Elections 2010 Lisa M Rockerffeller urge Tanzanians to reject Kikwete a 2nd Term

Status
Not open for further replies.
Wadau,
Kuna dada mmoja toka familia ya Rockerffeller amemvamia Rais Kikwete kwenye facebook Yake. amewachamba na wapambe wake kisawasawa. anadai familia yake imetoa michango mingi tanzania na kusaidia NGO's na serikli lakini hawaoni hela zao zilipokwenda. Anawaonywa watanzania kutokumpigia kikwete Kura

Someni hapa We're in last day... | Facebook

Moderator wa Facebook page ya JK AMEFUTA comments zote za Lisa Rockerfeller! LOL

Wanaogopa nini? Si watashinda tu huo Urais? Kazi kwenye Ubunge na Udiwani. HUKO hawana chao!

Halafu huyo Ernesto Sheka asijifanye mnjanja! Tushamshtukia! LOL
 
Mtu umeoa bado unakaa kwenye nyumba ya baba yako, baba yako ndiye anayekununulia chakula, nakukupa posho, anakununulia wewe, mkeo na watoto wako nguo, anawasomesha watoto wako, anakulipia umeme na maji na akiugua yeyote katika familia yako, yeye ndiye anayelipa. Wewe na mkeo hamfanyi kazi bali mnajisifia kuwa mzee wenu tajiri. Hivi siku baba akikuambia kuwa uache kulewa ovyo, usiwachape bila sababu watoto wako na usimpige mkeo utatanua kifua na kumwambia kuwa asikuiingilie katika himaya yako? Himaya gani hiyo!

Sisi tunapitisha kibakuli hata kuomba vyandarua, madawati, kuchimbiwa vyoo na visima n.k. Sisi tunapigiwa muziki ili hao mnaowaita wakoloni watusamehe madeni ambayo kweli tulikopa na tumeshindwa kurudisha ( ati.. we will pay them!)! Leo, miaka 50 baada ya uhuru, sehemu kubwa ya bajeti yetu wanaibeba hao tunaowaita wakoloni! Sasa hizo responsibility mnazojivunia ziko wapi? Mtu ambae ni responsible hata siku moja hataki kuwa tegemezi maana anajua athari zake. Utasemaje unapoenda kuomba misaada ( na sio mikopo) ati si kwa sababu mnataka kuwa watumwa! Mngejua hivyo basi mngehakikisha mnajitegemea na mnaweka mazingira ambayo wenyewe watawabembeleza kuwekeza. Hapo watawaheshimu. Hakuna mtu anayemheshimu mtembeza kibakuli! Tukubali makosa yetu na tujifunze kutokana nao. Tusipofanya hivyo tutabaki watu wakuonewa huruma na kudharauliwa.

Amandla.....

Ni kweli.

Pride si lolote si chochote kama vitendo vyetu ni vya 'baba suruali'.

Na kama wadau wengine walivyoongea sioni ubaya wa mtu kukushauri, hususan pale anapoona unataka kufanya makosa. Protokali zinaweza kuwa vimevunjwa ingawa huyo 'mzungu' ameji-identify kama 'activist' huwezi ukalinganisha ukubwa wa kosa na yale aliofanya yule VP wa Kenya.
 
whatever the case may be...................nimechukia sana huyu mzungu alivyom-compare JK na Mugabe.............JK atuachie sisi wenyewe tumkome nyani giladi.................

Kaka,

Nadhani wewe ni mmoja wa wale wapambe wa mfalme, wanaomwambia kila siku kapendeza, kumbe YUKO UCHI! Nawajua sana watu wa aina yako. Mnajipendekeza kwake ili MPATE ULAJI WENU! Hamna lolote!

Kubali kuambiwa ukweli, kwamba MFALME YUKO UCHI, AVAE NGUO!

