Uchaguzi 2020 Lissu ashtushwa na kitendo cha viongozi wakuu wastaafu kuhodhi ardhi kubwa sana na kupelekea migogoro ya wakulima na wafugaji nchini

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,606
51,514
Katika hali ya kuendelea na wito wake wa kuliponya Taifa kupitia kusema ukweli mchungu, Ndugu Tundu Lissu amewaeleza wananchi wa Ifakara na Kilombero mshtuko mkubwa alioupata baada ya kufahamu ardhi kubwa sana ya mkoa wa morogoro kumbe inahodhiwa na viongozi wakuu wa nchi wastaafu.
Lissu amesema amekuja kufahamu kuwa familia ya Mzee Mwinyi, Marehemu Mkapa na Sumaye wanamiliki maefu ya Eka katika mkoa huo wa Morogoro.

Ndugu Lissu amesema, kitendo hicho cha kuhodhi ardhi kinapelekea wananchi kukosa ardhi ya kilimo na ufugaji na ndiyo maana migogoro ya wakulima na wafugaji haiishi mkoani humo.

Lissu amesema Kama Chadema itaingia madarakani, miongoni mwa vitu vya kwanza kuvifanya mkoani humo ni kutwaa maelfu hayo ya ardhi na kuwagawia wananchi.

Katika suala hili la wastaafu kujimilikisha maelfu ya Eka za ardhi mkoani morogoro hatujaona rais Magufuli akigusa maelfu ya ardhi za marais wenzie wastaafu, tunataka rais Magufuli kabla ya uchaguzi wa october achukue hatua mara moja kutwaa ardhi hizo na kuwagawia wananchi ili kuondoa migogoro ya ardhi mikoani humo. Hii tabia ya kulindanalindana haiwezi kulisaidia Taifa kupiga vita ufisadi!

Kumbe sasa nimeelewa kwa nini wastaafu wanahaha kumsaidia Magufuli arudi madarakani, KUMBE ANAWALINDA!.

Naona sasa Taifa kupitia Tundu Lissu limepata mtu mkweli, mweledi, Jasiri na mzalendo!

Kwa habari zaidi Angalia Video hii ya Lissu
 

Attachments

  • VID-20200913-WA0029.3gp
    12.7 MB · Views: 1
Mtasubiri sana yaani Lissu awe Amiri jeshi duuuu!!!!!!.Kwanza kwa kura ngapi??? Hizo 200000 anazotarajia kupata
 
Kumbe ndio maana migogoro ya wakulima na wafugaji haiishi na hakuna hatua zozote za kuitatua wahusika ni hao hao.
 
Piga sana hizo
IMG_20200908_161108.jpg
 
Mtasubiri sana yaani Lissu awe Amiri jeshi duuuu!!!!!!.Kwanza kwa kura ngapi??? Hizo 200000 anazotarajia kupata
Hahaha inaonesha wewe ni mnafiki sana. Bashiru mwenyewe anakubali gemu la Lissu wewe kabwela unapinga nini?
 
Back
Top Bottom