Lowassa adaiwa kutaka kuuawa!

mwaka 2005 ccm walicheza mchezo wa kuwaogopesha watu kuhusu mrema
mwisho watu ikawa mrema,mrema,mrema...

nahisi haya marudio sasa
 
Napita tu ila nataka kusema kipimo anachowapimia wenzie naye ni kipimo hicho hicho atapimiwa na kila nafsi itaonja mauti.
 
Tujuze basi huo mfumo wa ccm,mwenyekiti wake taifa anachaguliwaje?

"Hii habari inawezekana kuwa kweli maana ugomvi wa EL na JK uko live kwa sasa na lazima mmoja apungue kwenye siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM mwakani. Unajua EL ana mtandao mkubwa wa wenyeviti wa CCM mikoani na anaweza kumshinda JK kwenye uenyekiti wa taifa which means baba Riz anaweza kutemeshwa kitumbua cha pale magogoni. Kikawaida hawezi kukubali hilo litokee akiwa anaangalia tu."

Maelezo hayo hapo juu yanadai kuwa Ikiwa EL atagombea uenyekiti na kushinda basi JK atatema Kitumbua pale Magogoni. Na huo sio Mfumo wa CCM. EL akishinda, atakuwa M/kiti na Jk ataendelea kuwa Rais, Ule Mfumo wa Ukiritimba ulishafanyiwa masahihisho na Mwasisi wa Mfumo wenyewe (JKN) Alipomkabidhi Mwinyi Urais na yeye akakumbatia Uenyekiti.

Ili uelewe zaidi tafuta katiba ya CCM (105). Na kwa maelekezo ya katiba ya CCM EL ameshapoteza sifa za kuwa Mwenyekiti.
Anatakiwa Mtu wa kusimama na kutoa Tafsiri fasaha ya katiba Katika kipind na Wakati Mwafaka and that will be THE END of Lowasa in Politics.
 

Sizungumzii mfumo mkuu bali nazungumzia hali halisi iliyo ndani ya CCM. We tuelezee mfumo wao wa uchaguzi labda nimekosea mwaka wa uchaguzi but waulize wakuu wa CCM watakwambia kuwa EL ana nguvu sana kwenye chama na ndio maana hata kumvua gamab juzi wameshindwa. Mkapa aliliona hilo na ndio maana akamwambia JK funga hiyo hoja watu wasiendelee kuichangia maana aliona JK anavuliwa nguo na watu walishaandaa hoja ya kumvua uenyekiti kama ilivyokuwa kwa Thabo Mbeki wa South na issue ya Zuma.

Kumbuka JK ni mzee wa visasi, kama aliamua kuwa mpole pale Dodoma, uandhani ataendelea kuwa mpole daima? EL ametoka dodoma ameenda kujitangazia ushindi kwenye harambee za makanisa huko Singida. Bado tu huoni kuwa hali ya JK na EL ni tete??

Sina haja ya kubuni tuhuma lakini kwa kuwa wote tuna macho basi tusubiri tuone mwisho wa issue ya magamba utakuwaae. Kama EL akibaki na nguvu zake sioni JK akibaki kuwa M/Kiti wa CCM na sioni hilo likitokea kwa JK kukubali adhalilishwe akiwa madarakani. Sijui mwenzangu mfumo wako wa ucahguzi wa CCM unakwambiaje. Jipime na huo mfumo uone kama utapata majibu sahihi.
"Hii habari inawezekana kuwa kweli maana ugomvi wa EL na JK uko live kwa sasa na lazima mmoja apungue kwenye siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM mwakani. Unajua EL ana mtandao mkubwa wa wenyeviti wa CCM mikoani na anaweza kumshinda JK kwenye uenyekiti wa taifa which means baba Riz anaweza kutemeshwa kitumbua cha pale magogoni. Kikawaida hawezi kukubali hilo litokee akiwa anaangalia tu."

Maelezo hayo hapo juu yanadai kuwa Ikiwa EL atagombea uenyekiti na kushinda basi JK atatema Kitumbua pale Magogoni. Na huo sio Mfumo wa CCM. EL akishinda, atakuwa M/kiti na Jk ataendelea kuwa Rais, Ule Mfumo wa Ukiritimba ulishafanyiwa masahihisho na Mwasisi wa Mfumo wenyewe (JKN) Alipomkabidhi Mwinyi Urais na yeye akakumbatia Uenyekiti.