JK hana tofauti kubwa sana na Mugabe. Anayo yake, ila kichinichini. Najua hata mimi naweza "kupotezwa" kiaina, na hakuna atakayenitetea. Mugabe yeye hajali, anafanya wazi wazi. Kama unadhani tuna demokrasia Tanzania, tembelea kituo chochote kile cha polisi, uone jinsi UDIKTETA unavyofanya kazi. Tanzania ni moja ya nchi ambazo HAZIHESHIMU haki za binadam. Ukikamatwa, kwa tuhuma yoyote ile - iwe ya kweli au ya uongo - na kupelekwa kituo cha polisi, ole wako, labda ukutane na watu walio na busara, lakini ukiwapata wale AROOO, basi, sahau kwamba UKO HURU!

UHURU GANI HUU wanaouzungumzia, huku kila siku tunaweka ndani watu wasio na makosa? Wengine wanakaa zaidi ya miaka KUMI bila kupelekwa mahakamani?

Sasa hapa kuna DEMOKRASIA au UDIKTETA?

Tuache unafiki! MNAKERA NYIEEEEEE!
 
- Mkuu ninajadili hoja muhimu kwa taifa langu as a Great Thinker, sio maneno maneno ya mitaani ambayo hayawezi kulisaidia taifa langu, ninasema hivi Mkoloni ajali mambo ya taifa lake la US, ya ndani ya Tanzania aniachie mwenye mwananch wa Tanzania.

William.

Mkuu, I have read all your threads and frankly speaking you cannot last a minute in any debate....you are repeating words Mkoloni, Mkoloni and it is redundant....you have not made your case at all. First of all, Ukoloni is not one person but a system, hence there is no way this Lisa can qualify to be a mkoloni. She is an independent person who has experienced the life of ordinary poor tanzanians (although she is neither ordinary nor poor) she has seen the potential that is Tanzania vs the actual governance shortcomings here. In addition, lets ask ourselves, don you think that this Lisa has any personal grudges against the President? No, because she does not and will not need anything from him. She has plenty and it is easy for her to ignore all this and spend her money on herself or other causes. But NO....ana uchungu wa kuona mamilioni ya watanzania wanaishi kwenye abject poverty when the country is endowed with plenty of wealth. I submit
 
Kwasasa watanzania tayari wameshasema kwa vitendo (KURA)kuwa hawataki utawala wa Kisultani na wa KIMLA wa hawa ma-ccm NA family zao!
Haya yote mengine mwachieni W.Malecela&cO...Huku ni vitendo zaidi, waacheni wenye kubwabwaja!
 
- Hao wazungu wangetuachia mambo yetu ya ndani tutayaamua wenyewe, wao wazungu mabaya waliyotufanyia Africa sio madogo eti, huyu mdada anasahau kwamba ni wizi wa familia yake kwa taifa lake ndio uliopelekea kuanzishwa kwa sheria ya Standard Act, ili kuzuia monopoly za wizi wa familia yake kwa wananchi wa US, sasa kama yeye ni mkweli angeanza kuwarudishia serikali ya US na wananchi wake hela walizoiba huko mpaka kuanzishiwa sheria.

- Africa bwana tunakuaga so desparate na ushindi wa uongozi kwamba hata huwa hatuulizi maswali magumu, halafu baadaye ndio tutakuja kuanza kutafutana uchawi, huyu dada hana moral authority yoyote ya kutufundisha wa-Tanzania kuhusu uzuri na ubaya wa viongozi wetu, kwa sababu tunayajua vizuri matatizo yetu, yeye na familia yake warudishe zile hela zote walizowabia wananchi wenzao huko US through biashara zao za mafuta na ngano!

Ahsanteni.

