Nicholas
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 25,260
- 7,195
Ndio shida ya wanaotetea kila kitu katika mfumo: Kupindisha ukweli. Haya ngoja tukusaidie. Dk Kitila Mkumbo hakuwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa kuteuliwa. Yeye alichaguliwa na Baraza Kuu katika kundi la wanaume bara, pamoja na Marehemu Shelembi na Profesa Baregu. Aliongoza kwa kura Profesa Baregu akafuatia Dk Mkumbo.
Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti mpaka sasa hivi ni wanne tu: Chiku Abwao, Marando, Safari na Mbogolo. Mwenyekiti amebakisha wawili. Hao ndio pekee wanaoweza kuvuliwa ujumbe wao na KK.
Ni uungwana kukiri kosa kwamba Mwanasheria wetu Mkuu alichemsha kuwashauri wajumbe wa KK wawafukuze hawa wandugu. Ingekuwa busara kuwaruhusu wajiuzulu kama walivyoomba. Lakini kwa sababu chuki ilitawala wakafanya maamuzi kwa ubabe na jazba. Matokeo yake wamevunja Katiba. La pili alilosema Msando ni kwamba kwa mujibu wa katibu ya CHADEMA huwezi kumhukumu mtu bila (i) kumpa tuhuma zake kwa maandishi (ii) mtuhumiwa ajibu tuhuma kwa maandishi. Yote haya hayakufanyika kwa sababu maamuzi yalifanywa nje ya vikao na KK ilitumika tu kuhalalisha.
Hili wala sio Msando tu. Hata Marando alijaribu kushauri ndani ya KK lakini wapi bwana kwa sababu ndani ya CDM mwanasheria pekee anayeheshimika ni TL.
Hapa makao makuu hali si shwari. Baada ya mkutano wa akina ZZK jana mambo ni magumu. Wakurugenzi wapo baridi sana, hasa Mrema na Kigaila. Wengine wanacheka, wakisema kwamba tuliwaambia huyu TL msimwamini ataua chama. Haya mambo ndiyo hayo sijui huko mbele kuna nini...
Kwa nini kinatangulia barua ya kufukuzwa au kikao kilichomfukuza?