Ili uelewe zaidi tafuta katiba ya CCM (105). Na kwa maelekezo ya katiba ya CCM EL ameshapoteza sifa za kuwa Mwenyekiti.
Anatakiwa Mtu wa kusimama na kutoa Tafsiri fasaha ya katiba Katika kipind na Wakati Mwafaka and that will be THE END of Lowasa in Politics.
 
Ili uelewe zaidi tafuta katiba ya CCM (105). Na kwa maelekezo ya katiba ya CCM EL ameshapoteza sifa za kuwa Mwenyekiti.
Anatakiwa Mtu wa kusimama na kutoa Tafsiri fasaha ya katiba Katika kipind na Wakati Mwafaka and that will be THE END of Lowasa in Politics.
Ndani ya CCM huwa hakuna kupoteza sifa ikipotea inanunuliwa.
 
DIRA YA MTANZANIA

ISSN 1821 – 641 TOLEO NO. 141 JUMATATU DESEMBA 19-21. 2011 BEI T.SH 500 KSH.80 USH.800

SIRI YA KUMUUA LOWASSA YAFICHUKA
· Mwanaye ahamaki, abugia kilevi, ashambulia usalama wa taifa
· Polisi wagwaya kumkamata, atoweka na kuzima simu yake ya kiganjani

Na Angela Kiwia

Siri ya kumuua Waziri Mkuu wa kwanza wa awamu ya nne aliyeondoka kwenye wadhifa huo baada ya kuhusishwa kweney kasha ya Richmond, Kapteni Edward Lowasaa, imefichulia. Aliyefichua siri hiyo ni mwanaye mkubwa wa kiume, Fred Lowassa ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alimshambulia kwa maneno makali mmoja wa maofisa usalama wa taifa mkoani Arusha, akimtuhumu kuwa ni mmoja wa watu wanaopanga njama za kumuua baba yake.

Taarifa zilizotufikia zimeelzea kuwa Fredo Lowassa ambaye wiki iliyopita alikuwa mkoani Arusha, alifikia Hotel ya Mount Meru akiwa na marafiki zake kadhaa kwa ajili ya kunywa pombe na kubadilishana mawazo.
Kwambba wakiwa hapo, mmoja wa maofisa usalama wa taifa mkoani hapo aliyetajwa kwa jina la Suleiman Mombo, naye aliingia katika hotel hiyo kwa lengo ambalo halijatajwa na kupita karibu na mahali ambapo Fred Lowassa na wenzake walikuwa wameketi wakifanya mazungumzo yaliyokuwa yakisindikizwa na unywaji wa kilevi.
Mashuhuda waliokuwa katika hoteli hiyo wamedokeza kuwa mara baada ya Mombo kuketi, Fred Lowassa alisimama na kumfuata alipokuwa na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku akimtuhumu kuwa ni mmoja ya wanausalama wanaopanga njama mbaya za kumuua baba yake.

"Fred alikutana na Mombo katika Hoteli ya Mount Meru, alikuwa na wenzake kadhaa wakipata kinywaji, Mombo naye alifika nadhani hakujua kam Fred alikuwa pale na alipoketi tu Fred alimfuata na kuanza kumtuhumu kuwa amepata taarifa kuwa jamaa ana mpango wa kumuua baba yake, Edward Lowassa. Watu walibaki wakiwa wameduwaa manake tuhuma hizo ni nzito", alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa wakati Mombo akituhumiwa kuhusika na njama hizo za mauaji alibaki akiwa ameduwaa lakini alipoona anazidi kushambuliwa kwa maneno makali aliamua kupiga simu polisi ili kupata msaada, ambapo haraka polisi walifika eneo hilo na kumchukua Fred Lowassa hadi kituoni ambako walimtaka aandike maelezo yake kuhusiana na tuhuma alizomuelekezea mombo. Wapasha habari wetu waliokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa karibu wamedokeza zaidi kuwa Fred Lowassa hakuwa tayari kuandika maelezo kuhusiana na tuhuma alizomuelekezea Mombo na alipobanwa afanye hivyo aliangua kilio huku akiomba asamehewe kwa sababu kilichomsukuma kutoa thuma hizo ni kilevi kingi alichokuwa amekunywa.

"Polisi walitaka Fred aandike maelezo ambayo pia alitakiwa kuyatolea ufafanuzi ili jeshi liweze kutunza kumbukumbu dhidi ya tuhuma hizo na kuzifanyia kazi, lakini aligoma kabisa na alipobanwa aliangua kilio huku akidai kuwa ni pombe alizokunywa ndizo zilizosababisha amshambulie Mombo. Utetezi huo ulikubaliwa na polisi na kumtana kurejea kituoni hapo siku inayofuata."