William.
Moral authority ndio nini, the truth 'll remain so regardless to the source! To me I dont think it is wise to start questioning her moral authorility in this matter, besides, it is her grand parents that did the deeds. She is now trying to share what was accumulated to poor people! Kama kitu ni kibaya hata ukikipamba vipi bado kitaendelea kuwa hivyo.
Cha msingi tujaribu kuangalia kile alichokuwa anasema kama kina ukweli ndani yake au la na sio kumshambulia, if at all u want to qualify as one of us (great thinkers)!
Yeye alitaka ku'share' her own experience about Kikwete!:A S-baby::A S-baby::A S-baby::A S-baby:
 
Mtu umeoa bado unakaa kwenye nyumba ya baba yako, baba yako ndiye anayekununulia chakula, nakukupa posho, anakununulia wewe, mkeo na watoto wako nguo, anawasomesha watoto wako, anakulipia umeme na maji na akiugua yeyote katika familia yako, yeye ndiye anayelipa. Wewe na mkeo hamfanyi kazi bali mnajisifia kuwa mzee wenu tajiri. Hivi siku baba akikuambia kuwa uache kulewa ovyo, usiwachape bila sababu watoto wako na usimpige mkeo utatanua kifua na kumwambia kuwa asikuiingilie katika himaya yako? Himaya gani hiyo!

Sisi tunapitisha kibakuli hata kuomba vyandarua, madawati, kuchimbiwa vyoo na visima n.k. Sisi tunapigiwa muziki ili hao mnaowaita wakoloni watusamehe madeni ambayo kweli tulikopa na tumeshindwa kurudisha ( ati.. we will pay them!)! Leo, miaka 50 baada ya uhuru, sehemu kubwa ya bajeti yetu wanaibeba hao tunaowaita wakoloni! Sasa hizo responsibility mnazojivunia ziko wapi? Mtu ambae ni responsible hata siku moja hataki kuwa tegemezi maana anajua athari zake. Utasemaje unapoenda kuomba misaada ( na sio mikopo) ati si kwa sababu mnataka kuwa watumwa! Mngejua hivyo basi mngehakikisha mnajitegemea na mnaweka mazingira ambayo wenyewe watawabembeleza kuwekeza. Hapo watawaheshimu. Hakuna mtu anayemheshimu mtembeza kibakuli! Tukubali makosa yetu na tujifunze kutokana nao. Tusipofanya hivyo tutabaki watu wakuonewa huruma na kudharauliwa.

Amandla.....
You really qualify to be among us (great thinker)
Umatonya unapenda, ukielekezwa namna ya kuacha umatonya ujitegemee unakuwa mbogo, eti unaniingilia uhuru wangu, what kind of uhuru are talking about??? Lisa just gave a valuable and genuine opinion!!!!!!!!!!!!
It is shame:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
 
Cdanganyiki na mzungu kuionea huruma tanzania tena mmarekani? hata kidogo jamani, nilikuwa nikifuatilia hoja zao kwa makini hawa wanamashairi wawili, huyo binti na mpinzani wake, habari za kuaminika ni hizi "rokafella ni kweli familia ya kitajiri marekani na babu mkwere ktk kutafuta nafuu ya maisha kwa wabongo hasa kipindi kile cha njaa aliitisha mkutano marekani na wabongo waishio huko, pamoja na wafanya biashara wenyenia ya kuwekeza nchini ktkt kuisadia jamii, hasa ktk afya, na elimu,huyo mneene(rokafelaa) tayari mwanaye alikuwa na kijiproject mbeya, hivyo inavyosemekana, jamaa alikubali kumwaaga minoti kupitia NGO ya mwanae lakini consideration ilikuwa mplace mzee kat viunga vya mbeya for investment with taxfree for a period of time, lakini jamaa kamzunguka kupitia maafisa wa usalama baada ya kugundua huyo demu alikuwa anafanya vitu kama vya mapanki(darwin's nightmare), ndipo mkwere kamywa ndani ya nchi bwana kapewa masaa tu, na misaada yake yote iko chini ya upekuzi mkali, mihasira yake ndio kaitafuta page ya mzee mkwere kabandika, malumbano yameanza zamani lakini kavizia sasa, kazi kwenu wabogo, kikulacho kiko ktk chupi yako mwenyewe.
 
