Lowassa ana bahati sana, sababu Magufuli hafai

Magufuli siyo mgombea mbaya,tena ni mzuri labda kuliko wote kuwahi kutokea CCM ukitoa baba wa taifa,lakini kaja wakati mbaya sana kwenye historia ya nchi yetu ,kapatikana kipindi ambacho CDM,wameungana na vyama vingine na kuwa na nguvu kubwa kuwahi kutokea,kaja kipindi ambacho mgombea wa upinzani ana nguvu kuliko wakati wowote ule,kaja kipindi ambacho watu wamehamasika kujiandikisha kuliko wakati wowote ule,kaja kipindi ambacho CCM inachukiwa kuliko kipindi chochote kile,kaja kipindi ambacho wananchi wanahitaji mabadiliko kuliko kipindi chochote kile,kaja kipindi ambacho matokeo yatatangazwa mapema kuliko kipindi chochote kile(nadhani kabla ya misa ya kwanza).
Njia pekee ya Magufuli kuwa kwenye serikali ijayo ni kurudisha kadi ya CCM na kuchukua kadi ya CDM,naye awe kwenye mizunguko yote ya kampeni ya Mzee wetu mpendwa kama wenzake walivyofanya.
Ni bora iwe haraka kabla mlango wa safina hujafungwa.
 
CCM kindakindaki wanasema hawatishiki mafuriko kuna magoli ya mikono,maarifa,uzoefu na mbinu za ushindi.
 
hilo uliloongea analitamani sana, tena ata mke wake kamshauri sana ila tatizo nafsi yake inamsuta, hawezi kumwangusha kikwete,mkapa etc. kwa sababu akifanya ivyo wana-mwondoa. ikumbukwe kuwa sasa hivi team Membe+familia ya kikwete wapo nyuma ya magufuli sasa ivi, ndio nguzo pekee ya kutegemea wakishach ia madaraka.
 
Kweli kabisa bora angeenda kugombea ubunge akihangaika kushindana na edo atapotea kwenye siasa....
 
wabongo bwana , hivi wenyeakili zetu tunaanzaanzaje kuchagua CCM B wakati CCM A ipo ?????mfyuuuu mtajitia moyo sanaaa na huyo mutu yenu .....Big up Lipumba / Dr Slaaa heshima zenu wakuu ! Nyie ndio mnenirudisha CCM A :ranger:

umeona eeeh.
 
wananchi kata lowasa fisadi wa kutupwa hatumpiii

Wadau ni wazi kwamba Magufuli amekata tamaa ya kuingia ikulu kutokana na upinzani mkali ulioko mbele yake. Pia anajutia nafasi aliopewa kugombea urais mwaka mgumu kuliko miaka yote ya uchaguzi iliyopita. Anahofu chama kufia mikononi mwake. Amekata tamaa kwa kweli, anaomba mungu kikombe hiki kimuepuke lakini haiwezekani. Amekonda kwa hizi wiki 2 tu, sijui mpaka october atakuwa na hali gani. Anahisi bado JK ana kisasi nae mpaka kumteua kugombea uraisi huku akijua CCM haiwezi kupita. Ni kama vile JK amemtwisha gunia la lawama. Lile nyomi la lowasa la jana limemnyima usingizi kabisa. Na mimi nasema na akate tu tamaa kwa sababu hakuna namna nyingine.
 
Hatumpi kura zetu huyo lowasa wao,na mumpigie huko kaskazini Kanda ya ziwa wameshashtuka mnawasifia halafu mkishinda mnaanza kuwapondea.
 
Huyo magufuri afie mbali watanzania tumechoka na sera ya jembe na nyundo .Kwanza ajibu swari kwanini Tz nimaskini ,mbali na hayo jembe na nyundo imewafikisha Watanzania wapi?na hasa mkulima.
 
wabongo bwana , hivi wenyeakili zetu tunaanzaanzaje kuchagua CCM B wakati CCM A ipo ?????mfyuuuu mtajitia moyo sanaaa na huyo mutu yenu .....Big up Lipumba / Dr Slaaa heshima zenu wakuu ! Nyie ndio mnenirudisha CCM A :ranger:
Rudi tu maana huku wanabaki wanaojielewa tu
 
Magufuli hana sera imebaki ni "CCM oyeee" na "Sitawaangusha" basi hajui hamwangushi mtu ila anaanguka mwenyewe.
 
Back
Top Bottom