"Kosa walilofanya polisi ni kumruhusu aondoke kwa makubaliano ya kurudi siku inayofuata ili kuandika maelezo akiwa hana kilevi, alipotoka hapo, alitoweka moja kwa moja na simu zake zote akazima", alieleza shuhuda mwingine wa tukio hilo.

Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kuondoka katika kituo cha polisi, Fred Lowassa alikwenda kujificha mahali pasipo julikana na kuzima simu zake zote kwa kuogopa suala la mauaji ya baba yake kuanza kuchunguzwa na vyombo vya usalama huku yeye akiwa shahidi namba moja na kwamba madai hayo aliyatoa pasipo kuwasiliana na Lowassa mwenyewe au watu wake wa karibu.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa hivi sasa polisi mkoani Arusha wanahaha kuhakikisha taarifa za kuibuliwa mpango wa siri ya kumuua Lowassa hazivuji zaidi kwa kile kinachoelezwa kuwa Lowassa amekasirishwa na taarifa hizo kwa sababu zinaweza kuwa na athari mbaya kwake kisiasa.

"Kuna jitihada za kumaliza suala hilo ili taarifa zake zisitoke, inasemekana mzee wake amekasirishwa na taarifa hizo kwa sababu ni mbaya na hataki zikuzwe,hata hivyo hakuna polisi mwenye uwezo wa kumkamata Fred, anaogopwa sana hapa Arusha kutokana na jina la baba yake. Hivi ninavyokuambia kila anayeambiwa kwenda kumtafuta anagoma kwani hakuna wa kumgusa, hajarudi na wala hawajui alipo pamoja na kuwa Mombo kuwaambia anamuhitaji ili kupata maelezo yake, polisi wote wamenywea, alieleza mtoa habari wetu.

Jitihada za kumpata Fred kuzungumzia tuhuma hizo hazijafanikiwa kwa zaidi ya wiki moja sasa baada ya simu yake ya kiganjani kutopatikana na hata jitihada za kupata taarifa zake kutoka kwa watu wake wa karibu nazo zimeshindwa kuzaa matunda baada ya kueleza kuwa hawajui alipo na hawampati katika simu zake za kiganjani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikana kufahamu kwa kueleza kuwa hana taarifa zozote kuhusu madai mazito kama hayo kutolewa na Fred dhidi ya afisa usalama wa taifa.

Huku akionyesha kushangazwa na taarifa hizo alisema ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwenye gazeti hili.
Wakati afabde Mpwapwa akikana kufahamu tukio hilo, Mombo amelithibitishia gazeti hili kuwa tayari amekwishatoa taarifa za tukio hilo la kushambuliwa kwa maneno makali na kutuhumiwa kupanga njama za mauaji dhidi ya waziri mkuu wa zamani, Lowassa, kwa polisiwa Arusha.

"Suala hili nililiwasilisha kwa kamanda wa polisi mkoa, hivyo yeye ndiye anaweza kukufafanulia ni hatua zipi zimechukuliwa mpaka sasa, ebu mtafute akwambie amefikia wapi kwani nilishatoa maelezo yangu polisi" alisema mombo.

Taarifa nyingine kutoka kwa watu walio karibu na familia ya Lowassa zimeelewa kuwa Fred lowass hakumshambulia kwa maneno makali Mombo bali alikwenda kueleza masikitiko yake kutokana na njama ovu za kumuua baba yake (Lowassa) zinazopangwa na wenzake.

"Hakukuwa na kurushiana maneno au kushambuliana kwa maneno, Fred na Mombo ni marafiki. Mombo akikwama kifedha huwa anapata msaada kwa Fred, sasa siku akiwa na taarifa mbaya dhidi ya Mombo alipomuona pale Mount Meru alimfuata na kumwambia wewe sio rafiki mzuri kwani licha ya kusaidiana katika shida na raha bado unashirikiana na watu wanaotaka kumuua baba yangu.

"Mombo alipotoka hapo, alikimbilia polisi na kufungua jarada, Fred akaanza kutafutwa lakini alikuwa amekwisharudi Dar. Alipigiwa simu na RCO akadokezwa kuwa amefunguliwa jarada na akamtaka afike kuandikisha maelezo yake. Baada ya hapo fred alimpigia Mombo na kumueleza masikitiko yake ya kulifikisha suala hilo walilokuwa wakiongea kirafiki polisi. Hapo ndipo akazima simu ili kujipanga", alisema mmoja wa watu waliokuwa karibu na familia ya Lowassa.

