Liyumba aachiwa lakini PCCB wambeba...

nani kakwambia hr manager na project manager wanaweza kuchukua $200m za benki kuu peke yao, uongo uliokubuu...

Nakubaliana na wewe,HAIWEZEKANI!it might be A SET-UP.wataipiga danadana weeeeeeeeee mpaka tutasahau mdogo mdogo

angalia sasa ulipoanza KULIKOROGA........
......isitoshe liyumba ametumia hizo hela na madada zetu...
.....kwa hiyo hela ALICHUKUA,AU HAKUCHUKUA?au yeye alichukua kidogo za kutumia na dada zako?na hizo zingine ZIMEENDA WAPI?jaribu kujustfy hata kwa suspuscious theories!pesa ya EPA walau watu 'wanahisi' ilikwenda wapi,na wewe tuambie sasa!

....................sasa angalia unavyomalizia post yako.......
siwezi kuamini hata siku moja liyumba na kweka wamechukua $200m, nina imani kabisa zaidi ya $150m zimechukuliwa na serikali(ccm)

ANYWAYS,TWENDE TU HIVYO HIVYO!tutafanyeje
 
Hakimu Lema amekubaliana na upande wa utetezi kuwa kweli hati ya mashtaka ina makosa na kwa maana hiyo imefutwa so inasubiriwa hati mpya toka upande wa mashtaka.

Watabaki chini ya ulinzi wa kova hadi iletwe hati mpya.
hilo ni goli la kwanza la ushindi wa mawakili wa utetezi.
tusubiri yatakayojiri wakishafungua hayo mashtaka mapya.

Madudu nchi hii hayatoisha mpaka mfumo ufumuliwe na kusukwa upya. Tunaweza ila hamna nia tu!
 
hao hao tumewasomesha kwa kodi zetu mpaka majuu huko kila angle ya dunia imradi wapate elimu kumbe wanaenda kutalii na kuzunguka zunguka na kupiga misere miingi kwenye majiji ya watu utendaji kazi ni wa kimazoea tu yaani tunakazi.

Hawa ni hao hao waliosomea hapa nyumbani ... mliowapeleka huko majuu kwani walirudi ... si walishajilipua! kalaghabao .... lol!!
 
Kwa kweli sitaki kuamini kile ambacho kimekuwa kikinikereketa siku zote kuwa Mahakama zetu, mahabusu zetu na magereza zetu ni kwa ajili ya walalahoi na si vigogo.

usione ajabu MJ1,
Tatizo ni kuwa huyo mlalahoi hakuna wa ku scrutinise hata charge sheet kuona kama iko defective na kuomba mahakama kuitupilia mbali angalau akapumue kidogo wakati kazi inafanyika kuirekebisha.Vigogo wanao uwezo kuajiri wakili na wakili atatafuta kila njia kumpunguzia mteja shurba na hatimaye kumwokoa kabisa asiingie kwenye mkono mrefu wa sheria.
 
Mseminari Liyumba ameachiwa huru punde na mahakama baada ya kujiridhisha kuwa charge waliyoileta mahakamani ni batili, lakini punde vijana wa Hosea wameshamchukua Liyumba na sasa hivi yuko PCCB Makao Makuu...

Wajuzi wa mambo nendeni Kisutu na ktk makorido tupatieni latest

Hii habari haijakamilika ... inaelea elea tu!!!
 
Hawa ni hao hao waliosomea hapa nyumbani ... mliowapeleka huko majuu kwani walirudi ... si walishajilipua! kalaghabao .... lol!!

walisoma hapa wakaenda majuu kuchukua masters na wengine Phd
 
Alipokamatwa nilisema there was a 'fault charge sheet ab initio' yaani kosa la msingi katika kuandaa shitaka hili tangu mwanzo. Kitu muhimu kwangu sio Liyumba kuwa is clean, bali haki zao za msingi kwenye kosa wanaloshitakiwa nalo ambalo sio kosa kweli.

Niliposema hayo, nilishutumiwa sana na kuitwa fisadi. Niliyoyasema sasa yanaanza kutimia, bado kina Mramba pia kesi itatupwa!.

Kwa kina Liyumba ilihitaji tuu simple logic, majengo pacha yalipitishiwa budget ya awali kugharimu bilioni 90. Kazi ilipoanza gharama zikaongezeka mpaka zilipofikia.

Walipowashitaki, wamewashitaki kwa gharama zote tangu mwanzo na sio zile za zida tuu.

Nikasema, angetokea mwanasheria makini, akatafuta hizo fedha zote za thamani ya majengo pacha, serikali ikarudishiwa na majengo pacha yakageuka mali ya Liyumba!.

Kosa la msingi ni kuwashitaki wakina Liyumba kusababisha hasara ya thamani ya kazi iliyofanyika na majengo yanaonekana, huku madai yakionyesha yote ni haswara tupu as if hakuna kilichofanyika.

Usahihi wa madai ya serikali ungekuwa kama ifuatavyo.