Lisa is right, haingilii mambo ya ndani ya nchi, anasema ukweli. Wala hajaomba ubunge, na wala hataki mashangingi yenu. CCM ni mafisadi na wanapandia mgongo wa wajinga!!!!!!!!!!!!!! ndio wanawapigia kura!
 
Ninaosoma hizi hoja za wengin, akina Malecela, ndiyo nazidi kukata tamaa juu ya nchi yangu. Hawa ndio Creem of the cream ya jamii ya Watanzania na mawazo yao yako hivi! Needless to say about those millions who have just seen school doors for a period of seven years (designated by th CCM as the pinnacle of the majority of Tanzanians' education). Sasa huyu Malecela, I know he was born with a golden spoon in his mouth, haoni taabu na mateso ya kujitakia ya Watanzania? Aniambie, ametembelea nchi yeyote duniani inayofanana na Tanzania kwa taabu za wananchi wake? (Including countries involved in civil wars since Adam). Kila anachogombania ni uhuru! Unajua maana ya uhuru? Ni Watanzania wacheche sana wako huru (your type). Acha kuwa indifferent ka mateso ya watu. Kama husumbuliwi na moyo wako (moral) kuon watu hawamudu hata mlo mmoja, acha wenye moral waseme. Hatumind hata akiwa Kaburu!
 
We Malecela,usiseme lolote!kama Wazungu wabaya mbona uko States,rudi kwenu Mvumi uone Wagogo wenzako wanavyo sota na poverty ya hali ya juu!

I tell you,Richmond,BoT towers,Patel & Co,Chenge na vijisenti sio Wazungu hawa.Hii blame game ya Wazungu ni upumbavu.
Malecela umefaulu matunda ya elites wa CCM/TANU ,ole wako uanzishe tawi la CCM huko DC,maybe Malecela Sr atakuja kufungua tawi hilo.
 
Mkuu, I have read all your threads and frankly speaking you cannot last a minute in any debate....you are repeating words Mkoloni, Mkoloni and it is redundant....you have not made your case at all. First of all, Ukoloni is not one person but a system, hence there is no way this Lisa can qualify to be a mkoloni. She is an independent person who has experienced the life of ordinary poor tanzanians (although she is neither ordinary nor poor) she has seen the potential that is Tanzania vs the actual governance shortcomings here. In addition, lets ask ourselves, don you think that this Lisa has any personal grudges against the President? No, because she does not and will not need anything from him. She has plenty and it is easy for her to ignore all this and spend her money on herself or other causes. But NO....ana uchungu wa kuona mamilioni ya watanzania wanaishi kwenye abject poverty when the country is endowed with plenty of wealth. I submit

- Mkuu heshima yako sana, well unasema I have not made a case at all, lakini umekuja kunjibu hoja yangu ya msingi kwamba mkoloni atuachie mambo yetu ya ndani na ya uongozi wetu hayamuhusu, yanatuhusu sisi wananchi wa Tanzania. Sio yeye aliyetuambia kwamba wabunge na madiwani gani wanafaa ni sisi wenyewe ndio tumeamua.

- Again ninaomba kurudia hivi huyu Lisa, ajali mambo ya uongozi wa taifa lake, aende kule Harlem walikochagua corrupt leader mwenye kesi bungeni lakini wamemchagua anyways, sio Lisa aliyetuambia kwamba Mramba mwenye keei mahakamani hafai tumeamua wenyewe wananchi, ndio maana ninasema huyu Lisa mkoloni abaki na ukoloni wake huko huko USA!

William.
 
