mpaka asubiri leo....lazima kuna chochote na jamaa wanachofanya ni kutaka kujisafisha kwa wananchi...anayetaka kukubali akubali...lakini mimi simo

aende zake akuchunge mbuzi bwana
 
Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu alisema, hapo ndipo walipoamua kuachana na TANESCO na kuamua kutumia timu ya wataalamu wa Serikali wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika.

Huyu jamaa mbona alijitetea sana kwenye kamati ya mwakyembe kwamba hajui chochote katika hili sakata. Ama kweli, ukistaajabu ya musa utaona ya firauni.
 
Picha (attached) ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akishuka kwenye ndege ya kampuni ya Coastal Air mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndge wa Arusha. Swali je pesa hizi na mandalizi kule Monduli anastahili na ni pesa zetu za kodi sisi walalahoi an ndio kutoka mfuko wa kifisadi??
 

Attachments

  • Lowassa.jpg
    Lowassa.jpg
    31.1 KB · Views: 60
Kweli Africa we have long way to go , kama mwamdishi anamuuliza Mheshimiwa maswali ya kitoto kiasi kile bila follow up question tumekwisha.

Ni matatizo na tuna hali mbaya sana..., sijui nani amemwambia aende kwenye TV kujieleza ni mambo ya kishenzi badala ya kuweka mambo ya maana wanatulete fisadi hawana hata aibu...waende zao na sisi hatukubali...huu muda wa matangazo wanaoharibu bure basi wangetuletea maendeleo ya uchaguzi kiteto.

Mimi siwezi kuwaelewa kabisa...anajitetea nini...kama angekuwa safi basi angeyafanya hayo yote miezi kumi iliyopita si sasa....hatuwezi kudanganywa kama watoto.

eeh bwana wahandishi walio wengi si wataalamu wa hiyo fani ni kudandia tu...hivyo usishangae nchi ilishaharibikiwa ....
 
Anaonekana kukata sana weight hadi mkanda kafungia tumboni.Sikuwahi kumuona kavaa namna hii katika maisha yake ya Uwaziri Mkuu ,lakini atajua kwamba Cheo ni dhamana.Gharama tena mmm sijui labda ndiyo faida za kuwa waziri Mkuu na Serikali inalipa ?

Mimi namuuliza ile deal ya mvua toka kwa wale Rushwa wenzake Thailand limeishia wapi ? Maana alilikazania naamimi alishapa kata cha juu .Jamani wale watetezi wake njoni na majibu .Mvua yetu aliyo tuahidi iko wapi ? Katika hand over notice kamwambia Pinda lini itafika ?
 
mwacheni aendelee kuspin/kujisafisha or whatever you can call it maana ndio demokrasi,lakini at the end of the day ni sisi wananchi kuamua kumpa yes or no maana hawezi kuwa mbunge au raisi bila kura zetu,ila haya mambo ya kuharibu kodi zetu kwa vitu kama TVT ni wizi wa mchana maana hilo TVT linakula tuu kodi zetu huku tukijua halina faida yeyote kwa nchi zaidi ya kuwa propaganda machine ya walioko madarakani,na vitu kama TVT ndio mwanzo wa ukandamizaji wa demokrasi na matumizi mabaya ya pesa zetu.
 
Picha (attached) ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akishuka kwenye ndege ya kampuni ya Coastal Air mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndge wa Arusha. Swali je pesa hizi na mandalizi kule Monduli anastahili na ni pesa zetu za kodi sisi walalahoi an ndio kutoka mfuko wa kifisadi??

Pesa za wananchi hzio ndugu...sasa analakiwa na umati ili iweje...nashangaa sana. Kwa kweli ni kufilikisa kimawazo na inaonyesha jinsi watu wetu walivyo na uwezo mdogo wa kufikiria...
 
Nimemsikiliza! kwanza katupotezea Muda sana, maana Jazba aliokuwa nayo Bungeni haijaisha anaonekana bado anayo, Pili TVT ni chombo cha uma sasa sijui mweshimiwa huyu kalipia???? au kaongea tu kupitia mlango wa nyuma katika mtindo wa kuendeleza tena ufisadi??? Inaonekana hana washauri wazuri Kama huwa anasoma sehemu hii basi namuomba atulie. Vinginevyo hasira tulionayo juu ya sh.milioni 152 kwa siku zinazoendelea kupotea hadi leo maana mkataba bado haujavunjwa, Hasira yetu ni kubwa haina mfano. Kwa hiyo atulie asisemeseme hovyo!

Kwanza kama ni rushwa hii ni kubwa inatosha asiendelee kutuchefua.
 
Anaonekana kukata sana weight hadi mkanda kafungia tumboni.Sikuwahi kumuona kavaa namna hii katika maisha yake ya Uwaziri Mkuu ,lakini atajua kwamba Cheo ni dhamana.Gharama tena mmm sijui labda ndiyo faida za kuwa waziri Mkuu na Serikali inalipa ?

Mimi namuuliza ile deal ya mvua toka kwa wale Rushwa wenzake Thailand limeishia wapi ? Maana alilikazania naamimi alishapa kata cha juu .Jamani wale watetezi wake njoni na majibu .Mvua yetu aliyo tuahidi iko wapi ? Katika hand over notice kamwambia Pinda lini itafika ?

Mvua....atawapelekea wamasai wenzake wakati anachunga nao...hakuna cha mvua wala manyunyu hapo....
 
Hizi pesa za kukodi ndege Dar- Ar amepata wapi? Au ni sehemu ya kikibacks from 1990s akiwa Maafa na AICC hadi PM?
 
Back
Top Bottom