Imebaki kiasi gani kupata chopa?Tofautisha michango ya wananchi na Mafisadi hiyo 5 bilion si anatoa nani pekee yake?then kesho watanzania tunamlipa na faida juu!
Salaam wakuu!
Naomba kumshauri mwenyekiti wa M4C bwana Godbless Lema kuwa ubabe hauna tija kwa CDM. Kauli kwamba "makampuni ya simu wakidhubutu kutuhujumu tutapita mtaani na kukusanya card zao na kuzitumbukiza chooni"!! Huu ni ujuaji. Cdm ni chama makini kinachochipukia kinatakiwa ustaarabu na maadili kukijenga chama na kukifikisha kule watanzania wanakotaka. Kutumia lugha na kauli za kujikweza kabla hata ya kukamata dola inanipa mashaka sana kama mwanachama. Ikiwa kama hawa ndio mawaziri tunaowategemea, mbona hawatakuwa na tofauti na hawa wa CCM tulionao!!
Nawatakia kila la heri.
Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania.
Tatizo la CDM kwa sasa ni kuset priorities. Huwezi kuniambia kama kweli ni akili kwa chama kununua magari ya 5bn wakati bado kina mambo mengi ya msingi ya kufanya. Kumbuka mpaka sasa CDM hakiwezi kujiendesha chenyewe, kinategemea sana donations. Wangeangalia kwanza njia mbadala za kukuza kipato. Nimewadharau sana kwa kitendo cha kuwa na mpango wa kununua magari ya 5bn!!! Tena Lema anasema kabisa zikipatikana zaidi wananua na helkopta, na tayari ameshaichagua hiyo helkopta.
Kuna njia nyingi sana za kuwafikia wananchi, siyo lazima kwa magari, helkopta na pikipiki. Serikali yetu imejitahidi sana kukuza mawasiliano. Wangeitumia vizuri hii advantage ya improvement ya communication sector ambayo ni cost effective kuliko kutegemea njia za kizamani kuwafikia wanachi.
Naamini kama ni badiliko yanaletwa na wananchi wenyewe wa eneo husika, sidhani kama ni lazima mchaga atoke moshi na Arusha aje kunishawishi mimi mmakonde nibadilike. Hii movement yao naona ni njia tu ya loserz kama Dr Slaa na Lema ya kujiongezea kipato!!
Katika hali iliyotarajiwa na wengi michango hiyo imeonekana ni mradi wa viongozi wa Chadema, ebu waambieni wananchi taingia muanze kuwachangisha watanzania mmeishawapa mchanganunuo wa matumizi yenu kuna mfuasi wa Chadema yeyote anajua matumizi ya ruzuku ya Chadema.
Lema anasimama anasema nataka bilioni tano nikanunue Chopa mbili na magari 100 unataka ukanune Chopa wakati ofisi mmepanga vyumba vitatu pale Kindondoni mtaa Ufipa.
Lema, Mbowe, Slaa, tuone michanganuo ya michango mnayowachangisha wananchi wambieni michango imefanya a.b.c siyo kukaa kimya

Bila shaka una matatizo ya mtindio wa ubongo,zitto ameingiaje hapa kwenye hii mada.pombe zakunywa ukubwani bwana