1. Kwanza angetafutwa mthamini kuyathamini hayo majengo yametua gharama halisi za kiasi gani.
2. Baada ya kupata gharama halisi, unatoa zile gharama zilizolipiwa.
3. Tofauti ya gharama halisi na kilicholipiwa ndio hasara/10% ama ulaji.

Kesi inge-base hapo angalau ingekuwa kesi ya ukweli.

Na wakiachiwa kama wakili wao mzuri, waifungulia serikali kesi na wanalipwa fidia.

Nilisema PCCB wana kiherehere cha kufungua kesi kwa papara ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao ambayo ilishuka sana.

Hii serikali yetu ni ya ajabu sana, wakati wa rada, kelele zikapigwa ni ya kijeshi na haina maslahi kwa taifa. serikali ilitia pamba masikioni. leo rada haifanyi kazi, pesa zimeliwa na taifa limekula hasara.

Hata huko kumtafuta Vithlani sio kwa kesi ya bei ya rada ambayo tumelizwa, bali kwa kutosema ukweli kwa PCCB.

Ndege ya rais watu wamepiga kelele, Bwana Mapesa, John Cheyo akatoa mpaka ushahidi wa website gharama ya ndege ni nusu ya bei tunayotaka kuuziwa. Serikali ilitia pamba masikioni na kuendeleza manunuzi, ajenti ni huyo huyo Vithlani na Somaiya wake.

Deal ya rada imebumbuluka kwa sababu BAE shirika la serikali na walioibumbulua ni waingereza wenyewe kupitia SFO. Ya Gulf Sream ni kimya...ulaji wa kiulaini.

"Hii ndio Tanzania yetu, Kikwete Rais Wetu na CCM Chama Chetu''.

Tanza..nia.. Tanzania...,.
 
Mkuu pasco tulikuelewa vibaya hapo mwanzoni ila utuwie radhi.
Ni kweli mwelekeo wa kesi hizi ni msaada kwa washtakiwa kukwepa mkono wa sheria.

Maajabu mengi yapo mbioni
 
Wamesharudishwa mahakamani kusomewa hati mpya sijui mashtaka yatakuwa yale yale?

Asante mkuu endelea kutuhabarisha. I hope dhamana itakuwa si ya ukandamizaji kama awali. Na hakika hii kesi watashinda!!!Hivi serikali imejiandaa vipi kulipa fidia ya kesi zote kubwa hivi ambazo wamefungua na hawana competence ya ku-deal nazo??? Halafu nyingi kwa mpigo???? Wakaazime wanasheria nje ya nchi ""Lawyers grants".
 
hao hao tumewasomesha kwa kodi zetu mpaka majuu huko kila angle ya dunia imradi wapate elimu kumbe wanaenda kutalii na kuzunguka zunguka na kupiga misere miingi kwenye majiji ya watu utendaji kazi ni wa kimazoea tu yaani tunakazi.

Fidel, kama Watanzania au binadamu tungekuwa hatufanyi makosa katika kazi zetu basi dunia hii ingekuwa tofauti kabisaandaa mashtaka ni binadamu kama wewe na mimi...kama wamekosea ni wazi kuwa hawakufanya hivyo makusudi. Utambue kuwa makosa kama haya ya akina Liyumba ni mapya hapa Tanzania. Lets not blame them maana sisi watz tunaongoza kwa kuangalia vibanzi na kusahau boliti katika macho yetu.
 
...........wakati wa rada, kelele zikapigwa ni ya kijeshi na haina maslahi kwa taifa. serikali ilitia pamba masikioni. leo rada haifanyi kazi, pesa zimeliwa na taifa limekula hasara...................,.

Ndege ya rais watu wamepiga kelele, Bwana Mapesa, John Cheyo akatoa mpaka ushahidi wa website gharama ya ndege ni nusu ya bei tunayotaka kuuziwa. Serikali ilitia pamba masikioni na kuendeleza manunuzi, ajenti ni huyo huyo Vithlani na Somaiya wake....,.

LOL!this is so IRRITATIVE
 
At times mimi nachoka kabisa na mambo yanavyokwenda hii nchi.
Kila kukicha nachanganyikiwa na habari zinazokuja. Vitu vinakuwa ndivyo sivyo.
So hao pccb hawana wataalamu wa sheria...
Thanks for the habari wenye dataz zaidi wazimwage
Bw. AL asipewe useminari ikiwa yeye hajawi kuwa mseminari, hofu yangu kubwa ni kuwa anapewa utukufu asiostahili.

Pili bw. Liyumba anayo haki ya kikatiba ya kupata dhamana ila anachotakiwa kukifuata ni utaratibu uliowekwa kisheria wa namna bora ya kupata dhamana. Kimsingi kwa hili anatakiwa kujilaumu yeye kwa kutofuata taratibu za kupata dhamana.

Hata hivyo ni maoni yangu kuwa Bw AL atakapobainika kuwa makosa anayotuhumiwa nayo kama yatabainika basi apewe hukumu kali ili iwe mfano kwa viongozi wengine wanaoaminiwa na serikali.

mbelakisa
 
Lakini sijui kwanini Hosea hataki kuachia ngazi.