Aliongeza kuwa kilichofanywa na Mombo ni kumshughulikia Fred kupitia mtandao wa wanasiasa wanaohasimiana na baba yake kwa saabu suala hilo likifikishwa polisi na ushahidi kukosekana, atakuwa matatani.

Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kunzungumza na Lowassa mwenyewe hazikufanikiwa baada ya simu kuita mara kadhaa pasipo majibu.

***********
Nikipata nafasi ntawawekea:

DIRA LA TAREHE 22-25 Dec: TISHIO LA KUUWAWA LOWASSA:pOLISI WAFICHA SIRI - WAKATAA KUTOA TAARIFA ZA MWENENDO WA UCHUNGUZI;

DIRA DEC 26-28:TISHIO LA LOWASSA KUUWAWA: CCM YANAWA MIKONO:YASEMA SI JADI YAKE KUSUKANJAMA ZA MAUAJI: YAMTAKA FRED LOWASSA ATOE USHAHIDI WAKE:EDWARD SOKOINE, KOLIMBA WASIHUSISHWE.

Nawasilisha
 
chanzo cha habari hii ni gazeti la Dira ya Mtanzania, inadai CCM wananjama za kummua Lowasa
walidokezewa na Fred Lowasa, mtoto wa mjini huyu(itakuwa kweli)
mzee wa visasi,ama wafuasi wake wamekerwa na kuvuliwa nguo na E.L kuhusu Richmond

aidha Katibu Mwenezi wa ccm(Nape) amekanusha akidai chama chao hakijawahi na hakitafanya hilo
pia amesisitiza TISS haipo chini ya ccm, hivyo hawana mandate ya kutoa order hata kama wangekua waovu

Lakini si ipo chini ya RAISI? na RAISI si ndio mwenyekiti wa CCM? Sasa itakuwa vipi aipo chini ya CCM?
 
mushi yamekua hayo tena swahiba? Mbona ikija issue ya el tunapoteza kabisa wisdom?
Naaw mkuu! BTW how is it i lost wisdom, naomba unieleweshe na mimi ntakupa ma position and also ku explain more and hoping you'll understand...

If naw ima try again..
 
thanks pasco, kwa weledi na upeo wako, we unadhani likelihood ya hilo kutokea yaweza kwenda percentage gani?
MTM hapa ndipo ile kauli ya politics is a dirty game inapo apply, kwenye siasa hakuna permanent friends, wala permanent enemies, there is only common interest!.

Kwa vile Lowassa alikubali kulibeba lile zigo la Richmond ili kuwasibia watu fulani aibu ya mwaka, sasa amegadhibika sana baada ya hao hao aliwafichia aibu zao, kuvituma vitoto vidogo vijinga vijinga kuzunguka nchi nzima huku vikipuliza vuvuzela za kujivua gamba na kutamba vimetumwa wakati ukweli ni kuwa hao wanaodaiwa kuvituma hivi vitoto ndio wenye richmond halisi!.

Kwa hali kama hii, hao jamaa watakuwa wanammnonitor EL 24/7 ili kujiridhisha hatasema ukweli, wakijiridhisha kuwa atakaa kimya kama alivyonyamaza mwanzo, then he is safe!, akiendelea kupayuka payuka, mwisho wa siku atausema ukweli halisi, sasa kuliko ukweli kujulikana, wanaweza kuamua kumpotezea kabla!
 
Mkuu let me be clear

ukisoma post ya pasco amepost kama vile tayari anajua likelihood ya jamaa kuuwawa au la, and that ahs been our weakness as JF members we usually throw some tokens of ideas and runa away from them when asked to justify... unaporejea post ya pasco na jitahidi sana kunielewa natafuta nini

it would have been easier kusema hivi: nijuavyo mimi uwezekano wa kuuwawa lowassa upo au haupo na ni xxx.

Personally sidhani kama Lowassa kwa tentacles alizonazo anahaja ya kutmia mwanawe kusema anataka kuuwawa this is not possible unless gazeti limemkopi vibaya au ni siasa uchwara

kama ni wa kuuwawa angeshajua kwani yeye ni mmoja wao

we just want to prolong uzushi wa wanasiasa.....

SIONI HAJA WALA ULAZIMA WA KUMUUA EL
nadhani jibu hili pia utalizingatia, kwani inakijua kilichomuua, Karume, Sokoine, Kulimba, Kombe, Mbatia etc and list goes on

MTM hapa ndipo ile kauli ya politics is a dirty game inapo apply, kwenye siasa hakuna permanent friends, wala permanent enemies, there is only common interest!.

