Lowassa akipata urais kupitia UKAWA tutarajie nini ndani ya CCM?

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
Wakuu mambo yanazidi kunoga noga kama chachandu,Lowasa ndio katia timu ukawa na lazima atakua mgombea urais wa ukawa na kwa jinsi huyu jamaa anavyopendwa na watu wallah CCM lazima wakae chini.

Lowasa ana nyota kali sana nadhani mpaka sasa CCM wanajuta sana,magufuli ni mzuri hatukatai lakini hana nguvu ya kupendwa kama Lowassa.

SWALI ikitokea lowasa kashinda uchaguzi na kuwa rais, tutegemee ni kitu gani kitakachotokea ndani ya CCM?
 
Tutawadhalilisha vibaya sana na watasahau miaka 50 waliyotesa na familia zao na kupitisha mikata mibovu.
 
Ndugu maisha yataendelea kama kawaida
ila waliohujumu uchumi wa nchi wajiandae
kwenda jera,na hakuna habari ya kuzifanyia jela
marekebisho maana hata wanaoishi huko ni watu pia.

Wengi wanasema EL atalipa kisasi
tunasema kisasi ni Mungu tu anayeweza kuwalipa wanadamu
lakini tukumbuke kumshtaki mharifu siyo kulipa kisasi
kwani alipokuwa anafanya uharifu alijua kwamba anavunja
sheria na hivyo alikuwa anajua kuwa siku moja ataangukia mikononi mwa sheria.
Hivyo akikumbwa na mkono wa sheria sio kisasi ni haki ya mtu.
 
wakuu mambo yanazidi kunoga noga kama chachandu,lowasa ndio katia timu ukawa na lazima atakua mgombea urais wa ukawa na kwa jinsi huyu jamaa anavyopendwa na watu wallah ccm lazima wakae chini, lowasa ana nyota kali sana nadhani mpaka sasa ccm wanajuta sana,magufuli ni mzuri hatukatai lakini hana nguvu ya kupendwa kama lowasa. SWALI ikitokea lowasa kashinda uchaguzi na kuwa rais, tutegemee ni kitu gani kitakachotokea ndani ya CCM?

Hiyo watajua wenyewe, wasitupotezee muda!
 
Ndugu maisha yataendelea kama kawaida
ila waliohujumu uchumi wa nchi wajiandae
kwenda jera,na hakuna habari ya kuzifanyia jela
marekebisho maana hata wanaoishi huko ni watu pia.

Wengi wanasema EL atalipa kisasi
tunasema kisasi ni Mungu tu anayeweza kuwalipa wanadamu
lakini tukumbuke kumshtaki mharifu siyo kulipa kisasi
kwani alipokuwa anafanya uharifu alijua kwamba anavunja
sheria na hivyo alikuwa anajua kuwa siku moja ataangukia mikononi mwa sheria.
Hivyo akikumbwa na mkono wa sheria sio kisasi ni haki ya mtu.

yeye EL ametokea wapi? ndio wale waleee
 
yeye EL ametokea wapi? ndio wale waleee
Ndugu mazingira unayoishi au kufanyia kazi yanachangia,

Ukimkuta simba anayefugwa na binadamu ukamlenga bunduki
na kumuua kisa eti simba wa porioni huwa na tabia ya kuua binadamu utakua unakosea.

Lowasa wa CDM/UKAWA ni tofauti nayule wa ccm
kwani sera za vyama ni tofauti,
Hivyo tusimuhukumu kwa sababu ya mazingira aliyotoka
bali tutamuhukumu kwa yale atakayoyatenda akiwa makazi mapya.
 
kwa nini mtu aliyewahi kufungwa jela haruhusiwi tena kufanya kazi serikalini?? hata kama atabadilika???
fikiria jibu kwa undani zaidi halafu fikiria na skendo alowahi kufanya huyo simba wako alipokuwa ccm na skendo za magufuli alipokuwa huko CCm
 
Back
Top Bottom