Credibility ya PCCB itarudi pale tu atakapoamua kuachia ngazi na kuchaguliwa mtu makini asiye na kashfa. Rais kumuacha Hosea pale PCCB ni ushahidi tosha kwamba Rais hayuko serious na mapambano dhidi ya rushwa. Au kuna kitu mkuu wetu wa nchi anajaribu kuficha, ndio maana watu kama akina Hosea, Mattaka na wengine wanaoboronga wanaachwa katika nafasi zao.

Nadhani umefika muda sasa, Rais aache kubeba watu ambao ni mizigo na wanazidi kulizika taifa letu katika lindi la umasikini wa kutupwa. Kushindwa kutengeneza hati ya mashtaka sahihi katika kesi muhimu kama hizi, ni ushahidi tosha wa ubovu wa PCCB. A major overhauling is needed.

Haingii akilini kwamba watu karibia wote wenye hizi "grand" cases wanabadilishiwa mashtaka kila siku.

Something is very wrong. Au tunapigwa kiini macho hapo?
 
mseminari liyumba ameachiwa huru punde na mahakama baada ya kujiridhisha kuwa charge waliyoileta mahakamani ni batili, lakini punde vijana wa hosea wameshamchukua liyumba na sasa hivi yuko pccb makao makuu...

Wajuzi wa mambo nendeni kisutu na ktk makorido tupatieni latest
hivi sheria inasemaje walalamikaji wanapokosea hati ya mashtaka???

Naomba kuelimishwa sheria hapooo...
 
Alipokamatwa nilisema there was a 'fault charge sheet ab initio' yaani kosa la msingi katika kuandaa shitaka hili tangu mwanzo. Kitu muhimu kwangu sio Liyumba kuwa is clean, bali haki zao za msingi kwenye kosa wanaloshitakiwa nalo ambalo sio kosa kweli.

Niliposema hayo, nilishutumiwa sana na kuitwa fisadi. Niliyoyasema sasa yanaanza kutimia, bado kina Mramba pia kesi itatupwa!.

Kwa kina Liyumba ilihitaji tuu simple logic, majengo pacha yalipitishiwa budget ya awali kugharimu bilioni 90. Kazi ilipoanza gharama zikaongezeka mpaka zilipofikia.

Walipowashitaki, wamewashitaki kwa gharama zote tangu mwanzo na sio zile za zida tuu.

Nikasema, angetokea mwanasheria makini, akatafuta hizo fedha zote za thamani ya majengo pacha, serikali ikarudishiwa na majengo pacha yakageuka mali ya Liyumba!.

Kosa la msingi ni kuwashitaki wakina Liyumba kusababisha hasara ya thamani ya kazi iliyofanyika na majengo yanaonekana, huku madai yakionyesha yote ni haswara tupu as if hakuna kilichofanyika.

Usahihi wa madai ya serikali ungekuwa kama ifuatavyo.

1. Kwanza angetafutwa mthamini kuyathamini hayo majengo yametua gharama halisi za kiasi gani.
2. Baada ya kupata gharama halisi, unatoa zile gharama zilizolipiwa.
3. Tofauti ya gharama halisi na kilicholipiwa ndio hasara/10% ama ulaji.

Kesi inge-base hapo angalau ingekuwa kesi ya ukweli.

Na wakiachiwa kama wakili wao mzuri, waifungulia serikali kesi na wanalipwa fidia.

Nilisema PCCB wana kiherehere cha kufungua kesi kwa papara ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao ambayo ilishuka sana.

Hii serikali yetu ni ya ajabu sana, wakati wa rada, kelele zikapigwa ni ya kijeshi na haina maslahi kwa taifa. serikali ilitia pamba masikioni. leo rada haifanyi kazi, pesa zimeliwa na taifa limekula hasara.

Hata huko kumtafuta Vithlani sio kwa kesi ya bei ya rada ambayo tumelizwa, bali kwa kutosema ukweli kwa PCCB.

Ndege ya rais watu wamepiga kelele, Bwana Mapesa, John Cheyo akatoa mpaka ushahidi wa website gharama ya ndege ni nusu ya bei tunayotaka kuuziwa. Serikali ilitia pamba masikioni na kuendeleza manunuzi, ajenti ni huyo huyo Vithlani na Somaiya wake.

Deal ya rada imebumbuluka kwa sababu BAE shirika la serikali na walioibumbulua ni waingereza wenyewe kupitia SFO. Ya Gulf Sream ni kimya...ulaji wa kiulaini.

"Hii ndio Tanzania yetu, Kikwete Rais Wetu na CCM Chama Chetu''.

Tanza..nia.. Tanzania...,.
.Nakupenda kwa moyo wote.... nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana.Nilalapo nakuota wewe niamkapo ni heri mama wee.Tanza..nia Tanzania.............................
 
Back
Top Bottom