Kwa vile Lowassa alikubali kulibeba lile zigo la Richmond ili kuwasibia watu fulani aibu ya mwaka, sasa amegadhibika sana baada ya hao hao aliwafichia aibu zao, kuvituma vitoto vidogo vijinga vijinga kuzunguka nchi nzima huku vikipuliza vuvuzela za kujivua gamba na kutamba vimetumwa wakati ukweli ni kuwa hao wanaodaiwa kuvituma hivi vitoto ndio wenye richmond halisi!.

Kwa hali kama hii, hao jamaa watakuwa wanammnonitor EL 24/7 ili kujiridhisha hatasema ukweli, wakijiridhisha kuwa atakaa kimya kama alivyonyamaza mwanzo, then he is safe!, akiendelea kupayuka payuka, mwisho wa siku atausema ukweli halisi, sasa kuliko ukweli kujulikana, wanaweza kuamua kumpotezea kabla!
 
Gazeti lililotoa habari hiyo ni Dira ya mtanzania.

Habari hizo si za kuupuuzia kwani lolote linaweza kutokea, na haya ni baadhi ya mambo muhimu ya kukumbuka au kuzingatia:

1. Mtoto wa Lowassa ni mtu muhimu sana katika harakati nzima za maisha binafsi & kisiasa ya Lowassa, Hicho alichokisema ndio kauli isiyo rasmi ya Lowasa. Hivyo kuna haja ya vyombo husika kumhoji au kufuatilia zaidi.

2. Ni ukweli usiofichika kuwa usalama wa taifa pia imehusika na matukio ya kutengeneza ya vifo vya viongozi mbalimbali hasa kama viongozi hao wanasiri ambazo wanaweza kuzitoa na kuhatarisha usalama wa taifa (mtu yoyote aliyewahi kufanyakazi na idara hii atakwambia hili)

3. Kwa Lowassa hili linaweza kutokea saa yoyote, kwani alichokiongea ndani ya CC ni kitu kikubwa sana,na kama atatakiwa kuutoa ushahidi kisheria,maana yake nchi lazima itayumba,kwani mkuu hatapona.

4. Viongozi ndani ya CCM hawaaminiani kabisa kila mtu anamtafuta mwenzie ammalize kabisa (Hili JK aliwahi kulisema pia ndani ya vikao vya chama)
Mkuu Herieely asante kwa hii, natumain MTM umensoma huyu jamaa!.
 
neither a counter nor premptive

this is a mis-calculated political fortune for EL

the end off the road is very close
 
Ooh Boy.. nadhani tumuunge mkono Lowassa awe chaguo la CCM ili yaishe.
Asante sana Mkuu Mzee Mwanakijiji, now we sail the same boat, kazi ya kwanza ni kumshawishi Lowassa alitue hilo zigo la ... lililomchafua na kumfanya anuke hadi wengine humu ukiwemo wewe kuamini kuwa hasafishiki!.

Lowassa hapa ni mbeba pakacha tuu, na pakacha kuvuja ndio nafuu ya mchukuzi, mwanzo Lowassa alipojitolea kulibeba pakacha hili, ilifanya papara bila kujua umbali halisi anapotakiwa kulifikisha pakacha hilo!. Mpaka sasa, safari imekuwa ndefu, hatimaye pakacha hilo limeanza kumuelemea.

Mwenye pakacha akishajua pakacha lake linamwelemea mchukuzi, anakuwa na option mbili tuu, kwanza ama amtue mchukuzi lile pakacha na mchukuzi apumzike ndipo safari iendelee (kumteua Lowassa kuwa mgombea wa CCM), au kumuacha mchukuzi alibebe mpaka atakapoishiwa nguvu kabisa, atalibwaga pakacha hilo na kujiishia vyake bila hata kusubiri malipo, sasa hapo ndipo wapitanjia watumshudia mwenye pakacha akijikusanyia bidhaa zake ambazo zitakuwa zimetawanyika chiniu na watu kushangaa kilichokuwemo mule kwenye pakacha lile!.

Swali ni jee, mwenye pakacha yuko tayari kumshudia mchukuzi akilibwaga pakacha lake?. Hapa ndipo sasa hii dhana inapopata nguvu, bora mchuuzi afe lakini mzigo ufike salama kuliko kumsubiri mchuuzi aelemewe na kulibwaga chini puu hilo pakacha na wapita njia wakaona kilichomo, masikini mchukuzi wa watu, ... atawahiwa!.
 
Back
Top Bottom