Liyumba (wa BoT) na wenzake kizimbani Kisutu

Mkuu YY,

Jamaa (Liyumba na Deogratias Kweka) wanapandishwa kizimbani dhidi ya kashfa ya Twin Tower.

Nipo hapahapa Kisutu, nitawafahamisha kinachoendelea

Mkuu salute, keep flowing...
Tunasubiri hizo charges za hawa jamaa
BTW: Hapa nilipo najifanya mzee wa breaking newz na info muhimu, kumbe nachungulia jf!
 
Huyu si ndiye yule aliwahi kuzungumzwa na mmojawapo wa viongozi wa juu nchi hii siku ya ukimwi duniani kuwa akiwanunulia visichana magari mekundu, nguo nyekundu na kufanyia mapenzi kwenye shuka nyekundu and of course akiwalipa noti nyekundu nyekundu za 10 thousand? SI ndiye huyu? Huyu hakuhusika na kusimamia ujenzi wa twin towers huyu? Jamaa mbwembwe na maringo mengi sana akitembea mabega juu. Yuko mwingine pia alihusika na kuileta Net Group Solutions pale TANESCO akishirikiana na shemeji wa kigogo mmoja wa awamu ya tatu. Naye alikuwa anapiga maji sana kwam vile fedha ilikuwepo mpaka maini yakaungua na figo kujaa mawe. Kufuru ya fedha na ufisadi. We acha. Kweli malipo ni hapa hapa duniani.
 
Ndiye yeye mkuu kwa akina dada wenye tamaa pale dar es salaam wamemfaudu lakini na yeye kawapa mambozzz...hakuna rangi wataacha ona hasa nyekundu...
 
Kwa sasa ishakuwa ngumu. Wamepelekwa Keko kwani bail yao ilikuwa ni nusu ya kiwango kinachoaminiwa kuibiwa (Bilioni 221).

Vogue ya Liumba ameiacha pale PCCB
 
Kiasi cha pesa kinachohitajika kurejeshwa ni Tshs 221,197,299,200/= ambapo wawili hawa wanatakiwa kwa pamoja ili kupata mdhamana watoe nusu ya kiasi hicho juu.

Kaazi kwelikweli
 
Kiasi cha pesa kinachohitajika kurejeshwa ni Tshs 221,197,299,200/= ambapo wawili hawa wanatakiwa kwa pamoja ili kupata mdhamana watoe nusu ya kiasi hicho juu.

Kaazi kwelikweli

Asante mkuu Invisible,

Hawa watatoka kweli? Hicho kiasi cha fedha kikubwa mno. Hapo si tungejenga reli ya maana japo km 100?
 
kiasi cha pesa kinachohitajika kurejeshwa ni tshs 221,197,299,200/=

mimi nasikitika tulivyo masikini wa kujitakia kwa kutofuata sheria tu. Jk amekwenda pemba kufungua barabara sijui ilikuwa km 9 vile?

Hii hela ya hawa inayotuhumiwa ingetosha kujenga barabara ya kiwango cha lami huko mikoani na wilayani zisizopungua km 500-800. Ukijumlisha epa, meremeta, deep green na kwingineko ni zaidi ya km 5000. Nchi hii ingekuwa imeenea mtandao wa barabara.

Sijui niseme je, inaudhi hasa. Wanafunzi hawakopeshwi fedha, afya hakuna na mengi mabaya tu huku nchi. Itabadilika lini?

Hebu wamkamate na mkapa mara moja, hawezi kuendelea kuzunguka tuu kama mjusi.
 
Last edited:
Mimi naona kama 'changa la macho' sidhani kama hawa jamaa watafungwa,mbona Malegesi hawamleti?
 
Wakuu mimi nashindwa kuelewa hapa kwamba Liumba anahusikaje maana he was more into administration. Huyu Kweka yeye alikuwa Projects manager kwa hiyo is a right target. Na itanishangaza Kuliko kawaida ikiwa eti Liumba alikuwa ndio anaapprove issue za ujenzi wa tower hizo. Mimi on my opinion naamini kabisa hawa ni vijidagaa na inawezekana kabisa hili ni changa la macho!
 
