List ya Watu Maarufu Waliowahi Kuchepuka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
Unakumbuka mkasa wa Bill Clinton na Monica Lewinsky au François Hollande na Julie Gayet.
Kati ya skendo kubwa za usaliti zilizowahi kuwakumba viongozi miaka ya hivi karibuni ni Bill Clinton akiwa rais wa Marekani na François Hollande akiwa Rais wa Ufaransa. Yalizungumzwa yakaisha lakini yanabaki kwenye historia.

1. ARNOLD SCHWARZENEGGER
Mwaka 1991, mwigizaji na Gavana Mstaafu wa Jimbo la California, Marekani, Arnold Schwarzenegger pamoja na aliyekuwa mke wake kwa kipindi hicho, Maria Shriver walimwajiri Mildred Baena kama msaidizi wa nyumbani.

Hata hivyo, kumbe nyuma ya mgongo wa mke wake, Schwarzenegger alikuwa akitoka kimapenzi na Baena ambaye naye pia alikuwa ni mke wa mtu kwa kipindi hicho na uhusiano huu wa siri, ulifika mbali zaidi ambapo Baena alibeba ujauzito ambao ilithibitika kuwa ni baada ya miezi tisa, mtoto alipozaliwa, ilithibitika kuwa ni wa damu ya Schwarzenegger.

Kwa sababu hiyo, Baena aliachana na mume wake ambaye alikuwa akidhani kuwa yeye ndiye muhusika wa mimba aliyoibeba mkewe, wakati Arnold naye alikubali kwamba yeye ndiye baba wa mtoto aliyezaliwa na Baena na akapewa jina la Joseph.

Mwaka 2011 baada ya Arnold kumaliza muda wake wa ugavana, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kwamba alimuweka wazi mke wake kuhusu mtoto aliyezaa na Baena, hiyo ikiwa ni miaka zaidi ya miaka, na pia iliripotiwa kwamba kwa kipindi chote hicho Arnold alikuwa akimuhudumia mtoto wake kwa siri jambo ambalo linadaiwa kuwa lilisababisha mke wake kuomba talaka na wakatengana mwaka huo.

2. TIGER WOODS
Anatajwa kama ni miongoni mwa wacheza gofu waliopata mafanikio makubwa kimichezo na kiuchumi pia.
Mwaka 2010 Woods alitalakiana na mke wake Elin Nordegren ambaye alizaa naye watoto wawili huku sababu ya kuachana kwao ikithibika waziwazi kwamba ni mchezo mchafu wa kuchepuka alioufanya Woods.
Kilichotokea ni kwamba, mwaka 2009 Elin aligundua kuwa Woods anachepuka na mwanamke aitwaye Rachel Uchitel na kwa mujibu wa simulizi za Elin mwenyewe, anasema arobain za mwizi zilitimia usiku ambao Woods alikuwa nyumbani amelala.

Elin akachukua simu ya mume na kuanza kupekua ambapo alikuta meseji ya mume wake kwenda kwa Rachel ikisema: “Wewe ni mtu wa pekee niliyewahi kumpenda.”
“Nimekumiss.” Elin akatuma meseji nyingine ya namna hiyo akijifanya ni Woods ambapo baada ya muda, Rachel alijibu kwa kuuliza lini wataonana tena.

Tangu hapo hakukuwa na msalie mtume, Elin akamuamsha mume na nyumba ikawaka moto.
Hata hivyo, mwaka 2010, Tiger Woods alikiri kosa mbele ya vyombo vya habari na ndani ya mwaka huo huo walitalakina na Elin.

3. KEVIN HART
Kevin Hart ni muigizaji wa Marekani ambaye naye ni mmoja wa mastaa waliojaribu kuchepuka lakini kwa bahati mbaya wakanasa na siri zikavuja.
Kwa sasa Kevin ni mume na baba wa watoto wawili wawili aliozaa na mke wake Eniko Parrish ambaye pia ni mjamzito.

Mitandaoni ilisambaa video inayomuonyesha Kevin Hart akiwa mtupu chumbani na mwanamke ambaye si mke wake. Kwa lugha nyepesi, alikuwa akichepuka.
Hata hivyo Hart alijaribu kupinga kile kilichosambaa lakini kwa muda mfupi sana alishindwa kuendelea kusimamia uongo wake na aliamua kukiri na hata kuomba radhi kwa mke wake, watoto, mashabiki na watu wake wa karibu kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

4. BRAD PITT
Brad Pitt ni muigizaji wa Marekani ambaye aliwahi kuwa mume wa Angelina Jolie. Lakini kabla ya kuwa na Angelina, Brad Pitt alikuwa ni mume wa muigizaji Jennifer Anniston ambaye walitalakiana mwaka 2005 baada ya Brad kutokuwa muaminifu kati ndoa yake. Brad Pitt alikuwa akichepuka na Angelina na kunogewa mpaka alipofumwa.

Brad alichepuka na Angelina Jolie, ambaye walikutana wakati wanatengeza filamu ya Mr and Mrs Smith ambayo waliigiza kama mume na mke.
Hata hivyo, licha ya kwamba mchepuko wa Brad Pitty ulifanikiwa kuwa mke, kwa sasa hawapo pamoja tena kutokana na kutengana mwishoni mwa mwaka 2016.

5. DAVID BECKHAM
Mume wa mke mmoja na baba watoto wanne. Ni mwanasoka mstaafu aliyetamba mwanzoni mwa miaka ya 1990 hadi 2003 alipokuwa akiitumikia timu ya Manchester united.
Mwaka 2003 alisajiliwa na timu ya Real Madrid ya Hispania na alipoanza kazi huko alikutana na mrembo Rebecca Roos ambaye baadae akawa mfanyakazi wake akimtumikia kama msaidizi binafsi.

Baadaye iligundulika kuwa Beckham na Rebeca sio tu walikuwa ni mtu na bosi wake, bali pia walikuwa wanatoka kimapenzi. Baada ya Rebeca kuacha kazi kwa Bechkam mwaka 2004, alifichua siri hiyo katika gazeti la News to The Word… hata hivyo, Beckahm hakuibuka kupinga juu suala hilo wala kukiri jambo ambalo linawafanya watu waunganishe nukta na kupata jibu. Beckham alikuwa na nafasi ya kutumia mahakama ili labda kulipwa fidia ya kuchafuliwa na gazeti lililochapisha habari hiyo.

6. KRISTEN STEWART
Supastaa wa filamu za Twilight, Kristen Stewart alikumbwa na skendo ya usaliti baada ya kufumwa na mwongozaji wake wa filamu za Snow White And Hunts Man, Rupert Sanders.
Kristen aliyekuwa katika uhusiano na mwigizaji mwenzake, Robert Pattinson alijikuta katikati ya dunia ya usaliti baada ya paparazzi kupiga picha akijicinjari ndani ya gari na mwongozaji huyo.

Ni moja kati ya skendo za kukumbukwa kwani Kristern na Pattinson walikuwa wakitajwa kama ‘Power Couple’ wa Hollywood wakilinganishawa na Angelina Jolie na Brad Pitt kwa wakati huo.

7. KRIS JENNER
Mama wa familia ya kina Kardashian, Kris Jenner amewahi kukiri kuchepuka wakati akiwa ameolewa na Robert Kardashian kwamba alifanya mchezo huo akiwa na mwongozaji wa filamu aliyocheza. Jenner alisema: “Ukiwa mdogo unafanya mambo mengi ya kukufadhaisha, ninachojutia ni kuwa nilimsaliti mume wangu.”

8. CHRIS ROCK
Mchekeshaji maarufu duniani Chris Rock aliachana na mkewe baada ya kukiri kuchepuka na mwanamke mwingine. Ndoa yake na
Megalyn Echikunwoke ilivunjika na sasa ameanzisha uhusino mwingine akijiapiza kuwa mwaminifu
 
Nilichojifunza hapo wenzetu kuchepuka kunaweza kukupeleka mahali pabaya ambapo hata hukutegemea na hata kufilisika pia.

Tiger Woods ndio nilimuonea hadi huruma.
 
Wenzetu wana misimamo sababu wanajua hata mkitalikiana kila mtu anae pa kwenda.
Huku bongo tunasameheana na kuvumiliana hasa wanawake wanavumilia sana huu uozo!anajua hapa tukiachana nitaenda wapi na hawa watoto??!!!maskini anabaki kuumia ndani kwa ndani!huu udhaifu wao wanaume tunautumia vibaya sana lakini mwisho muvi huwa haiishi salama
 
Wenzetu wana misimamo sababu wanajua hata mkitalikiana kila mtu anae pa kwenda.
Huku bongo tunasameheana na kuvumiliana hasa wanawake wanavumilia sana huu uozo!anajua hapa tukiachana nitaenda wapi na hawa watoto??!!!maskini anabaki kuumia ndani kwa ndani!huu udhaifu wao wanaume tunautumia vibaya sana lakini mwisho muvi huwa haiishi salama
Bongo kuchepuka tunaona ni jambo la kawaida tu na halina madhala.
 
Hawa wote tunajua habari zao na hazina msisimko.
Tuletee za bongo hasa za wanasiasa na watu wa dini. Mfano. Profesa J. Kapuya ...kipindi kilee
Mheshimiwa fulani au Askofu wa TTTK au Nabii fulani au mkuu wa mkoa wa Rad lete mambo iko musisimuko
 
Nasubiri hapa bongo maana no moja ni yule mtukufu na waziri, katoto ndo kana miezi kama 4 hivi kama sijakosea.
 
Sawa...
Sasa utuweke na list ya watu wa kawaida waliyochepuka😂😂😂

Ova
 
Back
Top Bottom