Ninaosoma hizi hoja za wengin, akina Malecela, ndiyo nazidi kukata tamaa juu ya nchi yangu. Hawa ndio Creem of the cream ya jamii ya Watanzania na mawazo yao yako hivi! Needless to say about those millions who have just seen school doors for a period of seven years (designated by th CCM as the pinnacle of the majority of Tanzanians' education). Sasa huyu Malecela, I know he was born with a golden spoon in his mouth, haoni taabu na mateso ya kujitakia ya Watanzania? Aniambie, ametembelea nchi yeyote duniani inayofanana na Tanzania kwa taabu za wananchi wake? (Including countries involved in civil wars since Adam). Kila anachogombania ni uhuru! Unajua maana ya uhuru? Ni Watanzania wacheche sana wako huru (your type). Acha kuwa indifferent ka mateso ya watu. Kama husumbuliwi na moyo wako (moral) kuon watu hawamudu hata mlo mmoja, acha wenye moral waseme. Hatumind hata akiwa Kaburu!

- Mkuu wangu naomba nikupe mfano mdogo sana wa kwa nini huyu Lisa asiruhusiwe kutufundisha what to do na viongozi wetu, kule Harlem USA wamechagua mbunge ambaye ana kesi bungeni ya corruption na Lisa hakusema kitu, leo sisi wanaanchi wa taifa hili tumempiga chini Mramba mwenye kesi pia kama huyo wa Harlem, sasa huoni my point brother kwamba huyu Lisa apuuuzwe tu maana hana lolote la maana kwa taifa letu!

- Mengine ni haki yako kusema maana yanakuja na terriotry ingawa huwezi ku-provide evidence lakini haina tatizo unajua katika hii kazi ya kuelimishana kuhusu taifa letu, ni lazima tutegemee haya! jifunze kutoogopa majina ya watu ni majina tu!

William.
 
We Malecela,usiseme lolote!kama Wazungu wabaya mbona uko States,rudi kwenu Mvumi uone Wagogo wenzako wanavyo sota na poverty ya hali ya juu!

I tell you,Richmond,BoT towers,Patel & Co,Chenge na vijisenti sio Wazungu hawa.Hii blame game ya Wazungu ni upumbavu.
Malecela umefaulu matunda ya elites wa CCM/TANU ,ole wako uanzishe tawi la CCM huko DC,maybe Malecela Sr atakuja kufungua tawi hilo.

- Hiii imenichekesha sana ha! ha! ha! sasa what my location has to do na mawazo yangu? I mean mkuu ni this June nilikuwa Mvumi ni kweli kuna wananchi wasio na uwezo na walionao, infact hata huku USA kuna wananchi wenye uwezo na wasionao,

- wazungu wabaya hayo ni maneno yako sio yangu, nilichosema na ninarudia tena ni kwamba Lisa mzungu ajali mambo ya uongozi wa taifa lake ya taifa letu atuachie wenyewe, kwenye uchaguzi huuu ulioisha tumeonyesha kwamba tunaweza kuamua mambo yetu wenyewe bila kuambiwa na wazungu kama Lisa, ambao kule kwao Harlem wananchi wamechagua kiongozi mwenye kesi na hawezi kusema kitu, lakini anataka kutufundisha kuhusu viongozi wetu wasio na kesi, Lisa hafai kabisaaa ni mkoloni anayetaka kurudi kuja kututawala, wananchi tukatae kwa nguvu moja kwamba hatutaki!

Wazungu hao hao ndio wanasupport govt ya baba yako miaka na miaka.
Najua unaenjoy matunda ya Uhuru na dada yako pia huko state,naomba umwambie arudi kutibu macho wagogo huko mvumi,maana taxpayers wa Tanzania waligharamikia elimu zenu.

You are real stupid,kumpinga huyo Lisa,eti kwa kuwa ni mzungu.
Najua nyie watoto wa elites wa CCM,mtatetea status quo mpaka kufa,lakini wananchi wanaanza kuelewa what is going on.

Najua unaenjoy matunda ya ufisadi wa CCM,hata msanii wetu akiwa hapo DC,naona huwa mnajumuika pamoja watoto wa status quo.

