Lipumba,mbatia,Mrema,na Cheyo kuingia katika meli inayozama?

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Katika siku za karibuni viongozi hawa wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kuishambulia chadema,eti chadema inahatarisha amani nchini,lengo lao kuu limekuwa ni kuinusuru serikali ya JK na CCM
Pamoja na wao kufikiri zimwi likujualo halikukuli ukaisha,je wana uhalali wa tena wa kushirikiana na ccm kuishambulia chadema mpinzani mwenzao na wao wakajiita wapinzani?
Wamedhihirisha kukerwa na umaarufu wa chadema kuliko ufisadi wa ccm
watahukumiwa na historia
 
Mkataa umoja mchawi...
na kila mtakia mama wa kambo shari, balaa humfika *****!
Wanasiasa wa Tanzania ni Wabinafsi, walevi wa madaraka na sifa...
hapana tofauti baina ya hivi vyama venu vya siasa mnavoviabudu na kuvitukuza....
VYOOTE NI USANII MTUPU kama ule WIMBO WA MJOMBA!!
BADILIKENI ILI VYAMA VYENU VIBADILIKE...
KINYUME NA HIVYO MTAENDELEA KUTOFOANA MACHO CCM INAPETA!
Mwisho wa siku mtakuja na singo iliyozoeleka "tumeibiwa... tumechezewa rafu!"
 
Wanachofanya kinastahili pongezi kwa kuwa kinatupunguzia utitili wa vyama vya briefcase, Hii ina maana tutabaki na vyama viwili tu yaani CCM na CHADEMA just like Democrat and Republican. Kwa maneno mengine ni kwamba CUF, NCCR, TLP, UDP vimejifia vyenyewe rasmi.

Sasa nimeanza kukubali maneno ya John Tendwa aliwahi kutamka huko nyuma kwamba hata vyama vya upinzani wakati mwingine huwa vinaoneana wivu !
 
Back
Top Bottom