Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 912
- 4,249
Tukiwa Monduli hapa majira ya usiku tunakula nyama kama ishara yakumuenzi ndugu yetu na kaka yetu Lowasa. Wazee wa kimila kutoka ukanda huu wa kaskazini wanapiga soga na kubadilishana mawazo huku wakifukua historia ya viongozi mbalimbali waliofaha kuwa viongozi wakubwa ila wakatengwa na historia.
Katika historia ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania anatajwa Mzee Sarakikya, huyu aliweza kupokea jeshi kutoka kwa wakoloni na kuweka misingi iliyopo sasa ya jeshi. Pamoja na umaskini wetu, wazee wanamtaja kama kiongozi aliyeweza kutumia akili na rasiliamali kidogo kujenga majengo ya jeshi na kuanzisha taassisi ikiwemo Lugalo.
Ni kiongozi aliyeweza kusimama imara na kumshauri mwalimu nyerere ipasavyo na kwa kutambua uwezo wake na nguvu yake ya ushawishi aliondoka Jeshini akiwa bado anahitajika. Mzee huyu anazaliwa katika wilaya ya Arumeru si mbali kutoka anapozaliwa Lowasa.
Wazee hawa wanaleta pia masikioni mwangu jina la mwanamapinduzi aliyekataa ukoloni Kaskazini aitwaye Japhet Kirilo. Wanavyosema wazee msibani ni kwamba, huyo Japhet Kirilo aliondoka Meru na kwenda umoja wa Mataifa kuomba Uhuru wa wa wameru.
Akiwa katika mchakato huo ndipo akafika mwalimu kwenye ofisi zilezile na kuomba Uhuru wa Tanganyika. Inaelezwa kwamba Japhet Kirilo na washili wa Meru walichanga fedha ya nauli na walikataa kabisa kufadhiliwa na wakoloni katika harakati hizo.
Japhet anaelezwa kuwa tishio kwa wakoloni na alifanikiwa kuifanya sehemu ya meru kutotawaliwa badala yake waliojipanga kutawala waliishia kutumia mfumo wa uwekezaji badala ya utumikishaji wa wazi.
Historia kama ya Japhet Kirilo kwanini haizungumzwi? Inaelezwa kwamba, baada ya wakoloni kuona vuguvugu la kudai uhuru limepamba moto waliamua kumuunga mkono Mwalimu kwa kumtaka afanye iwezekanavyo asimame kwa uhuru wa Tanganyika.
Kwa kuzingatia wakoloni walikuwa wanapashana habari mwalimu alipoingia madarakani alianza kupambana na wapigania uhuru wenzake bila kujua hizo zilikuwa trick za wakoloni.
Mwalimu kwa mujibu wa wazee alipopata Uhuru na bila hata sababu ya msingi alielekeza Japhet Kirilo awekwe kizuizini huko nyumbani kwake Meru na asiruhusiwe kutoka nje ya eneo lake bila kibali cha Mhe, Rais.
Inaelezwa kwamba baada ya Japheti waliendelea kuwekwa kizuizini akina Kambona na pia joto lilipopanda ilibidi hata Jenerali Sarakikya aondolewe Jeshini kuzima vuguvugu la ukinzani wa hoja ndani ya serikali. huo ndio ukawa mwisho wa Japheti katika siasa, wazee wanahoji endapo mwalimu asingemweka kizuizini Mwinyi angekuwa Raisi?
Wanamjadili pia kijana wao Sokoine, Mmmasai ambaye wazee wanaamini aliondolewa Duniani kwa sababu ya misimamo na uzalendo wake. Anatajwa Sokaine kama Rais wa pili wa Tanzania aliyekatishwa uhai kupisha nguvu ya rushwa kuendelea kutamalaki katika nchi.
Yawezekana wazee hawa wangepewa nafasi ya kuishi nchi yetu ingekuwa kama Malysia. Kwa bahati mbaya wanapozaliwa viongozi na wakaonyesha uongozi mifumo ya nchi inawakataaa, Buriani Sokoine
Katika moyo ule ule wakuendelea kufifisha ndoto za viongozi wanaozaliwa katika ukanda wa kaskazini, wanaibuka watu nakusema adharani kwamba kaskazini awatawala nchi, means hawa siyo watanzania.
Awamu ya nne ikachukua nafsi ya usaliti na kuamua kupambana na kiumbe mwenye uthubutu na anayesimamia kile anachokiamini. Anaadhibiwa Lowasa asipate Urais si kwa sababu nyingine bali ni kudhibiti ukanda wa kaskazini usivuke viwango vingine.
Lowasa analala akiwa na maumivu makubwa yaliyotokana na usaliti uliofanywa na mtu wake wa karibu ambaye hakustahili kumfanyia yote haya. Anapata stroke na kuugua kwa muda mrefu jambo inaloweza kulilinganisha na yule aliyewekwa kizuizini.
Kama aishivyo, matosa haya aliyopitia katika siasa yanamfanya awe mwanasiasa anayeondoka Duniani akiwa mwanachama wa vyama vyote vya siasa nchini. Ni mwanasiasa aliyeamini katika yeye na si katika wao.
Alitambua anachokitafuta na alipokikosa CCM alitoka adharani na kuwaambia wao siyo mama yao. Pamoja na kumuibia kura iliwalazimu watesi wake waanze kukamata mali zake na watoto wake kisha kuwaweka ndani kushinikiza arejee CCM.
Bila yeye kurejea CCM bado usalama haukupatikana, aliporejea CCM hakukaa kama mwana CCM bali alishiriki kuikomboa familia yake iliyokuwa inateswa si kwa kuwa na hatia bali kwa wivu wa wanasiasa kuhusu KWANINI LOWASA ANAPENDWA KULIKO WAO?
Wazee wa kimasai na kimeru wanakula nyama na kusherekea nguvu kubwa waliyojaaliwa kwenye viuno vyao yakuwezesha kuzaa watoto wenye nguvu ya kimamlaka na wanaweza kusimama imara kulitetea Taifa. Moja ya wazee akasema, Lowasa, Sokoine, Japhet na Sarakikya ni baadhi ya viongozi wanaoandaa njia ya MUSA kuwaondoa wana wa Israel utumwani.
Nenda LOWASSA.