Umefikia wapi kuanzisha tawi la CCM hapo DC na aliyekuwa balozi wa CCM London,Maajar?
 
- ...nilichosema na ninarudia tena ni kwamba Lisa mzungu ajali mambo ya uongozi wa taifa lake ya taifa letu atuachie wenyewe, kwenye uchaguzi huuu ulioisha tumeonyesha kwamba tunaweza kuamua mambo yetu wenyewe bila kuambiwa na wazungu kama Lisa, ambao kule kwao Harlem wananchi wamechagua kiongozi mwenye kesi na hawezi kusema kitu, lakini anataka kutufundisha kuhusu viongozi wetu wasio na kesi, Lisa hafai kabisaaa ni mkoloni anayetaka kurudi kuja kututawala, wananchi tukatae kwa nguvu moja kwamba hatutaki!

William.
Mkuu mbona unaji-contradict mwenyewe. Unasema wazungu watuachie mambo yetu wenyewe, vema na kweli. Lakini fahamu kuwa huyo Rais wako unayemtetea hapa, kila siku anakimbia kwenda kwa hao hao wazugu unaowapinga hapa--kuwabusu miguu ili walisaidie taifa letu. Hivi unajua kuwa sehemu kubwa ya bajeti ya taifa leu inategemea misaada ya hao wazungu unaowaita wakoloni? Ni kwa kigezo gani basi useme,"mzungu Lisa, tuachie mambo ya taifa letu," lakini hutoi tamko kama hilo kwa wazungu wengine kama Paul Wolfowitz na Robert Zoellick? Na kuhusu tuhuma zako za Harlem, I think hukumuelewa Lisa vizuri kuhusu alichokuwa anakiongelea/zungumzia. Point aliyokuwa ana-make ni kwamba Rais Kikwete ana uwezo duni wa kupambanua mambo; hivyo hafai kuiongoza nchi kama Tanzania yenye wasomi lukuki wenye wepesi wa kutambua/chambua mambo ya kidunia. And you can't just equate member of congress wa huko Harlem na Rais wa nchi. Rais wa nchi ana madaraka makubwa mno (especially kwa nchi kama Tanzania). Plus, huyo Charles Rangel wa Harlem unayemtaja hapa, hakuiba pesa ya mtu ikilinganishwa na ilivyo kwa hawa mafisadi wa CCM walioiba mabilioni ya shillings za walalahoi. Rangel kwa upande mwingine, anashitakiwa kwa kukiuka kanuni za House pamoja na kushindwa kuripoti income ya nyumba yake ya vacation iliyoko huko Dominican Republic. In fact, inasadikiwa kuwa mengi ya mashitaka hayo hayana ushahidi wa kutosha. So please acha kudanganya watu.
 
Ikiwa wewe ni omba omba, mtu amekusaidia several times na kila siku anakukuta bado uko pale Jangwani unaendelea kuomba, jioni unakunywa pombe na kustarehe kama tajiri.Kwanini asiamue kuingilia uhuru wako na kukurudisha kwenu.

Mfano mzuri wa hili ni yule Matonya, kwanini Makamba aliamua kumrudisha Dodoma.
Lisa ana kila haki ya kushauri kwani kamsaidia sana Matonya na haoni kwamba kuna nafuu na usiku Matonya anatesa na bado yuko Dar watoto wako Dodoma na hali ngumu. Kama tuliona Makamba alifanya sawa kwa Matonya iweje leo William ulalamike kwa Lisa?

Au kwa sababu Mzungu? Je mlikataa msaada wake kwakuwa yeye Mzungu au Mkoloni? Hamkujua hilo mwanzoni mlipopeleka bakuli?
 
W. J Malecela, there are two things. There is "what is said" and "who said it" (i.e. the speaker). If "what is said" can stand on its own merit then you need to consider "what is said" regardless of the speaker. The statement, "Murdering is bad", is true even if it was uttered by Satan himself. In my opinion what was said by Ms. Rockerfeller is true and stands on its own merit. "Who she is" has no bearing on whether "what she said" is true or not! Furthermore, all human beings are entitled to have an opinion about any subject and they should be able to express that opinion freely.

