Live from Dodoma: Wagombea CCM nafasi mbalimbali 2012

Majina rasmi yatasomwa muda si mrefu jopo la paparazi wapo hapa wakisubiri tamko la NAPE NNAUYE

Kuna majina yametajwa kweli katika ile habari iliyotangulia hapa yamekatwa kweli, ila kwa kulinda hadhi ya Forum MODS Funga uzi huo una habari nyingine si hakika sana inawezekana chanzo cha gazeti tajwa hapo kilipata habari za kiintelijensia ambazo nyingine hazikuwa sahihi.

Ntakupa mfano Jina la DR.ANTHONY DIALLO Naliona hapa katika list na atagombea Mwanza


GR IS LIVE SUBIRI UP DATE YA MAJINA KAMILI SOON


ADIOS

Dondoo Muhimu

  • Sura nyingi Mpya zatawala
  • Vigogo wengi wala mweleka
  • Mkono, Mpina, Filikunjombe, Derefa OUT
  • Diallo kukabana koo na Mabina
  • Chegeni apeta, Kamani naye kugombea Uenyekiti wa Mkoa wa Simiyu
  • Lowasa yumo
  • Ridhwani na Salma hawana wapinzani
  • Gachuma, Mathayo, Makongoro wamo Mara
  • Le Mutuz kugombea Dar
  • Chenge hana mpinzani Bariadi
  • Nagu na Sumaye kutoana jasho Hanan'g
  • Karamagi Aibuka upya kusaka Uenyekiti wa Wilaya huko Kagera
  • Bulembo, Martha Mlata na Cpt Balongo Kuwania M/Kiti Wazazi Taifa
  • Ngoma Nzito Viti 3 Wazazi Bara wamo Manyanya, Tizeba, Zungu, Kawawa na Nyawazwa
  • Mwendesha Mijadala ya TV Mayrose kupimana Ubavu na Kilango VS Sophia Simba UWT Taifa


FAMILIA YA KIKWETE IMAMUA KUBEBE CCM MGONGONI?


3. Ndugu, Mohamed Mrisho KIKWETE (57) - pia anagombea inaonekana ni MDOGO WA KIKWETE !!!
 
Majina rasmi yatasomwa muda si mrefu jopo la paparazi wapo hapa wakisubiri tamko la NAPE NNAUYE

Kuna majina yametajwa kweli katika ile habari iliyotangulia hapa yamekatwa kweli, ila kwa kulinda hadhi ya Forum MODS Funga uzi huo una habari nyingine si hakika sana inawezekana chanzo cha gazeti tajwa hapo kilipata habari za kiintelijensia ambazo nyingine hazikuwa sahihi.

Ntakupa mfano Jina la DR.ANTHONY DIALLO Naliona hapa katika list na atagombea Mwanza


GR IS LIVE SUBIRI UP DATE YA MAJINA KAMILI SOON


ADIOS

Dondoo Muhimu

  • Sura nyingi Mpya zatawala
  • Vigogo wengi wala mweleka
  • Mkono, Mpina, Filikunjombe, Derefa OUT
  • Diallo kukabana koo na Mabina
  • Chegeni apeta, Kamani naye kugombea Uenyekiti wa Mkoa wa Simiyu
  • Lowasa yumo
  • Ridhwani na Salma hawana wapinzani
  • Gachuma, Mathayo, Makongoro wamo Mara
  • Le Mutuz kugombea Dar
  • Chenge hana mpinzani Bariadi
  • Nagu na Sumaye kutoana jasho Hanan'g
  • Karamagi Aibuka upya kusaka Uenyekiti wa Wilaya huko Kagera
  • Bulembo, Martha Mlata na Cpt Balongo Kuwania M/Kiti Wazazi Taifa
  • Ngoma Nzito Viti 3 Wazazi Bara wamo Manyanya, Tizeba, Zungu, Kawawa na Nyawazwa
  • Mwendesha Mijadala ya TV Mayrose kupimana Ubavu na Kilango VS Sophia Simba UWT Taifa

WOW Another Kikwete...


Ndugu, Mwanaisha Halfani KIKWETE 55 (1957
 
Katika hili CCM chajiingiza zaidi matatani dhidi ya wapiga kuhusu janga la taifa UFISADI na uwezo wa chama hiki kuweza kujitenga nayo kweupe mchana. What a stronger political amunition to exploite to the maximum at a time oppotune .

Wale MAPACHA Watatu waUFISADI waliokua wajipime kuondoka chamani kwa kashfa nzito dhidi ya umma wa Tanzania sasa WAMEPIMWA NA CCM na kupandishwa vyeo vizito kuwa ni Makamanda wa kukipigania chama hiki kwa mtaji wa fedha za Uswisi.

Kambi ya upinzani, hoja nzito ajabu hiyo kutumika kwenye uchaguzi ujao dhidi ya Magamba.
 
Vita CCM

NEC YATANGAZA WAGOMBEA, MAWAZIRI WACHUANA KUNDI LA KIFO, YAWATOSA LONDA, MKONO, FAMILIA YA KIKWETE YAINGIZA WATATU

Mwandishi Wetu, Dodoma | Mwananchi

HALMASHAURI Kuu ya CCM (Nec), imetangaza majina ya wagombea walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho, huku ikionyesha kuwa uchaguzi huo utakuwa na mchuano mkali.

Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.
Mchuano mkali unaonekana kuwapo kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec Mkoa wa Manyara ambako Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye anachuana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.

Mchuano huo unatarajiwa kuwa mkali katika nafasi ya uenyekiti kwenye baadhi ya mikoa kutokana na kupitishwa kwa majina ya makada wake maarufu. Mwanza ni miongoni mwa mikoa hiyo kwani Nec imepitisha jina la Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo ambaye atachuana na Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo.


Makada hao watapata ushindani mkali kutoka kwa Zebedayo Athumani, Joseph Yaredi na Mashimba Hussein Mashimba.


Dar es Salaam nako kunatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwani mwenyekiti wa sasa, John Guninita atachuana na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Makao Makuu ya CCM, Matson Chizzi na kada mwingine, Ramadhan Madabida. Godfrey Mwalusamba, Harold Adamson na Paul Laizer wanawania nafasi hiyo mkoani Arusha.


Vita nyingine kali ipo kwenye Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT), ambako Mwenyekiti wa sasa, Sofia Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto anachuana na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalumu, Mayrose Majige.


Katika Jumuiya ya Wazazi, Mkono ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo ametupwa na kuwaacha Abdallah Bulembo, Martha Mlata na kada wa siku nyingi, John Barongo kuchuana.


Awali, Mkono alikatwa jina lake na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo na kutangaza hali ya hatari akisema asipopitishwa patachimbika. Jina lake lilirejeshwa na Kamati ya Usalama na Maadili kabla ya kukatwa tena na Kamati Kuu.


Alipoulizwa jana kuhusu kuondolewa katika kinyang'anyiro hicho, Mkono alisema: "Nimekubaliana na uamuzi wa chama na nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM. Nimelelewa na kukulia CCM na
nitaendelea kubaki CCM nikiwa mwanachama mtiifu."


Katika Jumuiya ya Vijana (UVCCM), mchuano mkali unaonekana kuwa katika nafasi ya makamu mwenyekiti kwani mmoja wa wagombea waliopitishwa, Paul Makonda anaaminika kuwa na nguvu kubwa kutoka katika kundi la wabunge na mawaziri wapambanaji wa ufisadi. Makonda anawania nafasi hiyo pamoja na Mboni Mhita na Ally Hapi.


Nafasi ya Mwenyekiti UVCCM inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Mshamu Abdallah.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa atachuana na Dk Salash Toure na Nanai Kanina kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Monduli.

Wagombea wa ‘kundi la kifo'
Vigogo kadhaa wamepitishwa kuwania nafasi 10 za Nec, wakiwamo baadhi ya mawaziri na viongozi wa juu wa chama hicho.


Miongoni mwao ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

Wengine ni Katibu wa Fedha na Uchumi CCM, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano, Stephen Wassira, Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana, Dk Fenela Mukangara na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela.

Kwa upande wa Zanzibar, nafasi 10 za Nec kupitia kapu zinawaniwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan.