Wakuu mimi nashindwa kuelewa hapa kwamba Liumba anahusikaje maana he was more into administration. Huyu Kweka yeye alikuwa Projects manager kwa hiyo is a right target. Na itanishangaza uliko kawaida ikiwa eti Liumba alikuwa ndio anaaprove issue za ujenzi wa tower hizo. Mimi on my opinion naamini kabisa hawa ni vijidagaa na inawezekana kabisa hili ni changa la macho!

tumewaza pamoja rejea mjibu ya aliyekuwa Waziri wa fedha Mhe. Zakia Meghji....
 
Mimi naamini kama ni waungwana watasema ukweli kwani hizo pesa ni nyingi sana kulinganisha na pesa walizonazo ina maana wamekula na wengine
 
Mkuu, Hii ni Billion 221 na ushee, za kina Maregesi unaongelea zile za EPA sio? Epa cha mtoto katika hii issue
...unazungumzia equivalent STG £60m au USD £84m hivi...?

ngoja zichangishwe chap chap...! within a week watakuwa nje.
 
Kiasi cha pesa kinachohitajika kurejeshwa ni Tshs 221,197,299,200/= ambapo wawili hawa wanatakiwa kwa pamoja ili kupata mdhamana watoe nusu ya kiasi hicho juu.

Kaazi kwelikweli

...mama yangu weeee,zaidi ya dollar milioni mia mbili? nina uhakika hii pesa ingeweza kukata ile foleni ya magari Dar kwa 100% na kujenga Kigamboni bridge na hata kuongeza 100MW kwenye grid ya Taifa,lakini jamani kama project moja tuu imeweza kulipua 200m USD,je ile nchi ina projects ngapi ambazo nyingine nina uhakika pesa zimetolewa lakini hata hatujawahi kusikia kwa sababu mafisadi walimaliza pesa kabla hazijaanza...yaani EPA,Radar,President Jet,Richmond,Twin towers,IPTL,mikataba ya kina Karamagi ya madini mpaka bandari,mashangingi ya serikali etc wakuu hapo tunaongelea zaidi ya dollar billion moja...naamini tulitakiwa tusiwe na shida ya umeme na barabara zote kuu zingekuwa za lami kama serikali ingekuwa makini,ukiangalia vizuri huu upuuzi wote ulikuwa under Mkapa watch,kweli Mkapa was sooooo much Mr Clean!
 
Oyaa....vipi yule mzungu wako wa kwenye trailer park....? keshakutosa nini
 
Kuna haja ya ku-revisit the foundations of this nation na kuona ni wapi tulienda wrong. Siku zote tumekuwa tukibeza corruption ktk Nigeria lakini kumbe na sisi wamo kwa sana tu. Hata ile taasisi ya kuhunguza/ kuevaluate ufisadi TI - Tranparency international nadhani imekaa kimazabe mazabe tu si walituambia kama miaka mitatu iliyopita kwamba ufisadi umepungua mno nchi hii!!!!!!!
 
Mkuu YY,

Jamaa (Liyumba na Deogratias Kweka) wanapandishwa kizimbani dhidi ya kashfa ya Twin Tower.

Nipo hapahapa Kisutu, nitawafahamisha kinachoendelea

Mwaka huu Mambo juu ya Mambo. Wakati Liyumba alikuwa Mkurugenzi anayesimamia maendeleo yote ya BOT ikiwemo ugavi na ununuzi, mwenzake Kweka ndiye Mhandisi Mwandamizi wa BOT. Katika vikao vya arusi za watoto wa vigogo hapa Dar salaama watu huwa huja na magari ya nguvu (Vogue, V8X etc); kumbe wizi mtupu. Basi tusubiri kumekucha kama TAKUKURU wamekusanya ushahidi wa uhakika, nafikiri hapa wanaweza fanikiwa kufunga na kuwafilisi watuhumiwa na kunasa msururu wote wa wafaidika..
 
Na hiyo kampuni ya Group five international (Mkandarasi mkuu kwenye twin towers) kuna haja ya kuichunguza
 
Back
Top Bottom