Live from Dodoma: Wagombea CCM nafasi mbalimbali 2012

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Majina rasmi yatasomwa muda si mrefu jopo la paparazi wapo hapa wakisubiri tamko la NAPE NNAUYE

Kuna majina yametajwa kweli katika ile habari iliyotangulia hapa yamekatwa kweli, ila kwa kulinda hadhi ya Forum MODS Funga uzi huo una habari nyingine si hakika sana inawezekana chanzo cha gazeti tajwa hapo kilipata habari za kiintelijensia ambazo nyingine hazikuwa sahihi.

Ntakupa mfano Jina la DR.ANTHONY DIALLO Naliona hapa katika list na atagombea Mwanza


GR IS LIVE SUBIRI UP DATE YA MAJINA KAMILI SOON


ADIOS

Dondoo Muhimu

  • Sura nyingi Mpya zatawala
  • Vigogo wengi wala mweleka
  • Mkono, Mpina, Filikunjombe, Derefa OUT
  • Diallo kukabana koo na Mabina
  • Chegeni apeta, Kamani naye kugombea Uenyekiti wa Mkoa wa Simiyu
  • Lowasa yumo
  • Ridhwani na Salma hawana wapinzani
  • Gachuma, Mathayo, Makongoro wamo Mara
  • Le Mutuz kugombea Dar
  • Chenge hana mpinzani Bariadi
  • Nagu na Sumaye kutoana jasho Hanan'g
  • Karamagi Aibuka upya kusaka Uenyekiti wa Wilaya huko Kagera
  • Bulembo, Martha Mlata na Cpt Balongo Kuwania M/Kiti Wazazi Taifa
  • Ngoma Nzito Viti 3 Wazazi Bara wamo Manyanya, Tizeba, Zungu, Kawawa na Nyawazwa
  • Mwendesha Mijadala ya TV Mayrose kupimana Ubavu na Kilango VS Sophia Simba UWT Taifa
 

Attachments

  • NEC.pdf
    132.5 KB · Views: 1,835
  • UVCCM.pdf
    35.6 KB · Views: 1,149
  • UWT.pdf
    79.1 KB · Views: 1,051
  • VITI10.doc
    29.5 KB · Views: 834
  • WAZAZI.pdf
    32.8 KB · Views: 854
Hakujatulia sana hapa si unajua maamuzi haya kama yalivyokwishasemwa jana ni magumu na kuna majabali yameenguliwa ila tutayaanika muda si mrefu baada ya kuanza tu kusomwa
 
CCM chama makini sana ninajua watatuleta viongozi safi wenye nia njema na nchi yetu.
 
Nitakwenda kwa mtindo wa kutaja maeneo ambayo yalikuwa na fukuto la kisiasa tu mengine tutakutana nayo katika mjumuisho wake baadaye nikashatulia vema, tazama mabadiliko katika Uzi hapo juu kwa updates.

Karatasi ni moja tu ngoja niidurufu kuwapa na wadau wengine kisha nikae na nakala pembeni kuendelea kufunguka zaidi
 
Majina nimeishayaona anachofanya JK ni kumtengenezea njia swaiba wake Lowassa.
nani kakuuliza umeyaona au ujayaona unaa tu ili uonekane wewe upo mbona hukutumbia kama uliyaona
 
Back
Top Bottom