LIVE:Jukwaa la Maoni ya katiba Mpya SUMBAWANGA MJINI

B.Panther

Member
Jun 5, 2012
52
4
Katika harakati zangu,leo nimebahatika kuwa Manispaa ya Sumbawanga na kuhudhuria Jukwaa la maoni ya Katiba Mpya,Stay tuned here for more updates.
 

Attachments

  • Jukwaa.jpg
    Jukwaa.jpg
    202.7 KB · Views: 59
  • Alfaz.jpg
    Alfaz.jpg
    133.9 KB · Views: 65
MKUU wa Wilaya anafungua Mkutano,Wananchi ni wengi kiasi.Mkutano unaanza saa 3 mpaka saa Sita.
 
Naona vikundi vikundi vya watu kajidalidiana mambo mbali mbali,Nacho kishangaa katika vikundi hivi,naona kuna dalili za itikadi za Kidini.Nawatambua kwa Mavazi walio vaa nikimaanisha Waislam.Sijui wanajipanga kwa lipi.Nawakilisha.
 
MWAMBIENI huyo Mkuu wa mkoa akae mkao wa kudhalilika, maana watasimama watu hapo waseme wazi kuwa Post ya Mkuu wa Wilaya ifutiliwe mbali...
Katika mikutano yote ya katiba niliyowahi kuhudhuria hilo lazima lisemwe.
Nimesikia leo asubuhi serikali imeanza kupata wasiwasi na mapendekezo hayo, wanasema kuwa watoa maoni waache kutumiwa na wanasiasa!... ha ha haaa, maji ya shingo hayo!
 
Halafu kuna maeneo wakazi wanajipendekeza kuwachinjia kuku hao watu wa maoni, tafadhali msifanye kosa hilo, maana hao wako full mahela.
Kijijini kwangu watu walichangishwa eti kupata chakula na vinywaji vya watu wa maoni ya katiba!...my hairs!
 
hii kitu mimi sielewi.Zanzibar walifanya hivi na wakapata katiba yao.Leo hii Tanzania tunafanya na kuna wawakilishi kutoka Zanzibar.Mimi nilidhani hapa tunachanganyana.Zanzibar wamefanya wenyewe.Tanzania tunafanya wote,Why?.Kuna haja ya kuwa na Serikali 3 au serikali Moja hapa...
 
hii kitu mimi sielewi.Zanzibar walifanya hivi na wakapata katiba yao.Leo hii Tanzania tunafanya na kuna wawakilishi kutoka Zanzibar.Mimi nilidhani hapa tunachanganyana.Zanzibar wamefanya wenyewe.Tanzania tunafanya wote,Why?.Kuna haja ya kuwa na Serikali 3 au serikali Moja hapa...
Aisee,
Mmevunja lini Muungano?
 
Kuna kina Mama wa Kiislam nawaona Mbele yangu.Kweli wamejipanga na shughuli hii.Inapendeza.Wako na vikaratasi vina maandishi fulani wanakumbushana,Inaelekea walikuwa na Darasa Maalumu ya hili na nini waje waseme.Nasubiri watakacho kiwakilisha NIWAJUZE WANA JF.
 
asilimia 95 ya wananchi waliotoa maoni yao katika kata ya Uru Kusini tarehe 12.10.2012 walisema nafasi za wakuu wa wilaya na mikoa hazina tija ziondolewe.Naunga mkono aliyesema mkuu wa wilaya aondoke kwenye huo mkutano kwani ataumbuliwwa sasa hivi.
 
kunagawiwa fomu.Kwa wasio taka kuongea watazitumia kujaza maoni yao.
Kwa wanao taka kutuma maoni kwa njia ya sms,Andika Jina,Kazi,Mahali unapoishi,Tuma maoni yako kwenda namba 0715 / 0787/ 0767/ 0774 081 508
 
Mama wa Kiilslam anawakilisha kuomba mahakama ya khadhi pia anaomba vazi la ijabu liingizwe katiba na litambulike kama vazi la heshima jwa wanawake...
 
Naona vikundi vikundi vya watu kajidalidiana mambo mbali mbali,Nacho kishangaa katika vikundi hivi,naona kuna dalili za itikadi za Kidini.Nawatambua kwa Mavazi walio vaa nikimaanisha Waislam.Sijui wanajipanga kwa lipi.Nawakilisha.

Achana nao hawa tushawachoka, usije ukashangaa wanataka kwenye katiba mpya kuwe kuna kipengere kinachoifanya ijumaa iwe siku ya mapumziko
 
Kuna Mama ameomba Ijumaa iwe siku ya Mapumziko kama Jumamosi na Jumapili.Amesema wasabato ni wachache lakini wanapumzika Jumamosi,Waislam ni wengi lakini hakuna Mapumziko Ijumaa.So Ijumaa isiwe siku ya kazi...
 
Kuna Siter wa RC anaombakuwe na Muda wa Kikomo Bungeni.Miaka 10 kama kwa Rais na Rais aondolewe kinga ya Mashtaka.Akifanya fyongo,ashtakiwe kama waahalifu wengine...
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Kuna Mama anahoji,Kwa Nini Waislam wanataka Mahakama ya Khadhi?,kwani kama ni kesi za Ndoa,mbona Wakristo wana huwa wanatatua matatizo ya Ndoa kwa kutumia Wachungaji na Mapadri?
 
Kuna Mzee anachangia,anaomba Elimu kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita iwe bure.Pili Mbunge anapokatiwa rufaa na kupokonywa ubunge,Mbunge wa pili ndio apewe ubunge kuepuka gharama za uchaguzi sizizo na sababu.
 
Wanachi wawe na uwezo wa kuwaondoa Wabunge na Madiwani pale ambapo hawata onyesha kuwajibika ipasavyo...
 
Back
Top Bottom