Debate hii ya Ujamaa ni nzuri na ilitakiwa iendelee katika nyanja zote za elimu Tanzania, bahati mbaya ni kuwa ukiwauliza watoto wa secondari Tz leo wengi watadhani Ujamaa ni mnyama fulani. Zakumi ni vigumu kusema Ujamaa ulifeli au la. Nimehudhuria mkutano aliousema Companero kule Whitesands uliojaribu kuelezea nafasi ya serikali katika kuleta maendeleo katika uchumi wa soko huria na moja kati ya yale yaliyojadiliwa ni kuwa siasa za ujamaa zilikuwa sahihi Tz kwa sababu zilikuwa zinajaribu kabisa kujibu maswali muhimu sana ya maendeleo. Labda tu matatizo na makosa yalitokea katika kujibu maswali hayo kwa upande wa uchumi. KIlichosemwa katika mkutani ni kuwa Tz ingeweza kutekeleza ujamaa ktk uchumi wa soko huria, yaani mfumo wa uchumi unaoruhusu free enterprising ungewezekana ktk ujamaa na kama ungeruhusiwa tangu zamani usinge sababisha matatizo makubwa ya kiuchumi ya miaka ya 80. Kwa taarifa tu ni kuwa Tz haijauacha Ujamaa. Ujamaa bado uko kwenye katiba ambayo inasema Tz ni nchi ya kijamaa. Na hata sasa tunaweza kurudisha mfumo wa ujamaa katika mazingira ya soko huria. Utaifishaji ulikuwa sahihi. Lakini ilikuwa kosa kutaifisha kila kitu.