Haka ka point kako ka "...ajali mambo ya uongozi wa taifa lake..." kana maana gani? Are you trying to say that it is impossible for her to have an opinion about CCM and the election in Harlem at the same time? Naomba ufafanuzi. Akikujibu kuwa she was also against the election of the so called corrupt leader in Harlem utajibu nini? You need to seriously examine cerezo's advice to you. I recommend you read books about ancient Greek philosophers.
 
- Hiii imenichekesha sana ha! ha! ha! sasa what my location has to do na mawazo yangu? I mean mkuu ni this June nilikuwa Mvumi ni kweli kuna wananchi wasio na uwezo na walionao, infact hata huku USA kuna wananchi wenye uwezo na wasionao,

- wazungu wabaya hayo ni maneno yako sio yangu, nilichosema na ninarudia tena ni kwamba Lisa mzungu ajali mambo ya uongozi wa taifa lake ya taifa letu atuachie wenyewe, kwenye uchaguzi huuu ulioisha tumeonyesha kwamba tunaweza kuamua mambo yetu wenyewe bila kuambiwa na wazungu kama Lisa, ambao kule kwao Harlem wananchi wamechagua kiongozi mwenye kesi na hawezi kusema kitu, lakini anataka kutufundisha kuhusu viongozi wetu wasio na kesi, Lisa hafai kabisaaa ni mkoloni anayetaka kurudi kuja kututawala, wananchi tukatae kwa nguvu moja kwamba hatutaki!

William.

Haujacheka lolote, ukweli ni kwamba kama hautaki wazungu, rudi kwenu Tanzania. Hacha kung'ang'ania nchi yao!

Waluachie uongozi gani, wakati kila siku Tanzania (Kikwete) anaongoza wenye njaa kuja kuomba hela? Kwa hiyo wao wanufaishe famili ya makamba, Malecela na Kikwete wakati wanadnganywa kwamba hela ni kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote?

Hata mimi nitasema ninapotoa hela na zisitumike vinavyostahili. Kwa hiyo William mimi nashuku sana, your mental stability, seriously. You have some issues and needs to see psychiatrist
 
- Hiii imenichekesha sana ha! ha! ha! sasa what my location has to do na mawazo yangu? I mean mkuu ni this June nilikuwa Mvumi ni kweli kuna wananchi wasio na uwezo na walionao, infact hata huku USA kuna wananchi wenye uwezo na wasionao,

- wazungu wabaya hayo ni maneno yako sio yangu, nilichosema na ninarudia tena ni kwamba Lisa mzungu ajali mambo ya uongozi wa taifa lake ya taifa letu atuachie wenyewe, kwenye uchaguzi huuu ulioisha tumeonyesha kwamba tunaweza kuamua mambo yetu wenyewe bila kuambiwa na wazungu kama Lisa, ambao kule kwao Harlem wananchi wamechagua kiongozi mwenye kesi na hawezi kusema kitu, lakini anataka kutufundisha kuhusu viongozi wetu wasio na kesi, Lisa hafai kabisaaa ni mkoloni anayetaka kurudi kuja kututawala, wananchi tukatae kwa nguvu moja kwamba hatutaki!

William.

Malechela Malechela unasema Lisa atuachie ya watanzania kwasabu unawapenda watanzania au kwasabu comments zake zinatishia kitumbua cha familia yako?
Watu walioshindwa kutawala au uongozi husingizia ukoloni huku wanatembeza mabakuli kwa haohao wanaotaka tuamini ni wabaya. Wanafiki kwelikweli.

Alichokiongea Lisa tunakiongea hata watanzania hapa hvo coni cha ajabu. Anyway what Lisa dozn know is that this a a continent of dead brains n morals.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom