Lowassa ana bahati sana, sababu Magufuli hafai

Mkuu,
Wewe ulitaka awambie nini? Wewe ni mmoja wa wale wamezoea siasa za kilaghai!

Ulitaka awaambie atawapa usafiri wa bure?

Fikra zako zinaonyesha Ukweli siku hizi umekuwa ni sumu ya kisiasa nchini.

Tanzania ya sasa inahitaji wanasiasa wanaosema ukweli hata kama unauma kifikra.

ila lile halikuwa jibu kwa wananchi, watu wa kigamboni na nje ya kigamboni liliwauma sana, kiongozi hutakiwi kutoa jibu lile, anaenda omba kura kwani kampeni tayari,
 
Nimeipenda japo si mawazo yako.

Hayo ya Meli kukamatwa kuna watendaji kubao hata wa UKAWA wameshiriki. Hayo yote pia. Mimi binafsi naona tukisema Mtu kama Magufuli siyo safi basi TZ yote si safi. Samaki kuna Polisi hawakulinda meli, Wanasheria walichelewesha na bado wanafanya hayo kwa kesi zetu kibao. UUzaji wa nyumba ulifanyika kipindi kile na si yeye peke yake aliuza kwa bei ya kutupwa. Wapo hao akina Eddo pia na wengi tu wa UKAWA. Maamuzi magumu kwa MAgufuli anamzidi EDDO mbali sana!
Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wanaopenda kusifiwa katika utendaji wao Wa Kazi.Bwana huyo amekuwa Na maamuzi ya peke yake na anachotaka yeye ndicho hicho.kwa mfano suala la kukamata meli ya Samaki , baadhi ya watendaji walimshauri lakini kama kawaida yake alikataa Na matokeo yake serikali inadaiwa fidia Na wahusika.Kuna suala la kubomoa petrol station Mwanza, kuna suala la ugawanaji Na uuzaji Wa Nyumba za serikali hakika huu in ufisadi mkuu.Mambo yote hayo ni kero kubwa kwa wanachi.Kama haitoshi kuna suala la ununuzi Wa boti kuukuu kwa kiasi kikubwa cha fedha za umma kiasi cha bilioni 8 boti ambayo haifanyi safari .Zote hizo in kodi za watanzania lakini zinateketea kirahisi.
 
kwani BVR zimetengenzwa wapi, na kama zimetengenezwa china basi tusubiri maumivu tu si unajua wachina na ile familia ya bagamoyo damu damu na hawatamuangusha
 
Mbona mtoa mada unakuwa kama haujala wiki nzima? na hayo mawazo yako ndo yameifikisha tanzania hapa, hatuhitaji mawazo hayo tena, tunahitaji kiongozi asimamie sheria na bila wogo wowote ule, hatuhitaji maamuzi ya kisiasa katika utendaji, bila Dr.Makufuri kusimamia sheria ungekuwa barabara wapi hapa Tz?

Wakati mwingine tutumie hekima zaidi na si mambo ya kukaririshwa, leo hii Dar, imejengeka ovyo ni kwa sababu ya kupuuza wataalamu wetu na kufanya maamuzi ya kisiasa, bado watu mna mawazo ya zamani wakati hii ni karne 21, ukienda mataifa mengine miji yao imejengeka vizuri ni kwa sababu wanaheshimu mwawazo ya wataalamu na si wanasiasa. kwa hali hiyo usimuhukumu Dr.Makufuri kwa upuuzi huo ambao hauna nafasi kwa wapenda maendeleo.
 
Tumpigie kura nani sasa?

pIGIENI kura hawa hapa wakomboe nchi na kukuza uchumi wa MTEI...................................
[h=3]UKOO WA CHADEMA BUNGENI WAANIKWA: GAZETI LA UHURU[/h]






BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.


"Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa Mwenyekiti wa Chama ana ndugu watatu, Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme? Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, Samahani Mh. Ndesamburo"

Akichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011,
Assumpter Mshama (Nkenge –CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.

"Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi," alihoji.

Aliongeza: "Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.

"CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje."

Kwa upande wake, Livingstone Lusinde
(Mtera-CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.

Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.

"Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme," alisema.

Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo kwani wa kuzuia fujo wapo.

"Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu," alisema.

Lusinde aliohoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.

Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.

CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.

Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.

Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.

Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo na pia aliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.

John Lwanji (Manyoni Magharibi-CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno abrakadebra.

Benardetha Mushashu (Viti Maalumu-CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.

"Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kama kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona," alisema.

Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.

"Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana," alisema.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.

Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi wangeshindwa kishujaa.














 
Yani huyu kaitia hasara serikali kuliko hata punje moja ya Lowassa, Meli imekuwa mazalia ya POPO hapo bandarini, Barabara za TANROADS wanapaka rangi nyeusi kwenye kokoto zilizogandamana eti lami, Barabara zote zilizojengwa na kampuni ya SKOL, Canop za wilaya ya kinondoni mfano, barabara ya kuelekea mbweni imebanduliwa na kuwekwa mbovu tena, barabara ya Kuanzia mianzini kwenda mbweni Hospital ni takataka kabisa, sijui anapunguza 10% au ikiwa hawa jamaa wanaomba tenda alafu wanalikologa kwa kushindwa kazi na kuleta usumbufu. Shangaa awafungiwi.
 
Katika kulinganisha uwezo wa Magufuri imeonekana kwamba Kumpambanisha magufuri na Lowassa , Ni sawa na kufananisha Mti wa Muhanzi na Mbuyu.

Kitu ambacho Huwezi kufananisha na kupambanisha, Magufuri kwa Lowassa Tunamuonea Bure, CCM walichemka, Saizi ya Magufuri ni Mzee Lembeli.

Lembeli anamtosha kabisa Magufuri, na Anaweza magufuri akagalagazwa na Mzee Lembele vilevile Kama Wote Wangegombea Urais Mwaka huu. Lakini Kwa Lowassa Anamuacha Magufuri kwa Mbali mno mno.

CCM wanalijua hilo ,Lakini hawataki kusema ukweli. Hata Magufuri mwenyewe anajua hilo.
. lembeli.jpg magufuli-piga-tumba.jpg

Picha Msafala wa mzee Lembeli Kahama, Picha ya pili Magufuri anapiga Lumba
 
Umenena vema sana! tatizo ccm hawakujua kama lowassa ana plan B, walidhani wameshammaliza! Lembeli ndo size ya magufuli! Lowassa jina lake lenyewe ni taasisi kubwa sana! Magufuli anaonewa sana!
 
Hata Magufuli mwenyewe anajua kuwa hawezi kupambana na Lowasa. Na wala hakutegemea kabisa kupitishwa na Chama chake kuwa mgombea. Alikuwa sahihi maana kweli hatapita.
 
Magufuli alichaguliwa kwa bahati mbaya..naona kama ana mawenge mawenge sana..anachosema ni sitawaangusha
 
Thubutu!!!Lembeli mla rushwa mkubwa Kwa wafugaji ili waendelee kuweka mifugo yao ndani ya hifadhi za wanyamapori Leo akafananishwe na MZEE wa Chato.Lembeli hafai kabisaaa
 
Magufuli alichaguliwa kwa bahati mbaya..naona kama ana mawenge mawenge sana..anachosema ni sitawaangusha
Na yule anayesema, "LABDA NISEME, LABDA NISEME, LABDA NISEME"? Kisha maneno hayaendelei!!
 
Back
Top Bottom