Katika orodha hiyo wamo, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa zamani wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Mohamed Seif Khatib, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalami Issa Khatib.

Katika uteuzi huo wa wagombea, majina matatu ya wagombea kutoka katika familia ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete yamepitishwa.


Waliopitishwa ni pamoja na mkewe Salma Kikwete ambaye anakuwa mgombea pekee katika nafasi ya ujumbe wa Nec Lindi Mjini na Ridhiwan Kikwete ambaye pia ni mgombea pekee wa nafasi hiyo katika Wilaya ya Bagamoyo.

Mbali ya hao, Nec pia imepitisha jina la Mohamed Mrisho Kikwete kuwania nafasi ya uenyekiti wa Wilaya ya Bagamoyo.

Vigogo watemwa
Nec imewatema vigogo kadhaa, baadhi yao ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Azim Premji na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo-Swai ambaye alikuwa anagombea ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hai na kada wa siku nyingi, Salum Londa.

Pia wamo wabunge, Sarah Msafiri, Munde Tambwe, Deo Filikunjombe na Victor Mwambalaswa.Wengine waliotemwa ni Hussein Bashe na hasimu wake mkubwa kisiasa Dk Hamis Kigwangalla, Jamali Kassim, Anthony Mavunde na Emmanuel Nzungu, ambaye aliomba kugombea Uenyekiti Wilaya ya Ilemela, Mwanza.

Mgeja chupuchupu
Mwenyekiti wa sasa wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja aliponea chupuchupu kutemwa baada ya Nec kurejesha jina lake kwenye orodha ya wagombea lililokuwa limeondolewa na vikao vya awali.Taarifa za kuondolewa jina la Mgeja zilivuja tangu juzi wakati kikao cha Kamati Kuu kilipoketi ikidaiwa ni kutokana na malumbano kati yake na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.


Inadaiwa wakati wa kujadiliwa Mgeja, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alitoka kwenye kikao na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na kumwachia kiti Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa.

Baada ya mjadala mrefu wa kumtetea Mgeja kwamba hakutendewa haki, Msekwa alifikia uamuzi wa kurejesha jina.

"Baadhi ya waliomtetea ninaokumbuka ni Dk Makongoro Mahanga na Peter Serukamba, lakini wakati wa mjadala wa Mgeja, Mwenyekiti (Kikwete) na Nape walikwenda chemba, kiti akaachiwa Msekwa," kilisema chanzo chetu.

Awali, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale - Mwiru aliituhumu Kamati Kuu kwamba imevunja kanuni za uchaguzi kwa kuteua majina zaidi ya matatu kwenye nafasi moja.


Hata hivyo, inadaiwa Msekwa alimsomea kanuni moja baada ya nyingine zinazohusu uteuzi hali iliyoonyesha kama kumweka darasani na hatimaye ikabainika hakuna kanuni iliyovunjwa.Hoja hiyo ilitokana na baadhi ya mikoa kwenye nafasi moja kusimamisha wagombea zaidi ya watatu kama nafasi ya mwenyekiti mkoa wa Mwanza.


Hatua hiyo inadaiwa inalenga kuondoa matokeo ya kupanga kwa baadhi ya wagombea na kwamba, kwa hali hiyo mshindi hawezi kupatikana kwa mzunguko wa kwanza.


Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba anadaiwa kushambulia mtandao
uliokuwa umejipanga na kuweka wagombea wao hata kama hawana sifa."Yule mzee (Makamba) amewachana-chana vibaya, anasema hapa tunasajili timu, kama majina hayafai yaondolewe," kilidokeza chanzo na kuongeza kwamba hoja hiyo iliungwa mkono na kada mkongwe wa chama hicho, Mzee Peter Kisumo.
 
Waandishi Wetu habari zao sio SAWA; MJENA Mara NDANI MJEMA Mra MJEMA Nje... ???

Tunavurugwa akili habari zao sio Sawa... Kila Mwandishi inaonekana anapata dodoso TOFAUTI na Mwingine...
 
Sijui wangapi wetu wamesoma hayo majina kwa jicho la pili.....Wengi wa wagombea wa CCM ni wa umri wa kati ya miaka 50 na 6o average 40s and very few 30s....Katika kila group japo group la vijana wamekwepa kuweka umri sijui kwanini....May be ungekuta wengi 35 plus and quite few 20s and below 35.

What does this tell? Nimejaribu ku-pick majina ya hao vijana wadogo (nje ya kundi la vijana) wengi ni wale wenye relatives ama wazazi nafasi ya juu another big problem to the survival of the party na utaona mikoa ambamo CDM wanakubalika kwa sana umri wa wagombea ndiyo hauvuki 50s hali ni mbaya sana Manyara, Arusha, Kilimanjaro meaning the party is already dead there!

I wonder what would make CCM to stay for another atleast 10 years!

mimi binafsi sifurahi hii hali kwani tungepata vyama viwili vitatu vikubwa vikashindana katika demokrasia nchi itasonga mbele kwa haraka sana kuliko kutengeneza another CCM kwa jina tofauti...

As a matter of fact hii hali ni nzuri katika kujijenga upya kama nchi lakini ningeomba tuanze kufikiria jinsi ya kujenga vyama vingine vya siasa baada ya kuiaga rasmi CCM maana kwa hali ilivyo ndiyo kwaheri.....
 
I wonder what would make CCM to stay for another atleast 10 years!

Vote splitting. CHADEMA vote will be split by CCM campaigning for ZZK that's if the constitution allows agewise
 
Vote splitting. CHADEMA vote will be split by CCM campaigning for ZZK that's if the constitution allows agewise

Unfortunately JF imeshalisaidia hilo tatizo wengi wako prepared na ikitokea impact itakuwa insignificant kwani kwa sasa vijana wengi wapo upande wa CDM not because of him being there ila kwakua alionyesha njia nao wakaona its possible....Its done once and for all! He is not that much stupid maana naye anajua he has a long way to go siyo mzee yeye na wala sikijana tena kama ilivyokuwa hapo mwanzo so risks loving character inaendelea kupungua na maturity inaongezeka.
 
THURSDAY, SEPTEMBER 27, 2012

shy-ccm.jpg


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Bhanji amefanikiwa kuwa mmoja wa wagombea 10 waliopitishwa kati ya 31 na Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM-NEC kugombea Ujumbe wa Halmashauri kuu ya CCM NEC Tanzania bara. Katika kinyang'anyiro hicho Mh. Shy-Rose Bhanji anapambana na baadhi ya mawaziri na viongozi wa juu wa chama hicho.
 

Congrats Shy-Rose; Kama ni wengine wasiokuwa na MOYO MGUMU kama wewe wangeisha JIACHIA

ZAMANI... Sasa hivi KISIASA Umejengeka IPASAVYO... Nakutakia Mafanikio MENGI...

* Sijui yule Hilderbrand Shayo - YUKO WAPI? Tangu kapigwa chini UBUNGE wa EAST AFRICA

Kapotea; Yeye ilikuwa ni sio Siasa ni kutafuta ULAJI?
 
Shyrose has nary shied away from fighting for what she believes in. Again, I admonish you to think about the other side of the coin--family life.
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Taifa alishasema kuwa alikuwa anaamini kuwa moja ya chimbuko la ufisadi nchini mwetu ni mgongano wa maslahi [CONFLICT OF INTEREST] kati ya viongozi ambao ni wanasiasa/viongozi wa serikali na pia wanajihusisha na biashara.

Ili kukomesha hii conflict of interest ambayo inazaa ufisadi aliahidi kuleta sheria bungeni ambayo ingetenganisha ufanyaji biashara na siasa kwa viongozi!!

Mpaka sasa hilo halijatendeka na imebakia kuwa ni ahadi nyingine ambayo ilikuwa na umuhimu wa peke katika mustakabali wa nchi ambayo mpaka sasa imekuwa ni ndoto!!

Je kuna ishara yeyote ya kuonesha kuwa Kikwete atatimiza ahadi hiyo katika utawala wake kwa kutunga sheria ya kutenganisha siasa na biashara kwa viongozi kutokana na teuzi zilizofanywa na chama chake?
 
Back
Top Bottom