Lissu, Wenje, Sugu, Msigwa, Kiwia kuunguruma Mwanza, Iringa na Mbeya (soma ratiba)

The Conquerer

Member
Aug 16, 2012
79
94
Wana JF, baada ya kuzuiliwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge, magwiji wa siasa wa CHADEMA ambao ni mwiba kwa serikali ya CCM wameamua kutumia muda wa siku hizo tano kupeleka ujumbe kwa wananchi jinsi CCM na serikali yake wanavyoendesha nchi kibabe na kibaguzi ili wananchi waamue haki ifikapo 2015.

Ratiba:
Jumapili 21/04/2013 watatikisa Mwanza
jumanne 23/04/2013 watarindima Iringa
jumatano 24/04/2013 watatema cheche Mbeya

wana Mwanza, Iringa na Mbeya kaeni mkao wa kula.

Ratiba ya maeneo mengine nitawaletea mara tu ikinifikia.

Pichani ni moja ya mikutano mikubwa ambayo walihutubia siku za nyuma.
 
Wasisahau kuzungumzia bilioni 29 za Presidential Delivery Unit zilizopitishwa baada ya wao kufukuzwa bungeni bila kufuata kanuni.
 
Posho posho wamebuni njia nyingine ya kupata posho kufidia hizo siku tano
 
CCM wanakazi kila siku watalala na viatu,

CHADEMA Wanapiga chenga zaidi ya Zidane! Ukuzuia bungeni hao Ikulu, Ukizuia Ikulu hao kwa Wananchi na Nguvu ya umma.

CHADEMA wanateleza zaidi ya kamabale.
 
hii habari ikiwafikia CCM lazima waweke vikwazo. Naomba RPC wa mikoa hiyo waache ushabiki wa Chama. Mwigulu na watu wenu mkae Mbali kabisa, hatutaki tindikali ktk hii mikutano.
 
hii habari ikiwafikia CCM lazima waweke vikwazo. Naomba RPC wa mikoa hiyo waache ushabiki wa Chama. Mwigulu na watu wenu mkae Mbali kabisa, hatutaki tindikali ktk hii mikutano.

Kwa sasa hawana kisingizio maana nao Kinana na kundi lake linazunguka mikoani.
 
Safi sana Magamba wakibana Bungeni majeshi yanaamia kwa wananchi kma ilvyokua enzi za ZZK na spika Sitta
 
Back
Top Bottom